Tetesi: Zuio la kutafuta mafuta katika visiwa vya Zanzibar

Tetesi: Zuio la kutafuta mafuta katika visiwa vya Zanzibar

Baraghash

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
2,713
Reaction score
1,790
Kuna tetesi kuwa "Mamlaka kuu" imezuia ndege ya kufanya utafiti wa kutafuta mafuta katika visiwa vya Zanzibar.

Inasemekana Rubani wa ndege hiyo alisema walishindwa kuanza kazi kutoka na kuzuia kwa madai kuwa hawana kibali cha kufanya kazi hiyo.

Mwenye taarifa kamili kuhusu ukweli wa kadhia hii auwasilidhe Mkekani ili tutaarifike
 
Zanzibar Ni Nchi Kamili
Huyo Anayezuia Ni Nani?
Mkoloni Tanganyika Ama UN
 
wanalazimisha muungano wakati huohuo wanashindwa kuusimamia ukaleta maslahi kwa pande zote,komaeni zanzibar
 
Hii tetesi umeisikia au kuisoma wapi?
Kiswahili ni lugha yako au ya kujifunza? Hujui maana ya neno tetesi. Waulize JF - Tetesi ni habari ambayo bado haijathibitika lakini inafukuta,inaweza ikawa na ukweli au harufu ya Ukweli
 
Kuna tetesi kuwa "Mamlaka kuu" imezuia ndege ya kufanya utafiti wa kutafuta mafuta katika visiwa vya Zanzibar.

Inasemekana Rubani wa ndege hiyo alisema walishindwa kuanza kazi kutoka na kuzuia kwa madai kuwa hawana kibali cha kufanya kazi hiyo.

Mwenye taarifa kamili kuhusu ukweli wa kadhia hii auwasilidhe Mkekani ili tutaarifike
Hebu acha uchochezi mimi niko Zanzibar na kazi inaendelea! Kumbe Mex. tunaomponza ni sisi. Mex ukiona shida we tulipue tu maana tumezidi!
 
Kazuia nani mkoloni Tanganyika au Serikali ya mapinduzi ya huko nchini Zanzibar.?
 
Taarifa iliopo ni kuwa kitengo cha jeshi JWTZ upande wa anga wamesema kuwa wapo tayar kuishusha ndege itakayo paa anga la Tanzania pasipo kibali
 
Hebu acha uchochezi mimi niko Zanzibar na kazi inaendelea! Kumbe Mex. tunaomponza ni sisi. Mex ukiona shida we tulipue tu maana tumezidi!
Sema kweli wewe upo Zanzibar au Zanzibara? ambae unatuthibitishia kuwa kazi ya utafiti inaendelea kaama kawaida na hakuna matatizo ya Kibali?
 
Taarifa iliopo ni kuwa kitengo cha jeshi JWTZ upande wa anga wamesema kuwa wapo tayar kuishusha ndege itakayo paa anga la Tanzania pasipo kibali

Sikufuata taratibu tu za kupata hicho kibali, maana ulinzi wa anga ni suala la muungano sasa ugumu uko wapi?

Na washawasha!
 
Ulinzi wa Tanzania haupo chini ya Zanzivar
upo chini ya Muungano
lazima Ndege ipate kibali
Usikute ni mpango wa hovyo unafanywa kwa kupitia utafiti
 
Mlitegemea mkoloni wenu akubali myapate hayo mafuta?

Hapo ndipo mtaelewa kwanini watu walikuwa wanataka serikali tatu..

Mtamkumbuka Maalim Seif.
 
Kiswahili ni lugha yako au ya kujifunza? Hujui maana ya neno tetesi. Waulize JF - Tetesi ni habari ambayo bado haijathibitika lakini inafukuta,inaweza ikawa na ukweli au harufu ya Ukweli
Hukujibu swali. Au kiswahili kinakupa shida na wewe? Hiyo "tetesi" umesikia wapi? Chini ya mti au chumbani kwako au kichwani mwako?
 
Back
Top Bottom