Zungu: Miamala ya M-Pesa kwa mwaka ni trilioni 50, wananchi tulipe kodi tuache kulia

Zungu: Miamala ya M-Pesa kwa mwaka ni trilioni 50, wananchi tulipe kodi tuache kulia

Nimeimiss hiyo nimesikia dakika tano za Jenerali Ulimwengu imebidi niishiwe kabisa yaani.Ni bora aruke vihunzi akubaliane na wengine
ipo youtube mkuu,kuna uzi wake pi umenzishwa hapa JF
 


Mbunge wa Ilala Azzan Zungu ameunga mkono kodi ya makato kwenye mihamala ya simu na kusema serikali inapoteza mapato makubwa sana, amedai makampuni yana lobby kuwa wananchi wataumia kumbe watakoumia ni wao, amewataka wananchi kuacha kulalamikia kodi kwani serikali inategemea kodi kufanya shughuli zake.

Pia amezungumzia fedha zinazopotea kwenye madini kwa makampuni ya madini kudanganya thamani ya mzigo, na wasimamimizi kukosa uelewa, amesema serikali imepoteza trilioni 18 kutoka 2002 mpaka 2011 kutokana na kudanganya bei na ameshauri hiki ni chanzo kingine kikubwa ambacho serikali inaweza ikatumia kama ikisimamiwa vizuri.


Wananchi watalipa kodi mara ngapi? Mbona bei za vyakula hazishuki angalau wananchi wakanunua chakula kwa bei nafuu kila siku vinapanda bei, tabu ni ile ile mlo1 kwa siku tabu. Izo hela za kodi zinaenda kufanyia nini serikali? Hela zilizookolewa kama mnavyodai serikali mbona bado hazimnufaishi Mtz mmoja mmoja zinaishia kwenye mfuko gani??
 
Hiyo kodi anayoongelea ilikuwepo toka zamani hamna kipya hapo, tatizo ni hili la 280 kwa kila 1000 ambalo tunahisi Zitto alijichanganya. Kama mtandao utaendelea kula 7000 kwa kila milioni serikali ikakata humohumo hakuna ubaya. Ila huwezi kata laki tatu kwenye milioni ni upuuzi hata kim jong eun hawezi fanya hivo na ugumu wake wote. Tilioni 50 transactions haimaanishi serikali ingepatamo 10%, hizo ni transaction tu sio income ya kukaba tax.

Huyu anataja matatizo bila kutoa solution, hiyo serikali wanayosema iangalie ni ipi hasa? Ndio maana akina Zitto wakiongea bunge linatetemeka, wakitaja matatizo wanataja na solution ambayo imekaa na kufikiriwa vizuri. Huyu hizo hadithi utasema kaambiwa jana kwenye dinner leo anakuja kumwaga.

Acha dharau. Labda wewe solution ulizotoa ni zipi
 
Tukateni na ninyi mkatwe, unashangaza wewe ni Zungu huyuhuyu? Kweli hela zinabadilisha mtu tabia. kwa nini uiwaambie wabunge wanaolia kukatwa kodi kwenye mafao yao watulie hela ni kwa maendeleo ya nchi hii?! Acha kuchangia upande mmoja Zungu waambie kina Lugola nao pesa inahitajika waombe radhi kuwa walifanya kosa kulalamika kutaka kuinjima serikali mapato.
 
Tukateni na ninyi mkatwe, unashangaza wewe ni Zungu huyuhuyu? Kweli hela zinabadilisha mtu tabia. kwa nini uiwaambie wabunge wanaolia kukatwa kodi kwenye mafao yao watulie hela ni kwa maendeleo ya nchi hii?! Acha kuchangia upande mmoja Zungu waambie kina Lugola nao pesa inahitajika waombe radhi kuwa walifanya kosa kulalamika kutaka kuinjima serikali mapato.
Mkuki kwa ngururuwe mtamu
 
Poor advice. Kuna pesa nyingi sana zaidi ya hizo za wabunge kiinua mgongo. Kuna madini kodi hazikusanywi kama inavyotakiwa, vitalu vya uwindaji wanyama wanawindwa kwa bei ya kutupwa, ufisadi wa kutisha kwny uuziji wa vitalu, makusanyo hafifu mazao ya baharini etc
Mkuu na wabunge nao ni sehemu ya chanzo kimojawapo, mbona wao wanalilia
 
Hatukatai,hizo tirion 50 ni zetu au za makampuni ya simu,wangeonana na makampuni waone ni namna gan watagawana hzo tiron 50,na wao kama Wabunge wawe tayari kukatwa kodi kwenye mafao yao
 
hata zikiwa trilioni 70 ni za kwetu..
tutaendelea kunenepesha matumbo ya CCM hadi lini ?
tangu uhuru wanakula serikalini leo wamekua wanyang'anyi chini ya kivuli cha mamlaka..
wakiachia madaraka hawa lazima wawe ombaomba..
 
Back
Top Bottom