The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Nabii mfalme Zumaridi anatakiwa kukumbushwa kuandika biblia ama ufunuo wake kama wlaivyofanya manabii wa zamani.
Dini hizi tunazoziona sasa zilianza kama ilivyo kwa Zumaridi lakini miaka kadhaa mbele sasa ni jamii kubwa ya waumini wakiamini kilichoandikwa na manabii kama Zumaridi wa huko nyuma
Miaka 2000+ iliyopita wakati Yesu Kristo anasema ametumwa na Mungu na kuanzisha ukristo, kwa miaka ile hakuna aliemuamini, alizomewa kama Zumaridi wa sasa, ila sasa Ukristo unabwafuasi zaidi ya Bilioni 2.
Miaka 1400+ iliyopita wakati Mohamed anaanzisha uislamu, kwa maelezo kwamba ameonyeshwa ana kuoteshwa na Mungu hakuna mtu aliemuamini ila leo uislamu una wafuasi zaidi ya Bilioni 1.
Miaka 150+iliyopita wakati Elen G white anaanzisha usabato kwa maelezo kwamba alionyeshwa na Mungu, hakuna aliemuamini miaka ile, ila leo Wasabato wamejaa Duniani Kote.
Miaka 160+ wakati Joseph Smith anaanzisha dhehebu lake la Mormon kwa maelezo kwamba Yesu baada ya kufufuka alienda Marekani kabla ya kwenda Mbinguni, hakuna aliemuamini ila leo Mormon wamejaa Duniani kote.
Miaka 140+ iliyopita wakati Charles Russel anaanzisha mashahidi wa yehova hakuna aliemuamini ila leo mashahidi wa yehova wamejaa Duniani kote.
Hao niliowataja wamefanikiwa kwa sababu waliacha maandishi ya ufunuo waliouona huko Mbinguni walipoonyeshwa na Mungu ama Yesu.
Zumaridi anapaswa kuandika kitabu ama biblia yake mwenyewe ya kile alichokiona kwa macho yake Mbinguni ili hata akifa miaka ijayo waumini na wafuasi wake watakua na kumbukumbu ya alichokuonyeshwa Nabii Zumaridi.
Ni jambo jema sasa kwa ulimwengu wa sasa oua na nabii anaeonyeshwa na kuoteshwa na kuja kutupatia mrejesho wakati akiwa hai hivyo tuna nafasi ya kuhoji na kuuliza alichokiona. Hao manabii wa zamani hatuna nafasi ya kuwahoji unabii wao waliutoa wapi, kuna vitu vingi vya kuwahoji ila hawapo hivyo nafasi haipo tena.
Zumaridi anapaswa kuenziwa na kuheshimiwa, miaka 50 ijayo tunaweza kua na dhehebu kubwa Duniani lililoanzia Tanzania kama madhehebu ama dini nyingine.