tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Aliyekuwa mtangazaji nguli wa BBC Swahili, Bi Zuhra Yunus ametundika daruga za utangazaji wa BBC tangu Ijumaa tarehe 14/01/2022 na kuhamia rasmi Azam TV kama Mkurugenzi mpya kuchukua nafasi ya Charles Hillary aliyeteuliwa na Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar kuwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Ikulu. Zuhra ameondoka BBC baada ya kuitumikia idhaa hiyo kwa kipindi cha miaka 14. Tukumbuke kwamba Charles Hillary naye alitokea BBC kabla ya kuja Azam TV. Karibu nyumbani Bi Zuhra.
Katika kazi zake za uandishi wa habari na utangazaji akiwa BBC, Zuhra amewahi kuwahoji watu mashuhuri wakiwemo marais, wasanii na wanasiasa mbalimbali. Mmojawapo wa wanasiasa waliowahi kuhojiwa naye ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Paramagamba Kabudi (a.k.a Profesa Majalala) kama unavyoweza kumsikia kwenye kipande cha mahojiano hapo chini.
MAONI YANGU
Binafsi namkubali sana mtangazaji huyu nguli kutoka anga za Tanzania na ninamjivunia sio tu kwa kuwa ni mtanzania mwenzangu bali kwa sababu ya kazi yake ya utangazaji iliyotukuka. Kwa kweli ameipeperusha vema bendera ya Tanzania. Ni nadra sana kumpata mtangazaji mwenye karba ya Zuhra hapa nchini.
Nawasilisha.