DocJayGroup
JF-Expert Member
- Jan 17, 2020
- 1,654
- 3,346
Kila mwaka, Marekani inatoa makazi ya kudumu kwa watu 50,000 kupitia mchezo wa bahati nasibu. Mchezo huo, unachezwa kuanzia mwanzoni mwa mwezi Oktoba hadi Mwanzoni mwa mwezi Novemba. Leo hii, Serikali ya Marekani imetangaza kwamba waTanzania wote watazuiliwa kwenda Marekani kupitia bahati na sibu hiyo. Kuzuiwa huko kutaanza tarehe February 22. Kwa hio kama ulishinda mwaka jana, basi wahi ubalozini sasa hivi upate viza yako ya kukupatia makazi ya kudumu USA, kabla ya hio tarehe ambapo ndio waTZ watazuiliwa. Serikali ya Marekani haijasema sababu halisia ya kufanya hilo.
Pamoja na Tanzania, nchi ya Sudan nayo imezuiliwa viza hio ya bahati na sibu. Nchi 2 nyingine za Afrika za Eritrea na Nigeria zimepigwa nyundo kali Zaidi ambapo wamezuia aina zote za visa zinazomruhusu mtu kuishi na kufanya kazi Marekani.