JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Baada ya Trump kutangaza kusitisha misaada nchini humo kisa madai ya ukiukwaji wa haki za Binadamu na Wazungu kunyanyaswa na kupokonywa ardhi wanazomiliki ambapo Ramaphosa amemtaka Trump aache kuingilia mambo ya Afrika Kusini kwakuwa hayamuhusu na kusema ardhi ya Afrika Kusini sio ya Trump. “Hii ishu ambayo Donald Trump anaiogopa sana, hii ardhi ni ya kwetu, sijui Donald Trump anahusika vipi na atafanya nini kuhusu ardhi ya Afrika Kusini kwasababu hajawahi kuwa hapa, aitunze America yake na tutaitunza Afrika Kusini yetu, Afrika Kusini ni ardhi yetu na inamilikiwa na Watu wote wanaoishi Afrika Kusini, Afrika Kusini haimilikiwi na Donald Trump” “Nikikutana na Trump nitamwambia, nitamwambia wewe Trump ni Mtu mbaya kwasababu...
Binamu wa rais wa zamani wa Syria, Bashar al-Assad aliukiwa kwa kunyongwa na baada ya kupandishwa juu na crane. "Baada yakuwasili kwa vikosi vya waasi wa Syria katika mji wa Latakia, ilitangazwa kuwa Suleiman al-Assad, ambaye alikuwa kiongozi wa Vikosi vya Ulinzi wa Kitaifa, aliuawa. Kwa mujibu wa gazeti hilo, Suleiman al-Assad alinyongwa kwa kutumia kreni katika uwanja mmoja huko Latakia. Sababu ya kuuawa kwake ilikuwa uhusiano wake wa damu na rais wa zamani, pamoja na "uhalifu dhidi ya wale waliopinga utawala huo."
Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, ameisifu Katiba ya mwaka 1977 huku akitoa rai kwa vyama vya upinzani, hususan Chadema, kuheshimu na kushiriki kikamilifu kwenye chaguzi kwa mujibu wa Katiba iliyopo. Padri Kitima alieleza kuwa, licha ya kuwepo mijadala kuhusu katiba mpya, Katiba ya sasa bado ina uwezo wa kuhakikisha uwazi na ushiriki wa kila mtu katika siasa. “Katiba hii imerekebishwa mara kadhaa na bado inatosha kutuongoza kushiriki siasa kwa ufanisi. Muhimu ni kuielewa na kuzingatia ili kuimarisha demokrasia yetu,” alisema. Aidha, alisisitiza kuwa msingi wa Katiba hiyo uliwekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. “Hii ni Katiba nzuri iliyoundwa na Nyerere, mtu wa Mungu. Msisitizo...
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimeibua mkanganyiko mkubwa kwa wanachama na wananchi baada ya kubadili msimamo wake kuhusu kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.Awali, chama kilieleza nia ya kushiriki uchaguzi lakini Freeman Mbowe alinukuliwa akisema hawatashiriki. Baadaye, chama kilikanusha kauli hiyo kikisisitiza hakijajitoa. Kwa mshangao mkubwa, Oktoba 27, Chadema kimetoa taarifa rasmi ya kutoshiriki uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27.Akitoa tamko hilo, Suzan Limo Spika wa kinachoitwa Bunge la Chadema alisema: "Leo tumewaita kwa hoja mahususi kuhusu mchakato wa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa... Chadema imejiondoa rasmi kutoka uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa." Hatua hii imeshtua wengi hasa...
Back
Top Bottom