Mwanaharakati Ahmed Kombo amewaomba radhi Wakristo na Waislam kwa kauli aliyoitoa kuwa akitoka Yesu na Mtume Muhammad (SAW) anayefuata ni Rais Samia.
Kombo amesema yeye ni Muislamu na anatambua kuwa Yesu Kristo na Mtume Muhammad (SAW) ni Manabii hivyo anaomba radhi.
===
Pia soma uzi huu...
Kwenye video hii Ahmed Kombo, mwanaharakati huru, anaelezea ukubwa wa Rais Samia na kumwaga sifa kedekede mpaka kufikia kusema baada ya Mtume Mohammad na Yesu anafuata Rais Samia! Amenikumbusha bwana Kabudi aliyemuita Magufuli Mungu afu akazuga kama amekosea!
Ndio tunaelekea huku na Rais Samia...