Zuhura Yunus wa BBC Swahili, amesema maisha ya London Magumu huwezi hata kusevu

Zuhura Yunus wa BBC Swahili, amesema maisha ya London Magumu huwezi hata kusevu

Inawezeka yapo juu Ila mshahara Ni mkubwa pia mwalimu wangu alisoma kule masters alisema kikombe Cha kahawa mjini London Ni sawa na elf 80,000 za kitanzania ...
na sahani ya chakula ni laki 6 siyo? Tafuta hela na ww uende London ukatembee ili siku nyingine usidanganywe
 
TZS haiwezi kuwa na thamani kubwa kuliko Pound popote duniani hata kuzimu. Labda tuzungumzie kuhusu Purchasing Power Parity (PPP) kwa Pound ikiwa UK na equal value yake in TZS ukiwa Tanzania.
Kama Andazi bongo ni sh 100 na andazi hilo UK ni pound 2 sawa na Tzs 7000. Hela ipi ina thamani?
 
Kama Andazi bongo ni sh 100 na andazi hilo UK ni pound 2 sawa na Tzs 7000. Hela ipi ina thamani?
Pale London wapi wanauza maandazi, tena ya 7000? Toa mfano wa vitu vinavyojulikana, kilo ya nyama ya ng'ombe hapa Dar na London. Weka factor kwamba wao hawafugi sana bali wanasafirisha. Kisha weka bidhaa inayotoka kule na ikaja kwetu mfano Range Rover. Linganisha bei
 
TBC wangelipa mishahara ya laki 7, watangazaji wao wasingefutuka kiasi kile! Ni zaidi ya kunenepa!

Mimi naona watangazaji wanatumia platform yao ya kujulikana kupata madili nje ya mishahara,sidhani kama wanalipwa mishahara hiyo....Bahasha za kaki ,kuwapaisha mapedeshee ,ueMC ndi unaowaweka mjini.
 
Pale London wapi wanauza maandazi, tena ya 7000? Toa mfano wa vitu vinavyojulikana, kilo ya nyama ya ng'ombe hapa Dar na London. Weka factor kwamba wao hawafugi sana bali wanasafirisha. Kisha weka bidhaa inayotoka kule na ikaja kwetu mfano Range Rover. Linganisha bei
Screenshot_20210613-152751.png

Mfano angalia hapo bei ya chakula kwenye restaurant ya kawaida Pound 25 (Tshs 75,000) alafu ulinganishe na bei ya bongo ambayo haizid Tshs 7500 (pound 2.5). Hapo hela ipi ina thaman.
 
Nimejaribu kuchunguza,

Kwa Wanawake wengi wa kiafrika kupata mume nchi za ULAYA Ni ishu ngumu Sana.

Wengi Sana wanarudi bongo wakiwa single na umri umeshawatupa mkono.

Nadhani ile ishu ya 50% kwa 50% imeleta shida Sana kule.

Vijana hawazitaki kabisa pingu za maisha.
Wanawake wa kizungu ile 50% 50% wanaipractice kwa vitendo na sio maneno. So mwanaume akiwa committed huwa ni rahisi kuishi nao. Wanaume wengi wa kiafrica wakienda majuu huwa hawapati kazi kuishi na wanawake wa kizungu sababu wanapenda kuhudumia mwanamke anaejitoa kwa kile anachopata na kuwa muwazi na matumizi yake.

Ila mziki wanawake wetu wa kiafrika, mambo ya haki sawa ni mdomoni, ukimwambia kushare cost utaitwa kila majina ya lawama na dharau. Wakienda majuu wanatafuta wanaume wenye pesa na kuishi nao kama wadangaji.

So that's why wengi huwa wanafeli mahusiano huko majuu sababu ya kukwepa 50% responsibility ya familia. Imagine mwanamke wa kibongo kuolewa halafu mwanaume anakwambia kwa kila kitu utalipia 50%.

Maandamano yake hadi ustawi. Ila bado wanahangaika kusema wanaume wa bongo ni bahiri kisa hampatii pesa ya kiwango anachotaka yeye.
 
View attachment 1817425
Mfano angalia hapo bei ya chakula kwenye restaurant ya kawaida Pound 25 (Tshs 75,000) alafu ulinganishe na bei ya bongo ambayo haizid Tshs 7500 (pound 2.5). Hapo hela ipi ina thaman.
Hela yenye thamani hapo ni Pound, kwa units zake 25 (£25) unapata chakula kwenye mgahawa. TZS ina thamani ndogo, kwa units zake 7500 (7500TZS) unapata chakula mgahawani. Thamani ya sarafu inakuwa kubwa ukitumia kiasi chake kidogo kununua kitu kilekile ambacho utatumia kiasi kingi cha sarafu nyingine kununua kitu kilekile.

Ndio maana tangu mwanzo nakwambia wewe huzungumzii thamani wala nguvu ya hela, bali unazungumzia Purchasing Power Parity (PPP).
 
Akihojiwa kupitia EATV live, Kilikuwa kipindi kizuri hasa ukiangalia ile kombinesheni ya wadada hawa wawili yani Da Salama kama mnavyo mjua na Da Zuhura wakiwa pamoja mezani na Da Salama anavyomchimba kumtaka ya ndani na nje. Mahojiano yalikuwa mazuri sana kwani Da Salama anajaribu kumchimba Zuhura ambaye anaakili sana namna anavyojibu maswali ya Salama.

Kiukweli walijadiliana mengi sana lakini mimi nimeyaona mawili kuwa ya muhimu, yaani uchumi na mahusiano. Kiuchumi Zuhura alikuwa anasema kuwa maisha ya London ni magumu sana ukilinganisha na hapa bongo (Dar), na amekiri kuwa na wakati mgumu kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao wamekuwa hawaelewi maisha ya London. Nilivyomwelewa kuna baadhi ya jamaa huwa akirudi wanamtolea macho kumtoa mchuzi wakidhani anamihela mingi, yaani maisha yake wanayatafsiri kwa kumwangalia kupitia runinga anavyo waka mtoto.

Da zuhura alikuwa anajaribu kutoa ufafanuzi wa gharama za maisha kama kulipia televisheni (ching'amuzi) chaneli kama laki 3 za kibongo kwa kadirio la chini kwa mwezi, kodi ya nyumba alisema iko juu sana, sikumwelewa vizuri lakini alikuwa anamaanisha inachajiwa kwa siku yaani kama huku basi umeenda zile gesti za kibongo za buku 50 au 60 hivi, hina kuwa kama 1,800,000/= kwa mwezi. Na ieleweke kuwa kule London unapohamia katika nyumba unabeba nguo zako tu, tofauti na huku Bongo mtu akihamia katika nyumba aliyopanga anabeba mpaka fuso inajaa wakati mwingine anarudia. Kwa Londoni kila kitu unakikuta ndani mpaka vijiko unavikuta.

Pia tofauti na uku unalipa chumba umeme na maji kule ni vyote vipo ila kimeongezeka kingine, kinaitwa gesi, na kina kazi zaidi ya kupikia nayo pia huwezi kuishi bila hiyo na ipo juu vile vile.

Maji amesema pia yapo juu, yaani bili ya maji London iko juu, lakini kunasheria kali Uingereza hairuhusiwi kumkatia mtu maji hata kama hajalipa bili ya maji tofauti na Bongo, hapa DAWASA wanang'oaga mpaka bomba lote wakibeba mita.

Hivyo dadetu ambaye ni mzaliwa wa hapa hapa mchangani leo ametoa ufafanuzi huo na kukiri kuwa kusevu ni ngumu sana, hivyo msimchukulie poa anapambana na hali yake.

Salama alipotaka kujua kuhusu maswala ya mahusiano yake binafsi kama kawaida alitumia engo nyingi na ndefu za kiswahili, nilimsikia Salama akisema sasa maisha umesema ni magumu lakini nasikia mtu akiwa na mpenzi huwa wanasaidiana maisha huko si kama huku bongo kuna vibenten (Salama alikejeli) ndipo Zuhura akaingia katika 3 zake na kusema kule Uingereza kugawa majukumu ni pasu pasu hakuna kukwepa hata kama una mshahara mdogo majukumu hayajui hilo.

Ndipo salama akamdondoshea swali pale pale kuwa vipi wewe umeolewa na una watoto, chakushangaza Zuhura bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno akajibu hana mume bado anatafuta, na anamwomba Allah apate mume.

Jamani kwa wale mnaojua Zuhura wa BBC hana mume anatafuta na ameonyesha hamu ya kuolewa na mtanzania mwenzake. Mimi mtoto wa mchungajia tayari nilisha oa na kanisa limetwambia mke mmoja tu hivyo mimi nashusha udende kazi kwenu.

Mtoto wa mchungaji.
Hivi kikeke kamwacha kweli
 
Vijana wa jf kuna kipindi walikuwa wanammendea huyu dada Zuhura Yunus.
Haya sasa fursa hiyo wazee wa kazi
 
Duu..
Inawezeka yapo juu Ila mshahara Ni mkubwa pia mwalimu wangu alisoma kule masters alisema kikombe Cha kahawa mjini London Ni sawa na elf 80,000 za kitanzania ...
 
London maisha ni magumu sana sana hata wazungu wanapaogooa !!! Niliwahi kwenda UK nikaishi Hereford and Reading(spelling) kidogo maisha yapo chini!!! Nilimuuza mwenyeji wangu ambaye ni mwalimu akaniambia kipato chake kwa mwezi !!!!!! Kwetu ni kiimua mgongo!!!
Hapo nilipoweka wino mzito labda alikudanganya huyo mwenyeji wako. Hakuna Mwalimu London anayelipwa zaidi Pound 5,000 (Tshs. 16,360,976.82) kwa mwezi. Hata wakuu wa shule hawafiki hiki kiasi. Wanalipwa Pound 4,500. Unless awe amefikia seniority level 10 na kuendelea hawa wapo wachache sana wanafikia mpaka Pound 9,000 kwa mwezi lakini kati kati ya jiji. Hoja ya kiinua mgongo umeongeza chumvi.

Hii hapa chini ni mapendekezo ya mishahara ya chama cha waalimu jiji la London baada ya Corona kutandika mwaka jana kulingana na eneo lako la kazi kama kati kati ya jiji (inner) , pembeni (outer) au swekeni (fringe). Hawa ni waalimu wenye madarasa (class teacher) na sio wasaidizi (assistant class teacher). Hii mishahara ni kwa mwaka.

1623618047139.png
 
HAPANAAAAA... nilimsikia vizuri sana akihojiwa, alisema She is Single and Happy to be in such situation.

Kifupi ameridhika na ana Amani kuwa single

Angekuwa anataka si angeshanikubali vile nampendaga sana

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kiukweli Zuhura ni mzuri sana kuanzia sura mpaka sauti ndani sijui lakini ni ngumu kupata muoaji, huko Ulaya wala Afrika sababu ya kazi yake, alivyokuwa anaongea ni kuwa anasafiri sana tena duniani ni ngumu kumaliza wiki mbili home sasa jiulize kunamwanaume gani anapenda kununua ugonjwa wa moyo kwa bei ya dola.
 
Back
Top Bottom