#COVID19 Zuio la mikusanyiko inaonekana ni kwa vyama vya upinzani tu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Miongozo na kauli zinazotolewa na serikali na viongozi wake kuhusu kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima inaonekana limelenga kuwazuia wapinzani kukusanyika lakini wao wenyewe wanaendelea na mikusanyiko ya watu huku wakionekana wakihutubia mikusanyiko mikubwa na wengi katika mikusanyiko hiyo hawajavaa barakoa.

Makamu wa rais ameonekana akihutubia huko Kigoma na Mtwara. Waziri mkuu ameonekana huko kwao Ruangwa akihutubia mikusanyiko ya hadhara na wengi wamesongamana bila barakoa. Waziri wa fedha aliyesema wanaopinga tozo wahamie Burundi naye ameonekana huko Songwe Tunduma akiandamana na kuhutubia maelfu ya watu katika mikutano ya hadhara. Waziri wa madini ameonekana akihutubia wachimbaji.

Hiyo ni mifano michache tu ya mikutano ya hadhara wanayofanya viongozi wa serikali katikakati ya zuio la mikutano ya hadhara waliyoizuia. Cha ajabu wapinzani hata wakikaa ndani na kanisani wanatimuliwa na kuswekwa ndani. Huu ni unafiki na ubaguzi mkubwa katika nchi.
 
Wapinzani ndio wanaotambua uwepo wa corona, ndio wanaopigia chapuo chanjo, Ndio wanaotaka chanjo iwe lazima

Huwezi kuamini kuna korona halafu ukakusanyika unless unatuigizia.

Kwahiyo wawe wa mfano waache mikusanyiko kwa hiari au kwa lazima kulilia kukusanyika ni kutuambia mlituigizia kusema kuna korona
 
Miongozo na kauli zinazotolewa na serikali na viongozi wake kuhusu kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima inaonekana limelenga kuwazuia wapinzani kukusanyika lakini wao wenyewe wanaendelea na mikusanyiko ya watu huku wakionekana wakihutubia mikusanyiko mikubwa na wengi katika mikusanyiko hiyo hawajavaa barakoa...
Good observation!
 
Mkuu yani huwa nashangaaga sana unakuta mtu mzima kabisa unaenda kulikimbilia gari la kiongozi barabarani nakuacha kazi zake yn km watu wamelogwa vile
Kuna mijitu mijinga sana nchi hii, na ndio mtaji wao!!hivi wasomi wa sayansi ya jamii wanaotafuta phD zao kweli, wameshindwa kuja kufanyia utafiti kwa viumbe hawa?

Wanaweza kuja na matokeo makubwa sana tena ndani ya mwezi tu, mtu akamaliza na kuandika andiko lake safi na kutunukiwa phD yake safi!!kuliko kung'ang'ania mambo magumu huko, ya kumaliza miaka 8 wakati kuna viumbe kibao hapa vya kuchukulia points?

Unaweza ingia kwenye Guines book of records kwa kutunukiwa Phd iliyotumia muda mfupi zaidi duniani, kupitia kwa nyumbu hawa!!!
 
Mkuu yani huwa nashangaaga sana unakuta mtu mzima kabisa unaenda kulikimbilia gari la kiongozi barabarani nakuacha kazi zake yn km watu wamelogwa vile
Hiv unafikir ccm siyo wachawi?HAKUNA watu wachawi DUNIA HII KAMA CCM...NA UCHAWI WAO MKUBWA NI UMASIKINI NA UJINGA KWA WATANZANIA
 
CCM ni sawa kabisa na mvinyo wa zamani katika kiriba kipya. Kinajaribu kuji "rebrand" ktk mfumo wake lakini ukweli unabakia ni kwamba sera zake hazina mvuto tena kwa wanachi kwa kuwa ni chakavu na zimepitwa na wakati.

Kwa hiyo basi viongozi wake kwa kuutambua ukweli huu hawana msaada zaidi ya kutegemea msaada wa vyombo vya dola ili kukandamiza upinzani. Kuhusu suala la "fair competition within the polical space" hili kamwe usilitegemee kutoka kwao, kwa kuwa uoga umewakumba.

Awamu ya mwisho ya CCM kuendesha siasa zenye sura angalau za kiushindani bila ya kutumia rafu za dhahiri za matumizi ya nguvubza ilikuwa ile ya hayati Mzee Mkapa. Lakini tumeshuhudia ikiwa "at its worst zenith stage" wakati wa JPM, na sasa wakati huu wa SSH ambapo anaanza rasmi kulewa madaraka.
 
IMG_0130.JPG
 
Hii Nchi kwa double standard ndiyo yenyewe! Siku zote Serikali ya ccm inatuchukulia Watanzania kama Ng'ombe vile.

Ila naamini ipo siku tutageuka na kuwa binadamu kama wao! Na siku hiyo ikifika, basi tutaheshimiana tu.
 
Miongozo na kauli zinazotolewa na serikali na viongozi wake kuhusu kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima inaonekana limelenga kuwazuia wapinzani kukusanyika lakini wao wenyewe wanaendelea na mikusanyiko ya watu huku wakionekana wakihutubia mikusanyiko mikubwa na wengi katika mikusanyiko hiyo hawajavaa barakoa.

Makamu wa rais ameonekana akihutubia huko Kigoma na Mtwara. Waziri mkuu ameonekana huko kwao Ruangwa akihutubia mikusanyiko ya hadhara na wengi wamesongamana bila barakoa. Waziri wa fedha aliyesema wanaopinga tozo wahamie Burundi naye ameonekana huko Songwe Tunduma akiandamana na kuhutubia maelfu ya watu katika mikutano ya hadhara. Waziri wa madini ameonekana akihutubia wachimbaji.

Hiyo ni mifano michache tu ya mikutano ya hadhara wanayofanya viongozi wa serikali katikakati ya zuio la mikutano ya hadhara waliyoizuia. Cha ajabu wapinzani hata wakikaa ndani na kanisani wanatimuliwa na kuswekwa ndani. Huu ni unafiki na ubaguzi mkubwa katika nchi.
Kigogo amewaambia undeni jeshi...
 
Waliapa KUILINDA KATIBA Ila WANAIVUNJA KATIBA ila Maadamu Jina la MUNGU LILITAJWA Malipo Yao yanaandaliwa
 
Back
Top Bottom