Zuhura Yunus wa BBC Swahili, amesema maisha ya London Magumu huwezi hata kusevu

Zuhura Yunus wa BBC Swahili, amesema maisha ya London Magumu huwezi hata kusevu

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Akihojiwa kupitia EATV live, Kilikuwa kipindi kizuri hasa ukiangalia ile kombinesheni ya wadada hawa wawili yani Da Salama kama mnavyo mjua na Da Zuhura wakiwa pamoja mezani na Da Salama anavyomchimba kumtaka ya ndani na nje. Mahojiano yalikuwa mazuri sana kwani Da Salama anajaribu kumchimba Zuhura ambaye anaakili sana namna anavyojibu maswali ya Salama.

Kiukweli walijadiliana mengi sana lakini mimi nimeyaona mawili kuwa ya muhimu, yaani uchumi na mahusiano. Kiuchumi Zuhura alikuwa anasema kuwa maisha ya London ni magumu sana ukilinganisha na hapa bongo (Dar), na amekiri kuwa na wakati mgumu kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao wamekuwa hawaelewi maisha ya London. Nilivyomwelewa kuna baadhi ya jamaa huwa akirudi wanamtolea macho kumtoa mchuzi wakidhani anamihela mingi, yaani maisha yake wanayatafsiri kwa kumwangalia kupitia runinga anavyo waka mtoto.

Da zuhura alikuwa anajaribu kutoa ufafanuzi wa gharama za maisha kama kulipia televisheni (ching'amuzi) chaneli kama laki 3 za kibongo kwa kadirio la chini kwa mwezi, kodi ya nyumba alisema iko juu sana, sikumwelewa vizuri lakini alikuwa anamaanisha inachajiwa kwa siku yaani kama huku basi umeenda zile gesti za kibongo za buku 50 au 60 hivi, hina kuwa kama 1,800,000/= kwa mwezi. Na ieleweke kuwa kule London unapohamia katika nyumba unabeba nguo zako tu, tofauti na huku Bongo mtu akihamia katika nyumba aliyopanga anabeba mpaka fuso inajaa wakati mwingine anarudia. Kwa Londoni kila kitu unakikuta ndani mpaka vijiko unavikuta.

Pia tofauti na uku unalipa chumba umeme na maji kule ni vyote vipo ila kimeongezeka kingine, kinaitwa gesi, na kina kazi zaidi ya kupikia nayo pia huwezi kuishi bila hiyo na ipo juu vile vile.

Maji amesema pia yapo juu, yaani bili ya maji London iko juu, lakini kunasheria kali Uingereza hairuhusiwi kumkatia mtu maji hata kama hajalipa bili ya maji tofauti na Bongo, hapa DAWASA wanang'oaga mpaka bomba lote wakibeba mita.

Hivyo dadetu ambaye ni mzaliwa wa hapa hapa mchangani leo ametoa ufafanuzi huo na kukiri kuwa kusevu ni ngumu sana, hivyo msimchukulie poa anapambana na hali yake.

Salama alipotaka kujua kuhusu maswala ya mahusiano yake binafsi kama kawaida alitumia engo nyingi na ndefu za kiswahili, nilimsikia Salama akisema sasa maisha umesema ni magumu lakini nasikia mtu akiwa na mpenzi huwa wanasaidiana maisha huko si kama huku bongo kuna vibenten (Salama alikejeli) ndipo Zuhura akaingia katika 3 zake na kusema kule Uingereza kugawa majukumu ni pasu pasu hakuna kukwepa hata kama una mshahara mdogo majukumu hayajui hilo.

Ndipo salama akamdondoshea swali pale pale kuwa vipi wewe umeolewa na una watoto, chakushangaza Zuhura bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno akajibu hana mume bado anatafuta, na anamwomba Allah apate mume.

Jamani kwa wale mnaojua Zuhura wa BBC hana mume anatafuta na ameonyesha hamu ya kuolewa na mtanzania mwenzake. Mimi mtoto wa mchungajia tayari nilisha oa na kanisa limetwambia mke mmoja tu hivyo mimi nashusha udende kazi kwenu.

Mtoto wa mchungaji.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Screenshot_20210613-020018.png
 
London ni moja ya jiji kubwa duniani lenye watu wa mataiga karibu yote duniani.na watu wengi wanaokuja uingereza lazima watembelee huo mji.

Bei ya kupanga nyumba kwa private landlords ni ghali sana maana chumba kimoja kinaweza anzia pounds 400-500 (shs mil 1.3 - mi 1.5)

Nyumba za bei affordable ni z council, nazo kupata kwake ni mlolongo mrefu kidogo ila njia rahisi ya kupata ni ukiwa umeoa halafu mkeo mjamzito/una mtoto mdogo hivyo unapewa priority hivyo unapata nyumba kutokana na gender za watoto (kama una watoto 2 ke na me basi unapewa ya vyumba 3...kama una mtoto mmoja unapewa ya vyumba 2)

Bei za kupanga kwenye nyumba z council ni kuanzia pounds 400-500+, hivyo utaona jinsi ilivyo rahisi.

Fahamu kuwa nyumba z council sio mbaya, ni nzuri n zipo maeneo tofauti tofauti(unaweza fananisha na nyumba za nhc kwa bongo )
Kwenye suala la kipato, mkazi wa london analipwa zaidi kwa kazi hiyo hiyo ambayo mwenzake wa nje ya london anaifanya (mfano police wa london analipwa mshahara mkubwa kuliko police anayeishi nje ya London)

Suala la kuzichanga ni wewe mwenyewe. Sikubaliani na zuhura juu ya hilo. Inabidi uwe na discipline ili uweze kutoboa (hii ipo popote ulimwenguni).
 
Yap ukweli wa majuu, tuchaguwe wenyewe, bongo au kule, kipato kikubwa, ila matumizi nayo makubwa mno, kila kitu pasu kwa pasu na mpenzi wako, hakuna kuleta zile za nifulie au pika na asafishe nyumba sababu ni demu, sheria nayo msumeno, ukimgusa demu waondoka wewe hasa kama mna watoto, bado weather, miezi 9 baridi ya kibabe, 3 kajoto fulani ka geresha, duh..
 
Yaan para 3 mantiki hamna mzee vp unatuchosha.[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Inawezeka yapo juu Ila mshahara Ni mkubwa pia mwalimu wangu alisoma kule masters alisema kikombe Cha kahawa mjini London Ni sawa na elf 80,000 za kitanzania ...
Na wewe ukaamini huo uongo [emoji3][emoji3]
 
kwa nini Jiji la DSM na lenyewe lisiwe ghali, tupandishe bei kodi za nyumba, hoteli n.k ili jiji letu liendane na majiji makubwa duniani.
 
Back
Top Bottom