Wakuu salama?
Nadhani mmeona mkeka wa mama, Zuhura Yunus kaondolewa kutoka kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu mpaka kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Zuhura atakuwa kamkorofisha wapi mama mpaka katolewa Ikulu? Au ndio anapikwa kuja kuwa Waziri baadaye?
Kuna mtu alidokeza X Zuhura anataka kuondolewa... je, kuna fukuto nyuma yake? Baadhi ya majirani zetu Kenya walimpa za uso Zuhura baada ya details za mkopo wa Korea kuvuja. Je, hii ndio inaweza kuwa sababu?
=====
Pia soma: Rais Samia afanya uteuzi na mabadiliko ya watendaji wa Serikali. Zuhura Yunus aondolewa Ukurugenzi wa Mawasiliano Ikulu
MKOPO wa KOREA umemuondoa ZUHURA IKULU.
“It's dangerous to be right when the government is wrong”; ‘ni hatari kuwa sahihi wakati serikali imekosea’, maneno ya mwandishi na mwanafalsafa wa kifaransa, François—Marie Arouet "de plume Voltaire",
THE 48 LAWS OF POWER, Robert Green, Law number 1: Never Outshine The Master, (Act less smarter than your boss, Present your ideas in a way that they echo your boss's thought, Discreet flattery is very powerful.)
Robert Green anataka uwafanye walio juu wajisikie wenye nguvu na mamlaka, katika kuwafurahisha na kuwapendezesha hakikisha hauoneshi kipaji chako chote, usifanye zaidi ya wakubwa zako,
Kanuni hii inataka usiwe na weledi, ujuzi, utaalamu zaidi ya mabosi zako, sheria hii inaeleza, ukitaka kufanikiwa mbele ya mabosi (watawala) hakikisha unamsifia bosi, unamsafisha na kumpongeza. Uchawa.
Tuelewane. Binafsi, sipo hapa kumtetea mtangazaji wa kwanza mwanamke kutangaza BBC Swahili, Bi. Zuhura Abdallah Yunus, @venusnyota, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu
Nipo hapa kuwaeleza sababu za Bi. Zuhura Yunus Abdallah kufurushwa na kuwa ‘demoted’ kutoka katika viunga vya IKULU hadi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Walemavu.
Bi. Zuhura Abdallah Yunus ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu
Taarifa ya Mwisho ya Bi. Zuhura Yunus akiwa kama Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu (Director of Presidential Communications, State House) ni 02 June, 2024 anuani yake Chamwino, Dodoma.
Taarifa kwa umma (press release) hiyo ambayo ilitolewa na Bi. Zuhura Yunus Abdallah ilihusu Tanzania kupewa mkopo wa TZS 6.7 bilioni na kutoa sehemu ya bahari na ardhi yenye madini kwa Korea Kusini.
Taarifa ya Ikulu Mawasiliano iilikuwa na kichwa cha habari “TANZANIA, KOREA SIGN FRAMEWORK AGREEMENT FOR $2.5 BILLION CONCESSION LOANS”. Hiyo ilikuwa ni taarifa kwa umma 02/06/2024
Pamoja na Bi. Zuhura Yunus Abdallah kujitahidi sana kuipaka ‘icing sugar’ taarifa hiyo, isinuke kinyesi kibichi cha mkopo wenye masharti ya kutoa ardhi na bahari kwa Korea Kusini, bado Zuhura amefyatuliwa.
Mnajiuliza, icing sugar gani kwenye kinyesi? Taarifa ya Bi. Zuhura Yunus Abdallah iliweka neno “CONCESSION LOANS” ili kupunguza makali ya mkopo huo ambao umekaa kinyonyaji na sura ya kimangungo.
Concessional loans: Loans that are extended on softer terms than market loans, either through interest rates below those available on the market or by grace periods, or a combination of these. Umeelewa?
“Tanzania & Korea have signed a framework agreement that will enable TZ to obtain concessional loan from the economic development cooperation fund (EDCF) worth $2.5 billion over the next five years”
Hadi hapo, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu alikuwa ametoa taarifa kwa umma kwamba Serikali ya Tanzania imekopa TZS 6.7 trilioni kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Korea. Wajibu wake ni huo.
“The two heads of state held official talks at the Yongsan Presidential office & also witnessed the signing of other agreements that aim to bolster cooperation in critical minerals & blue economy”
Kwamba, viongozi walifanya mazungumzo rasmi ofisi za Rais, Yongsan na kushuhudia utiaji saini mikataba mingine ambayo inalenga kuimarisha ushirikiano katika madini muhimu na uchumi wa bluu.
Kuonesha msisitizo, akaandika Rais Samia ameomba ushirikiano na Serikali ya Korea katika sekta mahususi ikiwepo uchumi wa bluu (blue economy) na maendeleo ya gesi asilia (development of natural gas)
Bi. Zuhura Yunus Abdallah akawa ametimiza wajibu wake wa kuujulisha umma kuhusu mikataba ambayo imesainiwa na Serikali ya Tanzania katika ziara ya Korea Kusini. Wapiga spana tukapata nyenzo.
Wahafidhina ndani ya mbogamboga hawakupenda. Wao wakaanzisha vurumai, Bi. Zuhura Yunus Abdallah aondolewe IKULU na apangiwe shughuli nyingine kwa kuwa anahujumu shughuli za IKULU.
Hii iliwafanya wapambe wa Serikali, machakaramu wa CCM na watawala kutoka ndani ya Serikali kuingia mitandaoni rasmi kuanza kukanusha taarifa iliyotolewa na Voice of America (VOA) na REUTERS.
Balozi wa Tanzania - Korea Kusini, Togolani Mavura, alikwenda mbali zaidi na kuwataka Voice of America (VOA) waondoe taarifa yao na pia waombe radhi kwa kuwa wanafanya upotoshaji, wamedanganya.
Kitila Mkumbo, Waziri wa Uwekezaji, alikwenda katika chapisho langu, akasema ni taarifa ni uongo na akatoa maelezo ya kibwanyenye bila facts. Tukamuomba mkataba, akalaza kipara, hakurudi kamwe.
Jokate Mwegelo, Katibu Mkuu wa UVCCM, akajitokeza na kueleza faida za mkopo wa TZS 6.7 trilioni kutoka Korea Kusini, tukamuuliza, huo mkataba umefanikiwa kuona au unatupa hadithi? Akalaza komwe.
Ummy Mwalimu na Nape Nnauye pia. Wakawaulizwa kama wanao mkataba wa mkopo, wapewe wasome ili waone ni kitu gani Serikali imeweka rehani. Unajua hao wawili ni ‘low voltage’, hawakurudi.
Arirang TV (Korea) katika habari zao, News Day, wakatoa taarifa za mkopo huo wa TZS 6.7 trilioni ($2.5 billion) na baadhi ya mikataba iliyosainiwa. Wakawa wameokoa jahazi sana. Spana zikapigwa sana.
Akaunti za ‘maroboti’ CCM na Serikali (zilizomshughulikia Chongolo) zikaanza kuchapisha taarifa kwamba Zuhura Yunus hafai kwamba anahujumu Serikali na Ikulu ya Rais SSH.
Kandarasi imefanywa hadi na mtangazaji wa WASAFI, anayeshinda na Earpods, katika kipindi cha Radio amekwenda kusema "idara ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilipwaya" akachapisha na ujumbe huo X.
Kandarasi ikavuka hadi mipaka, wakapewa hadi tweeps kutoka nchi jirani ya Kenya, wakibeba ujumbe huo kwamba Bi. Zuhura hatoshi na kwamba anamuhujumu Rais. Na maandishi yao, ujumbe unafanana.
Siku nne tangu taarifa ile ya Bi. Zuhura Yunus Abdallah itoke kwa umma kuhusu mkopo wa TZS 6.7 trillioni na mambo ya bahari, uchumi wa bluu na masuala ya gesi asilia, Zuhura akafyatuliwa 06/06/2024.
Bi, Zuhura Yunus amefyatuliwa katika mkeka ambao umetiwa saini na katibu mkuu kiongozi, na mkeka huo umemteua Milton Lupa, ambaye ni marehemu kuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri.
Ni kama, IKULU wamemueleza kwa vitendo Bi. Zuhura. Tumecheza 'blunder' kwanini ukawasanue raia? Kwanini uandike taarifa ya ukweli? Kwanini usidanganye? Adhabu yako, kahudumie walemavu sasa.
Hivyo, Zuhura Yunus sasa atakuwa anapangiwa majukumu katika ofisi ya Waziri Mkuu, na siyo tena bosi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais- Ikulu. Ni dhambi sana kuwa sahihi wakati serikali inakosea.
NB; awamu mbili za utawala wa JPM na SSH, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu wanahitaji 'mpambe nuksi' kama Gerson Msigwa, kiumbe ambaye anaweza kusema Mlima Everest upo Tanzania
Martin Maranja Masese, MMM.