"achakachue" contextually linamaanisha kughushi, kuficha uhalisi, kuchanganya (kama ilivyo kwa mafuta ya taa na dizeli); hapa likimaanisha kuchanganya utz na usomali...just a few to mention.
Kinachonishangaza si aache kusema lolote... Mtu anasema "uraia wake hauna utata" Hii ni sentenso tata. Maana unaweza jiuliza hakuna utata ni mtanzania au msomali. Yeye anakwambia hivo tu...
Kama anasubiri mbayuwayu aseme si angejibu "no comment" kuliko kuchanganya umma namna hii. Hawa ndo vijana wa mbayuwayu...
Mazee nimeiona hiyo nikasema au ni wikiendi wamemshtukizia Rose Garden nini? Kuangalia tarehe si wikiendi wala nini. Nikasema huu umagharibi hata wa kuwashinda wamagharibi wenyewe unatoka wapi?
Vitu kama hivi ambavyo wengine wataviona vidogo vinaonyesha mtu kama Masha anavyojali muonekano na hata utendaji.