Zuio Kwa WaTZ: Wahi Ubalozi wa USA Kabla haijala Kwako Kama Ulishinda Viza ya Kukupa Makazi ya Kudumu Marekani

Zuio Kwa WaTZ: Wahi Ubalozi wa USA Kabla haijala Kwako Kama Ulishinda Viza ya Kukupa Makazi ya Kudumu Marekani

Halafu kama Nimesoma mahali,kuwa Hii bani haitahusisha Watu wanaoenda Kupata Matibabu,watalii,Wanaofanya Nazi,nk,
Ila ni Immigrants tuu,na watu wanaoenda kwa Muda!
Nisahihishe kama nimekosea!

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi kabisa. Hata immigrants, kama umeoa au kuolewa na raia wa USA bado unaruhusiwa, au kama umepata kampuni inakufadhili green card, bado unaruhusiwa. Ni hiyo tu ya Dv visa basi. Kwa hio sio mbaya sana, tatizo ni kwamba kuwa katika hio list ndio tatizo sababu inafungua a can of worms ya matatizo mengine tu.
 
Wamarekani tumeifanya nchi kama mbingu.

Halafu tumejipa uungu.

Ukifanya dhambi, tunakukataa kuingia mbinguni.

Ukiwa na passport haieleweki, huingii mbinguni.

[Sarcasm]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani ina viza za aina mbili kuu. Aina ya kwanza, inamfanya mtu anakuwa na karibu haki zote kama raia (immigrant visa), na ya pili haimpi haki na anatakiwa kuondoka USA muda wa visa ukiisha (mtalii, viza ya biashara, mwanafunzi nk).

Makonda amepigwa marufuku kabisa kwa asilimia zote viza za aina zote. Eritrea na Nigeria wamepigwa marufuku viza zote hizo za immigrant visas. Katioa immigrant visas pia ina aina tofauti, kwa Tanzania tumepigwa marufuku visa inaitwa Dv Lottery visa ambayo mtu unaipata kwa kucheza hio bahati nasibu.

Kwa hio kwa waTz, bado unaweza kuomba visa kama wewe unaenda kusoma, kutalii nk. Ila kwa ujumla, mambo yatakuwa magumu kwa waTz. Kwa hio mtu ni kwenda ubalozini ukiwa uko fiti kwelikwelii
Umejibu vema Mkuu,ila Kuna Sehemu nilisahahu kuuliza,
Vipi Kuhusu Diplomatic, je Waziri say mambo ya Nje anaweza kwenda USA?
Au kwa ufupi Diplomatic officials?
Pili,MTU ataweza kwenda Marekani kubeba Maboksi? Namaanisha kufanya Kazi USA?
Mengine na Athari zake nilikuelewa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamarekani tumeifanya nchi kama mbingu.

Halafu tumejipa uungu.

Ukifanya dhambi, tunakukataa kuingia mbinguni.

Ukiwa na passport haieleweki, huingii mbinguni.

[Sarcasm]

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio hivyo ndugu. Mimi personally naishi nusu nusu kati ya USA na Tanzania. Na nakuambia sijutii kamwe uamuzi wangu wa kuishi USA pia. Imenifundisha mengi sana kuhusu maisha, biashara nk. Inaitwa exposure. Mtu ukikaa tu tanzania maisha yako yote, kuna vitu unakosa kujifunza, Na USA imekuwa ni nchi nzuri sana kwa weusi kuishi, lakini kwa sasa kwa kweli baada ya Trump kuwa rais, hali imebadilika na immigrants tunaonekana kama kero. Kwa hio tunapambana kwa kweli tuwekeze Tanzania ili tuondoke kimoja kimoja kama mambo yakikubali Tz. Japo hiyo nayo ni challenge nyingine, sababu mambo tz kufanikiwa inachukua muda mara nyingine.
 
Umejibu vema Mkuu,ila Kuna Sehemu nilisahahu kuuliza,
Vipi Kuhusu Diplomatic, je Waziri say mambo ya Nje anaweza kwenda USA?
Au kwa ufupi Diplomatic officials?
Pili,MTU ataweza kwenda Marekani kubeba Maboksi? Namaanisha kufanya Kazi USA?
Mengine na Athari zake nilikuelewa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wafanyakazi wote wa serikali ya Tz wanaweza kuomba viza ya kusafiri kwenda USA. Aliyepigwa marufuku ni P Makonda tu. Ila sasa ubalozi nao una ruhusa ya kumnyima viza mtu yeyote pamoja na viongozi wa serikali kama ubalozi unaona mtu ni duwanzi. Unaweza pia kufanya michakato ya kuishi na kufanya kazi USA. Njia mojawapo rahisi zaidi ni kupata mke mmarekani, njia ya pili rahisi zaidi ni kusafiri USA kusoma, na wakati ukisoma unaomba vibali vya kazi nk. Siku hizi sio kirahisi kama zamani, lakini bado inawezekana.
 
Hizi ban huwa zinafutwa?

Kama ni ndiyo, ni baada ya muda gani?

Au kuna vigezo mpaka mtimize kama nchi ndiyo ban ifutwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ban huwa zinafutwa?

Kama ni ndiyo, ni baada ya muda gani?

Au kuna vigezo mpaka mtimize kama nchi ndiyo ban ifutwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes. Inaonekana sababu ya Tanzania kuwa kwenye hii list ni serikali ya marekani iliomba tanzania ishirikiane nao kwenye mambo ya uhamiaji ila wakashindwa kuonyesha ushirikiano huo. Hio report niliisoma kwa gazeti la New York Times online pamoja na BBC online. Tz kama itafanya vile wametakiwa wafanye, watatuondoa kwa hii orodha. Nchi ya Chad ya afrika magharibi, ilikuwa kwa orodha ya kwanza ya mwaka juzi (2017), mwaka jana ikaondolewa kwenye orodha. Ni ushapu wa serikali yetu ndio uta-determine ni haraka namna gani tutatolewa kwa hio list
 
Is this ban retroactive?

Sent using Jamii Forums mobile app
I don't know for sure. We know Paul Makonda's ban is retroactive due to his past actions against humanity. For Tanzania's general ban, I think the government failed to fulfil some inter-country obligations with USA, hence being placed on this list.
 
Nafikiri kuna nchi zaidi ya Tanzania zilizo fail hayo mambo ya security obligations.

Ila, ikiwa Wamarekani wanaona uongozi wa Tanzania unavunja misingi fulani, wanaanza na Tanzania kama mfano kwa nchi nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri kuna nchi zaidi ya Tanzania zilizo fail hayo mambo ya security obligations.

Ila, ikiwa Wamarekani wanaona uongozi wa Tanzania unavunja misingi fulani, wanaanza na Tanzania kama mfano kwa nchi nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante na pointi nzuri. Nakibaliana na wewe kwa ulivyosema. 👌👌👌. Na ndio maana wamechukua hatua against PM same day walivyotangaza travel ban. Thoughts nzuri, na asante kuchangia mada
 
Nadhani ameuliza walioomba mwaka Jana ambao wanasubiri majibu, sio waliopata / kuchaguliwa mwaka jana

Sent using Jamii Forums mobile app
Got it! Kweli nimeona matokeo ya waliocheza mwaka jana (DV-2021), bado hayajtoka na yatatoka May 5. Kwa bahati mbaya kwa directives za US government, hao watakuwa na mbinde kupata DV visa sababu ni effective kuanzia February 22, 2020.

Itakuwa maybe matokeo kwa Tanzania wala hayatatolewa. Manake, Tanzania tayari inatolewa kwenye drawing ya lottery ya mwaka jana kwa hio hakuna Mtanzania atakayeshinda. Hio ni assumption yangu tu, na sina uhakika.

Kwa namna yeyote, kama mtu ulicheza mwaka jana, bado usije ukaacha kuangalia matokea Mwezi May. Kama msemo unayosema "It is not over, until it is over." Kwa hio ni muhimu sana kwa mtu aliyecheza kucheki kama ameshinda, na kama umeshinda, hata kama hio ban waTz tumewekewa, bado nenda ubalozini ukajaribu bahati yako.
 
Mkuu, ubalozi hujipangii mwenyewe kwenda hata kama umeshinda. Wana utaratibu wao wa kufuata mpaka wakupangie interview. Haujiamulii mwenyewe.
Asante kwa comment yako mkuu. Leo wote hapa tunajifunza na kuelimishana. Kwa hio mtu ukishinda, hatua inayofuata ni kujaza fomu ya maombi ya viza. Form hio (Form DS-260) inajazwa online. Halafu unasubiri ubalozi ukupatie jibu kuhusu interview date nk. Kwa sasa maybe hata kama mtu umeshinda, na ukajaza hio fomu ya kuomba viza, jibu litakuwa hapana hatuwezi kukupa appointment ya viza interview. Once again, hio ni assumption sababu ya ban hiyo waliyoweka. Thanks again for your inputs.
Ila kwa ufupi, itakuwa kosa kama mtu utashinda DV-2021 halafu usijaze hio fomu. Ni kupambana tu hadi hatua ya mwisho.
 
Kwa uzoefu kwa nchi zilizowahi kupewa ban, ukishinda ukaendelea kujaza form, ukatuma na documents, process zote zitaendelea na interview utapangiwa. Ila kwenye kupata visa ndio inakuwa ngumu. Japo kwa baadhi ya watu wachache saana wa nchi zenye ban wanapewa kitu wanaita waiver. Inawasaidia kuepuka ban.
 
Back
Top Bottom