Zungu: Miamala ya M-Pesa kwa mwaka ni trilioni 50, wananchi tulipe kodi tuache kulia

Nimeimiss hiyo nimesikia dakika tano za Jenerali Ulimwengu imebidi niishiwe kabisa yaani.Ni bora aruke vihunzi akubaliane na wengine
ipo youtube mkuu,kuna uzi wake pi umenzishwa hapa JF
 

Wananchi watalipa kodi mara ngapi? Mbona bei za vyakula hazishuki angalau wananchi wakanunua chakula kwa bei nafuu kila siku vinapanda bei, tabu ni ile ile mlo1 kwa siku tabu. Izo hela za kodi zinaenda kufanyia nini serikali? Hela zilizookolewa kama mnavyodai serikali mbona bado hazimnufaishi Mtz mmoja mmoja zinaishia kwenye mfuko gani??
 

Acha dharau. Labda wewe solution ulizotoa ni zipi
 
Tukateni na ninyi mkatwe, unashangaza wewe ni Zungu huyuhuyu? Kweli hela zinabadilisha mtu tabia. kwa nini uiwaambie wabunge wanaolia kukatwa kodi kwenye mafao yao watulie hela ni kwa maendeleo ya nchi hii?! Acha kuchangia upande mmoja Zungu waambie kina Lugola nao pesa inahitajika waombe radhi kuwa walifanya kosa kulalamika kutaka kuinjima serikali mapato.
 
Mkuki kwa ngururuwe mtamu
 
Mkuu na wabunge nao ni sehemu ya chanzo kimojawapo, mbona wao wanalilia
 
Hatukatai,hizo tirion 50 ni zetu au za makampuni ya simu,wangeonana na makampuni waone ni namna gan watagawana hzo tiron 50,na wao kama Wabunge wawe tayari kukatwa kodi kwenye mafao yao
 
Zungu sa'nyingine ana akili.

Ila aliwa CCM sjui zinaendaga wapi!
 
hata zikiwa trilioni 70 ni za kwetu..
tutaendelea kunenepesha matumbo ya CCM hadi lini ?
tangu uhuru wanakula serikalini leo wamekua wanyang'anyi chini ya kivuli cha mamlaka..
wakiachia madaraka hawa lazima wawe ombaomba..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…