Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Tanzania ikizuia all imports from Kenya kutulinda raia wake tusisikie mnamlalamikia Meko na nyie
 
Mkuu upo sahihi kabisa. Tatizo letu kubwa tuliachana na sera za Mwl Nyerere za kuwa na ma bwana shamba kila kata au tarafa, unakuta watu wanalima na kuhifadhi mahindi kwa njia zenye kuhatarisha usalama wa chakula. Ni kweli kabisa mahindi, karanga nyingi za Tanzania zina sumu kuvu (aflotoxin) kwa wingi na watu wengi sana wamekufa na wanaendelea kufa. Ukitaka kujua hii issue ni hatari fuatilia kiwango cha cancer kilivyo juu na pia cancer eti mpaka vijijini. Serikali ni wakati wa kutoa ajira kwa watalaamu wa kilimo na mifugo waende huko vijijini
 
Umesahau sakata la mayai toka Kenya?
Nakumbuka pia walivosumbua madereva wetu mpakani.
Teteeni wakenya bt mmesahau they have a lot to lose. They have more producing industries than us na wanahitaji soko la bidhaa zao kutoka Tanzania na Uganda.
Subiri tuone
 
Umesoma jinsi mamlaka za Kenya zinavyopima chakula kinavyoingia nchini Kenya? Unadhani wameanza kupima hivi juzi.
Na lini walilalamika kwa Tanzania au Uganda. hizi sio biashara unaamka asubuhi na kupanga nyanya barabara. Biashara za kimataifa zinafanyika kwa mikataba na majadiliano ya kina.
 
Na lini walilalamika kwa Tanzania au Uganda. hizi sio biashara unaamka asubuhi na kupanga nyanya barabara. Biashara za kimataifa zinafanyika kwa mikataba na majadiliano ya kina.
TBS wakigundua chakula toka Kenya kina sumu,lazima watoe tangazo huku wananchi wanaendelea kuumia na sumu?
 
Mngekuwa mnamtegemea Mungu mkekuwa mnapiga watu risasi hovyo? Mngekuwa mnamtegemea Mungu miili ya watz ingekuwa anawekwa kwenye sandarusi na kutupwa mto ruvu na huko bahari beach? Ni Mungu yupi aliyewaruhusu kuchoma hovyo vifaranga kutoka Kenya? Ni Mungu yupi aliwaruhusu kutaifisha ng'ombe zaidi ya 1000 wa Kenya?.Kwa hiyo mnafanya upuuzi kwa 7bu wazee wetu walitoa ardhi na kusaidia ukombozi wa nchi jirani zetu?

Huu moyo wa kikatili mnaouonyesha siku hizi mmeutoa wapi?Si mlisema hamtishwi sasa Kenya wameagiza mahindi kutoka kwingineko je ninyi na serikali hii ambayo haina mbele wala nyuma mnauwezo wa kununua mahindi yote ya wakulima na wafanya biashara? Mlivamia korosho za wakulima kule kanda ya kusini tena kwa mbwembwe kwamba mtanunua zote matokeo mkaaachia wakulima umasikini wa kutisha.

Kwa hiyo mmelikoroga mnaisingizia chadema kwamba imefurahi kwani wakati mnafanya upuuzi wenu dhidi ya kenya chadema ndo iliwashauri kufanya huo upuuzi? Kumbe tz ni kubwa ina kila kitu kinachowaliza ni kitu gani baada ya kenya kuchukua action? Nchi hii yenye umasikini wa kutupwa serikali kila uchao inazidi kuharibu juhudi za wakulima na wafanya biashara za kutafuta masoko juzi hapa zambia ilipunguza uingizaji kutoka tz mazao ya bustani eg matikiti sikuona juhudi zozote za serikali kuokoa jahazi.

Leo mawaziri wa wizara husika wanalalama kwamba hawajapewa taarifa ya kiofisi kuhusu zuio la mahindi kutoka tz kwenda Kenya inamaana wanadhani Kenya ni Halmashauri ya Buhigwe kwamba haifanyi kitu bila kuiomba wizara ya tamisemi? Huu nao ni upuuzi mwingine.
 
Tbs wakigundua chakula toka Kenya kina sumu,lazima watoe tangazo huku wananchi wanaendelea kuumia na sumu?
Wangeanza na kuondoa sembe yote iliyo madukani na kuwaambia watu wamwage na wasile sembe iliyotoka Tanzania au Uganda. Lakini mpaka muda huu, bado kuna sembe madukani Kenya na majumbani kwa watu iliyotokana na mahindi hayo hayo yanayosemwa yana sumu.
 
Usiwapangie kazi.
 
Wa Kenya wana hoja ya msingi sana na wamezi umbua mamlaka zetu za viwango yaani TFDA, TBS sijui wizara ya kilimo etc mijitu imekaa maofisi na matumbo yao makubwa badala ya kufanya kazi imekalia kusoma magazeti tuu, wengi tunajua hali ya mahindi ki ukweli zile dawa za kuhifadhia mahindi usalama wake kwa binadamu ni mdogo, hata panya hawali mahindi yaliyo puliziwa hizo ‘ETG’ zenu...
 
Tanzania ikizuia all imports from Kenya kutulinda raia wake tusisikie mnamlalamikia Meko na nyie
Tanzania inapashwa kuzuia all imports from kama itadhibitika hazikidhi viwango vyetu sio kwa kulipiza kisasi.
Kwa sasa ni Tanzania kutoka na majibu ya kisayansi juu ya ubora wa mahindi yake bila kuingiza siasa kwenye afya za watu.
 
Tanzania inapashwa kuzuia all imports from kama itadhibitika hazikidhi viwango vyetu sio kwa kulipiza kisasi.
Kwa sasa ni Tanzania kutoka majibu ya kisayansi juu ya ubora wa mahindi yake bila kuingiza siasa kwenye afya za watu.
Acha upuuzi, unga huohuo tunakula watanzania. Nenda Ocean Road kaulize kansa ipi inaongoza na kama ina uhusiano wowote na hizo sumu za unga.
 
Lakini si wamesema mahindi yetu yana sumu, kwanini tusihakiki na kuchukua hatua stahiki?
Kama mahindi yetu hayana sumu hatari zilizodaiwa na Kenya basi tuchukue hatua kwani kwa madai haya wametuharibia kwenye masoko mengine pia, na kama hayana hiyo sumu tajwa basi tuchukue hatua za kisheria na watulipe fidia kwa kutuharibia soko.

Kama ni kweli yana sumu tajwa tuchukue jukumu la kuwaelimisha wakulima wetu jinsi ya kutumia mbolea na kutunza hizo nafaka ili zisipate hiyo sumu kwani pia tutawalinda raia wetu pia.

Sisi Watanzania tumekuwa walalamikaji tu bila kufuata taratibu kukabili tatizo lililopo kisayansi na kisheria badala ya kulalama tu ni vita ya kiuchumi.

Kama sisi hatulindi raia wetu dhidi ya takataka kutoka nchi zingine tusitegemee kila nchi itakuwa hivyo. Lazima tubadilike kwa kuanza kukabiliana na haya mabo kisayansi na si kisiasa.
 
At least wewe umeongea point. Kuna wapuuzi wao washa'conclude kweli mahindi yana sumu wakisahau ugali wanaokula hawajalima wao hayo mahindi.
 
Wangeanza na kuondoa sembe yote iliyo madukani na kuwaambia watu wamwage na wasile sembe iliyotoka Tanzania au Uganda. Lakini mpaka muda huu, bado kuna sembe madukani Kenya na majumbani kwa watu iliyotokana na mahindi hayo hayo yanayosemwa yana sumu.
Upimaji wa ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchi mbalimbali ikiwemo Kenya na Tanzania upo kitambo na ni endelevu.
Endapo jana kilipimwa kikakutwa kinakithi viwango na kuruhusiwa haimaanishi siku nyingine bidhaa itakayokutwa haifai kwa matumizi ya binadamu iruhusiwe.
 
Acha upuuzi, unga huohuo tunakula watanzania. Nenda Ocean Road kaulize kansa ipi inaongoza na kama ina uhusiano wowote na hizo sumu za unga.
Ningekujibu lakini kwa avatar yako hiyo nitaonekana na mimi ni hao hao.
 
Kuna kada mmoja mtiifu wa chama fulani hapo juu amecomment eti "Mungu bariki jamhuri ya watu wa Kenya"
 
Back
Top Bottom