Baadhi ya Halmashauri zimedaiwa 'kuwapiga' cha juu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa.
Kwa utafiti wangu usio rasmi wa kuwapigia watumishi wa Halmashauri tofauti tofauti, nimegundua kwamba kuna Halmashauri zingine zimewalipa wasimamizi siku 19, zingine zikalipa siku 14 na zingine zikalipa kwa siku msimamizi atakazoingia darasani kusimamia. Kwa mfano, kama shule ina mchepuo wa sanaa pekee na ratiba ni siku tano au saba basi wamelipwa kwa siku hizo.
Kwanini siku za malipo zitofautiane? Malipo hayo yamegharamiwa na NECTA au kila halmashauri inalipa kulingana na uwezo wake?