MATUMIZI ya dawa za kulevya aina ya bangi, yametajwa bado ni tatizo nchini, huku mkoa wa Mara ukiwa ni kinara katika kulima cha zao hilo ikifuatiwa na Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, ndiye aliyebainisha hayo bungeni...