Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Miongozo na kauli zinazotolewa na serikali na viongozi wake kuhusu kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima inaonekana limelenga kuwazuia wapinzani kukusanyika lakini wao wenyewe wanaendelea na mikusanyiko ya watu huku wakionekana wakihutubia mikusanyiko mikubwa na wengi katika mikusanyiko hiyo hawajavaa barakoa.
Makamu wa rais ameonekana akihutubia huko Kigoma na Mtwara. Waziri mkuu ameonekana huko kwao Ruangwa akihutubia mikusanyiko ya hadhara na wengi wamesongamana bila barakoa. Waziri wa fedha aliyesema wanaopinga tozo wahamie Burundi naye ameonekana huko Songwe Tunduma akiandamana na kuhutubia maelfu ya watu katika mikutano ya hadhara. Waziri wa madini ameonekana akihutubia wachimbaji.
Hiyo ni mifano michache tu ya mikutano ya hadhara wanayofanya viongozi wa serikali katikakati ya zuio la mikutano ya hadhara waliyoizuia. Cha ajabu wapinzani hata wakikaa ndani na kanisani wanatimuliwa na kuswekwa ndani. Huu ni unafiki na ubaguzi mkubwa katika nchi.