Tetesi: Zuio la kutafuta mafuta katika visiwa vya Zanzibar

Hukujibu swali. Au kiswahili kinakupa shida na wewe? Hiyo "tetesi" umesikia wapi? Chini ya mti au chumbani kwako au kichwani mwako?
Swali limejibiwa kitambo ,tatizo lugha ya kiswahili inakupa shida. Soma thread tena kwa utulivu utajua kama ni kitandani, sakafuni au juu ya dari.
 
Tanganyika itaikomesha sana zanzibar , hapo bado kukatiwa umeme !
 
Ikithibitika mleta tetesi habari ulioweka sio kweli utanyakuliwa kwa kuhatarisha Muungano msipende kuleta vitu vya hovyo kwenye mambo sensitive hivi
 
Swali limejibiwa kitambo ,tatizo lugha ya kiswahili inakupa shida. Soma thread tena kwa utulivu utajua kama ni kitandani, sakafuni au juu ya dari.
Umesomeka. Source ya tetesi yako ni either kitandani, sakafuni au juu ya dari.
 
Mnazo ela za kurusha ndege ela za kulipa Tanesco hamna
Nchi yenu mamuzi yao
 
Uwezi kurusha dege bila kibali toka mamlaka usika,je kama ni ndege ya adui?hiyo anga ni ya Tanzania nasio Zanzibar
 
Kama ndege haina kibali si waende tu kwenye mamlaka husika wakapate kibali?kutafuta mafuta sio kigezo cha ndege kuwa juu ya sheria.
 
Huenda ni suala la kiufundi tu.

Hakuna ndege inaweza kuruka kwenye anga ya Tanzania bila idhini ya JWTZ!

Nahisi inaweza kuwa hilo. Jeshi au Ulinzi ni suala la Muungano! Haiwezi kuwa suala la SMZ pekee kuruhusu ndege kuruka
 
Kamu ulivyonukuu kuwa rubani huyo hakuwa na kibali. Jee atarukaje nchi ya watu bila kuwa na kibali stahiki?
 
Huenda ni suala la kiufundi tu.

Hakuna ndege inaweza kuruka kwenye anga ya Tanzania bila idhini ya JWTZ!

Nahisi inaweza kuwa hilo. Jeshi au Ulinzi ni suala la Muungano! Haiwezi kuwa suala la SMZ pekee kuruhusu ndege kuruka
Siyo Kweli, Ndege zote za kiraia zinaruka kwenye anga la tanzania ni lazima zipate kibali toka mamlaka ya usalama wa anga.
Kwa zile ndege zinazofanya utafiti kama wa mafuta ni budi kwanza kupata kibali cha wizara husika na baada ya hapo ni budi kibali toka jeshini kabla kuombwa kibali toka mamlaka ya usafiri wa usalama wa anga. Bila taratibu hizo kufuatwa ni vigumu sana kwa ndege ya kigeni kuruhusiwa kufanya kazi hiyo.
 
Kiswahili ni lugha yako au ya kujifunza? Hujui maana ya neno tetesi. Waulize JF - Tetesi ni habari ambayo bado haijathibitika lakini inafukuta,inaweza ikawa na ukweli au harufu ya Ukweli
Na wewe jifunze Kiswahili, neno "inaweza" si la kuonyesha uhakika wa tukio.
Upande wa pili ni wa kuonyesha uwezekano huo kutokuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…