Ni fedheha sekta ya mawasiliano kwa umma hususan vituo vya radio, stesheni za televisheni, online media kukosa weledi wa kutambua kinachoendele katika mazingira yao kwa mfano hali halisi nzima ya kisiasa nchini Tanzania :
- Mtangazaji Zungu East AfricanRADIO - " ugomvi baina ya dola *(Polisi), No Reforms No Election na Wafuasi wa CHADEMA" wakati ukweli siyo ugomvi bali CHADEMA wanadai haki
- Mwandishi jukwaa la wahariri Paschal Mayala " Tundu lissu akiwa anaumwa Rais Samia alimtembelea Hospitali Nairobi" wakati ukweli ni kuwa Tundu Lissu hakuwa anaumwa bali alikuwa hospitali akitibiwa majeraha na siyo mgonjwa.
Hii tabia ya waandishi habari kushindwa kuona hali halisi kuwa fulani ni mgonjwa au kikundi kina dai haki ya kikatiba na siyo ugomvi.
Je misemo hii ya kutumia maneno yasiyo sahihi ni matatizo ya kushindwa kufafanua jambo lilivyo katika uhalisia wake au ni nia ovu kufunika matendo mabaya yanayofanyika kwa kutumia vyombo vya dola kunyima haki ya kikatiba inageuzwa ni ugomvi na mtu kujeruhiwa kwa kushambuliwa inageuzwa ni ugomvi.
Ni wakati waziri wa habari na michezo *(
wizara ya ukweli). *kuwafunda waandishi, wahariri na watangazaji kuacha kupotosha ukweli, na wachukuliwe hatua za kinidhamu za Maudhui ya Habari kwa kusema uongo katika vyombo vya habari kwa kujifanya wanachambua vitu serious labda watuambie kwa uwazi walikuwa wanafanya propaganda kwa ajili ya manufaa ya chama tawala na dola.
View: https://m.youtube.com/watch?v=pSumg8yOqMk
Pascal Mayala mwandishi guli msomi aliye mwanasheria wa Mahakama Kuu - " Samia alikutembelea Tundu Lissu ukiwa
unaumwa hospitalini Nairobi Kenya..."
TOKA MAKTABA :
Profesa Palamagamba Kabudi kuongoza Wizara ya Ukweli - Wizara ya Habari Propaganda
Serikali ya CCM inahagaika sana kujisafisha baada ya uchafuzi uchaguzi TAMISEMI 2024. Hii inakumbusha kazi ya mtunzi wa riwaya George Orwell na kitabu chake maarufu duniani kiendacho kwa jina
1984 ambapo kuna
wizara ya ukweli.
Mfano Ni nini kinashangaza kuhusu jina la
Wizara ya Ukweli? (ya CCM) itakayowaleta waziri Kabudi, katibu mkuu SG balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, Mzee S.Wassira, Prof. Kitila Mkumbo, CPA Amos Makalla n.k kwenu wananchi wapenzi mubashara kila mara kupitia TBC ikijiunga na kituo huru cha Channel Ten siku ya jumapili usiku muda kuanzia saa 3 usiku kuzungumzia
HAKI
Wizara kubwa na muhimu kupita zote ni Wizara ya Ukweli. Hapa ndipo
Winston (kinara waziri Prof. Kabudi ) anafanya kazi.
Kinachoshangaza ni kwamba, Wizara ya Ukweli imejikita katika kuunda uwongo. Wafanyakazi katika idara ya Winston na kule mtaa wa Lumumba ofisi ndogo ya CCM kupitia UVCCM hutumia siku yao kubadilisha rekodi za kihistoria ili ziakisi chochote kinachotokea wakati huo, ikiwemo ya mwendazake aliyoiacha katika miradi ya vitu n.k .
Je, kazi ya Winston kada wa chama katika nukuu ya Wizara ya Ukweli ni ipi?
Winston anaenda kufanya kazi katika idara ya kumbukumbu ya Wizara ya Ukweli. Anakaa kwenye meza yake, akiangalia maandishi yake, mashine ambayo huandika kile anachozungumza ndani yake.
Kazi yake profesa itakijikita zaidi kusasisha taarifa zozote za maandishi ambazo zimethibitishwa kuwa si sahihi au zenye madhara kwa Chama - George Orwell 1984
Je, Wizara ya Ukweli inatumia msemo gani? Wizara ya Ukweli ina kauli mbiu tatu: "Vita ni Amani," "Uhuru ni Utumwa," na "Ujinga ni Nguvu." Mistari hii mitatu imeandikwa nje ya jengo ya Ofisi Ndogo ya Chama mtaa wa Lumumba . - George Orwell
George Orwell :
Je, ni nukuu gani kuhusu ukweli na uongo George Orwell 1984?
"Na ikiwa wengine wote walikubali uwongo ambao Chama kiliweka - ikiwa rekodi zote zilisema hadithi moja - basi uwongo huo ulipitishwa katika historia na kuwa ndiyo ukweli wote.
'Ni nani anayedhibiti yaliyopita' aliendesha kauli mbiu ya Chama, 'anadhibiti siku zijazo: ni nani anayedhibiti sasa anadhibiti yaliyopita. ni mwanazuoni mkubwa ...'” - George Orwell
'The Ministry of Truth: A Biography of George Orwell's "1984"