Zungu: Miamala ya M-Pesa kwa mwaka ni trilioni 50, wananchi tulipe kodi tuache kulia

Wabunge wetu muache kuwadanganya wananchi. Excise tax is primarily a consumer tax na hivyo haya makampuni ni wakusanyaji tu...anayelipa kodi hiyo ni "mlaji" (huyo huyo anayemtetea kwenye ishu ya mitumba!). Haya makampuni yataongeza tu tariff zao ili kureflect ongezeko la kodi.

Wakipitisha kodi zote hizi wakidhani wakidhani zitabebwa na haya makampuni wanajidanganya sana na kutudanganya sisi wananchi.

Wawe wawazi tu, kuwa kodi hizi atabeba mwananchi lakini ni kwa faida ya nchi yetu (kama zitatumika vizuri) badala ya kupotosha.
 
Wabunge hawana fair play kabisa, ila nimegundua wabunge wetu ni mahiri kwa kujisemea wao kuliko wananchi waliowachagua, wako kimya kuhusu fao la kujitoa PPF.

Ndiyo ujue UHESHIMIWA na NDUGU maana yake nini.Kosa la JINAI kukubali wao waitwe waheshimiwa sana na sisi tuitwe bandugu
 

Si ajabu kutunga mtihani,kusahihisha,kujifahulisha WENYEWE SO NOTHING NEW FROM THESE PEOPLE OF CCM.

Binafsi sioni cha ajabu hapa, maana ukweli wakati mwingine huwa sina mbavu toka kwa utawala wa swisswism....huwa wanapinga hoja weee mwishoweee utasikia Spika/N/Spika akihoji wangapi wanao unga HOJA waseme Ndiyo na utasikia Wabunge wa swisswism NDIYOOOOOOOOOO......na vigelegele pamoja na ngonjera nyingi.

Wanasahu kuwa wanacho itikia kina madhara hata kwao binfsi na familia zao.
 
Acha uchama mkuu, muna wabunge makini kutoka CCM pia
 
Najaribu kufanya hesabu zangu za darasa la tatu nilipoishia.

- Kama Trilioni 50 ndio miamala ya kipesa inayofanyika kwa mwaka (average)
- Kwa kuwa mtu akitoa milioni 1 anakatwa na mtandao wa simu elfu 10 (ambayo ni asilimia 1 ya hela iliyotolewa).

- Hii ina maana katika Trilioni 50 zinapotolewa, makampuni ya simu yanakata billion 500 katika miamala hiyo kwa mwaka.

- Na Kwa kuwa kwenye kutoa hela sasa hivi hamna kodi, ina maana makampuni ya simu yanapata faida ya billion 500 ambayo hawaitolei kodi.

- Hivyo basi, kama serikali watakata 10% kwenye hela ambayo makampuni ya simu wanatukata billion 500, serikali itapata kodi yake ya 10% ya shilingi Bilioni 50.

Aaaah hizi hesabu za trilioni na bilioni sisi wa darasa la tatu zinatusumbua sana....
 
Zungu ana upeo mdogo sana kwenye kufikiria. Nini kinafuata! Hawezi kuona kuwa hizo gharama zote zinarudishwa kwa mwananchi wa kawaida? Hajiongezi kuwa kampuni za simu haziwezi kubeba mzigo ule ila ni wananchi wake? Ma ccm hayajielewi!!

 
Hata ktk vituo vya mabasi mawakala watoe risiti za kielectronic maana wizi ni mkubwa.
 
Mbona wao wabunge wanalalamika kukwatwa kodi? au wao sio raia wa nchi hii?
 
Reactions: BAK
Yaani anasema hivyo halafu baadae analalamika wao wabunge kukatwa asilimia 5 ya viinua mgongo vyao..!
 
Kweli lakini serial wadhibiti kampuni za simu wasiongeze gharama za kutuma na kupokea pesa(Makato) kwa watumiaji huduma zao
 

Tatizo kubwa ni kwamba wafanyabiashara hawakubali kupunguziwa faida yao au kupata hasara.

Watakachofanya ni kuongeza gharama za makato ili ile kodi inayochukuliwa na serikali isipunguze faida yao waliozoea kuipata.
 
Zungu ana upeo mdogo sana kwenye kufikiria. Nini kinafuata! Hawezi kuona kuwa hizo gharama zote zinarudishwa kwa mwananchi wa kawaida? Hajiongezi kuwa kampuni za simu haziwezi kubeba mzigo ule ila ni wananchi wake? Ma ccm hayajielewi!!
Kaandikiwa cha kuongea.
 
As long as kuna amani na debe la unga hamna haja ya kulalamika. Bora tu tusinyimwe hivyo viwil
 
Wanaokataa kukatwa kodi hawajui chanzo cha hela za serikali ni kodi. Huwezi dai barabara kama hulipi kodi. Unataka nani alipe?

Wazungu wanakatwa mpaka basi, sisi hatutaki kuktwa. Kinachotakiwa ni kusimamia hiyo hela baada ya kupatikana.
 
Sawa sisi tunakubali kulipa japo kishingo upande kutokana na kuminywa kwa demokrasia, basi na nyie wabunge mkubali kukatwa ile kodi kwenye mafao yenu.
Sio wabunge tu ni kwa viongozi wote wa kisiasa.na wale wote wanaopata 80%ya mshahara baada ya kustaafu hiyo 80% wasilipwe iondolewe.
 
naona watu wanamchana huyu mkulu kila kona, Tamasha la mwalimu Nyerere watu wameponda sana haya anayoyafanya

Nimeimiss hiyo nimesikia dakika tano za Jenerali Ulimwengu imebidi niishiwe kabisa yaani.Ni bora aruke vihunzi akubaliane na wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…