chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. Analogia Malenga

    UNICEF: Nchi tajiri zatoa chanjo zinazokaribia kumaliza muda wake

    Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO limesema kasi ya maambukizi ya virusi vya corona aina ya omicron inaanza kupungua barani Afrika, baada ya wiki kadhaa za kusambaa kwa haraka. Mhudumu wa Afya akiandaa dozi ya chanjo ya Covid-19 Mkurugenzi wa shirika hilo anayehusika na hali ya dharura kiafya...
  2. Analogia Malenga

    #COVID19 Wanyarwanda waliotoroka chanjo ya Covid-19 nchini mwao wamerejeshwa nyumbani

    Mfalme wa Kisiwa cha Ijwi huko Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anasema Wanyarwanda zaidi ya 100 waliokuwa wamekimbia nchi yao kukwepa chanjo ya Covid-19 walirejeshwa nchini Rwanda siku ya Alhamisi. Katika mahojiano na BBC, Mfalme Roger Ntambuka alisema wameweza kuwashawishi...
  3. beth

    #COVID19 Dubai, UAE: Wasiopata Chanjo kutoruhusiwa kusafiri nje kuanzia Januari 10

    Mamlaka za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zimesema zitapiga marufuku Raia ambao hawajapata Chanjo dhidi ya COVID19 kusafiri nje. Waliopata chanjo kikamilifu wanatakiwa kupata ya nyongeza (Booster) ili kukidhi vigezo vya kusafiri Hata hivyo, marufuku hiyo itakayoanza Januari 10 italegezwa...
  4. Replica

    Full Text: Hotuba ya Rais Samia Suluhu ya kufunga mwaka 2021. Kirusi kipya cha Corona cha Omicron kimeshaingia Nchini Tanzania

    Rais Samia Suluhu anahutubia Taifa kuuga mwaka 2021 na ameanza na mfumuko wa bei. Rais Samia ametaja changamoto ya mfumuko wa bei ulioshuhudiwa 2021 kuwa ni zao la ongezeko la bei za mafuta kwenye soko la dunia. Aidha Rais Samia amelitaja janga la COVID19 kuwa sababu nyingine ya ongezeko la bei...
  5. L

    #COVID19 Nigeria yateketeza chanjo ya COVID-19 iliyokwisha muda wake

    Hivi karibuni, Nigeria iliteketeza dozi milioni 1.06 za chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca iliyokwisha muda wake. Wakati virusi vipya vya Corona Omicron vinaenea haraka duniani kote, jambo hilo lililotokea katika nchi ya Afrika, ambako kuna uhaba mkubwa wa chanjo na idadi ndogo ya watu waliopata...
  6. M

    Je, chanjo ya COVID-19 inachukua muda gani hadi kuanza kufanya kazi mwilini?

    Natarajia kuchanja chanjo ya COVID-19. Hivi inachukua muda gani mpaka kuanza kufanya kazi mwilini?
  7. Cannabis

    Kampuni ya Disruptive Subdermals nchini Sweden yatengeneza chip itakayowezesha kuhifadhi taarifa za chanjo ya Corona ndani ya miwili wa binadamu

    Sweden, Kampuni ya DSurptive Subdemals nchini Sweden imetengeneza chip itakayoingizwa mwilini mwa binadamu ili kuweza kuhifadhi na kuhakiki taarifa za muhusika kuhusu kupokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. Teknolojia hiyo inatumia NFC, ambayo pia hutumika kwenye mifumo mbali mbali ya...
  8. S

    NI CHANJO IPI INA UFANISI WIMBI LA NNE(OMICRON) ? ?

    Tunaomba wataalam watusaidie kujua hili mapema kadri ya wimbi hili la nne linavyo kuja kwa kasi Au kwa yeyote mwenye uwelewa huo
  9. T

    #COVID19 CDC imeshauri watu kuachana na chanjo ya J&J kwani inasababisha kuganda kwa damu kwenye ubongo, watumie Moderna ama Pfizer

    Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya Marekani, CDC imeshauri watu kupata chanjo za Pfizer ama Moderna kuliko J&J. CDC imefikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na wataalamu wa afya kwamba hizo chanjo ni salama zaidi kuliko J&J. Sababu kubwa ya kupendekeza hivyo ni kwamba J&J inasababisha matatizo ya...
  10. T

    #COVID19 Chanjo za Sinopharm, Johnson & Johnson na Sputnik hazina uwezo wa kumkinga mtu dhidi ya kirusi kipya cha Omicron

    Tafiti zimeonyesha kua chanjo ya J&J na chanjo ya China, Sinopharm hazina uwezo wa kumkinga mtu pale atakapopatwa na kirusi kipya cha corona cha omicron. Utafiti umeonyesha kwamba chanjo hizo hazina uwezo wa kutoa kinga yoyote kwa mgonjwa wa omicron. Kwa sasa kama umechanja hizo chanjo ni...
  11. F

    Siasa za Chanjo za Uviko (Politics of Covax)

    Kwakuwa chanjo ni vijidudu vilivyofubazwa nguvu vinapandikizwa mwilini ili viishi na wewe milele, sasa je, nisipochanja Corona alafu mtu aliyechanja akaniongezea damu wakati nilipohitaji damu je, vijidudu vile (chanjo yake) haviwezi kuhamia kwangu kwenye damu yake ile aliyoniongezea na kwamba...
  12. Analogia Malenga

    #COVID19 Elon Musk apinga suala la kulazimisha chanjo

    Mmiliki wa kampuni ya Tesla, Elon Musk amesema kulazimisha watu kupata chanjo si sahihi Yeye amepata chanjo lakini haitakiwi kuwapotezea wengine kazi zao Suala la kulazimisha chanjo ameliita 'un-American' yaani sio Umarekani === Musk: "I am against forcing people to get vaccinated" The...
  13. B

    Ni kweli kuna uhaba wa mabomba ya kuchomea chanjo za kwanza za watoto wachanga mkoani Geita?

    Wadau, Tumeenda kituo cha afya Kanyala kilichopo halmashauri ya Geita Mji kwa nia ya kumpatia chanjo ya awali mtoto mchanga. Wahudumu wa afya wametuambia mtoto ataruhusiwa kupata matone tu ya kuzuia polio lakin chanjo nyingine hawezi kupata. Wahudumu hao ambao walinisubirisha kwa zaidi ya...
  14. jingalao

    #COVID19 Wizara ya Afya ikishirikiana na Wizara ya Viwanda ituletee kiwanda cha chanjo ya COVID-19

    Moja ya mapendekezo ya Tume iliyomshauri Mhe. Rais kuleta chanjo ilikuwa ni kujenga kiwanda cha chanjo kwa haraka. Napena kusisitiza kuwa pendekezo hili namba 7 lifanyiwe kazi kwa uharaka ule ule ili nchi isiingìe kwenye deni lisilo la lazima.
  15. beth

    #COVID19 Ghana: Wasafiri wote lazima wapewe chanjo dhidi ya Corona

    Serikali ya Ghana imesema kwamba wasafiri wote wanaoingia nchini humo kuanzia saa sita usiku jumapili hii, wanastahili kuwa wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya Corona. Wizara ya huduma za afya imesema kwamba raia wa Ghana wanaopanga kurudi nchini humo wanalazimishwa kupokea chanjo wanaporejea...
  16. J

    #COVID19 Ufuatiliaji wa usalama wa chanjo ya COVID-19 ni mchakato endelevu

    Ufuatiliaji wa usalama wa chanjo ni muhimu katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa. Baada ya chanjo yoyote kutambulishwa, WHO hufanya kazi na watengenezaji chanjo, maafisa wa afya, kamati za ushauri za kitaifa na washirika wengine kufuatilia maswala yoyote ya usalama kwa kila mara. Maswala...
  17. Miss Zomboko

    #COVID19 WHO yaonya kuhodhiwa kwa chanjo kutoka na aina mpya ya kirusi cha Omicron

    Shirika la afya duniani WHO, leo limeelezea wasiwasi kwamba mataifa tajiri yanayotishiwa na kuzuka kwa aina mpya ya kirusi cha Omicron huenda yakahodhi chanjo za ugonjwa wa COVID-19 na kutatiza usambazaji wa chanjo hizo kote duniani hali itakayotatiza juhudi za kukabiliana na janga hilo. Mkuu...
  18. L

    #COVID19 Kuibuka kwa aina mpya za virusi kungeweza kuepukwa kama chanjo ingetolewa kwa usawa

    Wiki hii dunia imejikuta tena ikitamalaki baada ya kusikia aina mpya ya COVID-19 imeenea karibu katika mabara yote duniani. Mamlaka zote za afya duniani zimekuwa kwenye tahadhari kuhusu virusi vilivyopewa jina la Omicron, baada ya kutangazwa kuwa vina uwezo mkubwa wa kuenea kuliko virusi...
  19. beth

    #COVID19 WHO: Chanjo zilizopo zina ufanisi dhidi ya Omicron

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Chanjo dhidi ya COVID19 ambazo tayari zipo bado zinapaswa kuwalinda watu wanaopata maambukizi ya Kirusi cha Omicron, na hakuna dalili aina hiyo mpya inakataa Chanjo kuliko aina nyingine. Dkt. Mike Ryan amesema chanjo zina ufanisi mkubwa, na zimethibitisha...
  20. Sky Eclat

    #COVID19 Vitamin B12 pamoja na chanjo vina uwezo mkubwa wa kupambana na Covid

    Wataalamu wetu wanashauri tupate chanjo ya Covid, lakini waliojiongeza na kutumia vitamin B12 pamoja na chanjo waliweza kupambana na maambukizi ya Covid na kupona haraka. Kuna wakati Vitamin B12 hazikupatikana katika mtandao pendwa wa Amazon. Watumiaji waliongezeka kwa wingi kutokana na...
Back
Top Bottom