chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. J

    #COVID19 Usinywe pombe kupindukia baada ya kupata chanjo ya COVID-19

    Watu wamekuwa wakijiuliza endapo kama kuna madhara pale ambapo mtu atakunywa pombe siku au saa chache baada ya kupata chanjo ya COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema unywaji wa pombe baada ya Chanjo ya COVID-19 hauna madhara lakini ulevi wa kupindukia unaweza kupunguza ufanisi wa...
  2. J

    #COVID19 CDC: Hakuna madhara kupata chanjo za maradhi mengine kabla au baada ya chanjo ya COVID-19

    Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) kinasema watu waliopata chanjo ya COVID-19 wanaweza kupokea chanjo za maradhi megine. Mwitikio wa chanjo mwilini hautofautiani endapo mtu atapata chanjo ya aina moja au tofauti. ====== Getting a COVID-19 Vaccine with Other Vaccines People...
  3. Analogia Malenga

    #COVID19 Ubelgiji kuipatia Tanzania dozi 115,200 za Johnson & Johnson

    Serikali leo inatarajia kupokea chanjo aina ya Johnson & Johnson dozi 115,200 kutoka Ubelgiji ili kuchangia kuongeza kasi ya kampeni ya kuchanja. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ubalozi wa Ubelgiji na kuthibitishwa na serikali ya Tanzania, chanjo hizo zitachangia kuongeza kasi ya...
  4. Analogia Malenga

    #COVID19 Dola milioni 115.7 zatolewa kwa ajili ya kutoa chanjo za Malaria Afrika

    Muungano wa chanjo ulimwenguni wa Gavi Alhamisi umesema kwamba bodi yake imeidhinisha dola milioni 155.7, kuelekea zoezi la utoaji wa chajo za kwanza za malaria kwa watoto kwenye mataifa yalioko chini ya jangwa la Sahara barani Afrika. Mwenyekiti wake Jose Manuel Barroso ameeleza kufurahishwa...
  5. Abdalah Abdulrahman

    #COVID19 Kuna haja ya Serikali kulazimisha Watumishi wa Umma kuchanja chanjo ya UVIKO-19

    Watumishi wa umma ndio wanaowahudumia wananchi,kasi ya ugonjwa wa uviko-19 inaweza kupungua kwa serikali kuwalazimisha watumishi wa umma kuchanja. Hii itasaidia 1. Watumishi kuto ambukizana 2. Watumishi kuto ambukiza wananchi 3. Wananchi kuto kuwaambukiza watumishi Nchini Kenya idadi ya...
  6. Jidu La Mabambasi

    #COVID19 Waziri Gwajima: Viongozi wa Serikali wasiochanjwa waachie ngazi

    Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima karudi na rungu. Ametoa rai kuwa viongozi ambao mpaka sasa hawajachanjwa, watatakiwa waachie ngazi kwani hawawezi kusimamia kampeni ya kusimamia uchanjwaji dhidi ya corona. Waziri wa Afya amesema kama Rais kachanja ili iwe mfano, sasa hao viongozi hawatetei...
  7. J

    #COVID19 Usiwe sehemu ya upotoshaji kuhusu COVID-19 na Chanjo

    Cha kusikitisha ni kwamba, kuna habari nyingi zisizo sahihi mtandaoni kuhusu virusi vya COVID-19 na chanjo. Habari potofu wakati wa janga la kiafya zinaweza kueneza hali ya wasiwasi, hofu na unyanyapaa. Inaweza pia kusababisha watu kuachwa bila ulinzi (kinga) hivyo kuwa kusababisha dhaifu dhidi...
  8. Analogia Malenga

    #COVID19 China yaahidi dozi Bilioni 1 za Chanjo kwa Afrika

    Rais wa China Xi Jinping ameahidi kutuma barani Afrika dozi bilioni moja za chanjo ya Covid-19 ili kusaidia kuziba "pengo la chanjo". Rais alitoa ahadi hiyo wakati wa mkutano wa kilele wa China na Afrika. Kati ya bilioni moja, dozi milioni 600 zitatoka China moja kwa moja huku milioni 400...
  9. Analogia Malenga

    #COVID19 Rwanda yaanza kutoa chanjo ya ziada kwa wazee na wenye maradhi nyemelezi

    Wizara ya afya ya Rwanda imetangaza kuwa itaanza kutoa dozi ya tatu kwa wazee na wale ambao wana maradhinyemelezi kuanzia leo Jumanne. Wizara hiyo inasema utekelezaji huo utafanywa kwa awamu na utaanza katika mji mkuu, Kigali. Waziri wa nchi wa Rwanda anayehusika na huduma za afya ya msingi...
  10. Swahili_Patriot

    Je, kwanini unadhani watu bado wanagoma kuchanja chanjo hii?

    Swala la chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa uviko unaosababishwa na kirusi hatari zaidi kwa sasa, bado halijakuwa na mwamko kama ilivyo kwa chanjo nyingine kama polio, bcg. Je, kwanini unadhani watu bado wanagoma kuchanja chanjo hii? Kama mwezi ulopita nilikutana n rafiki yangu wa muda...
  11. L

    #COVID19 Kuibuka kwa aina mpya za virusi vya COVID-19 kungeweza kuepukwa kama chanjo ingetolewa kwa usawa

    Wiki hii dunia imejikuta tena ikitamalaki baada ya kusikia aina mpya ya COVID-19 imeenea karibu katika mabara yote duniani. Mamlaka zote za afya duniani zimekuwa kwenye tahadhari kuhusu virusi vilivyopewa jina la Omicron, baada ya kutangazwa kuwa vina uwezo mkubwa wa kuenea kuliko virusi...
  12. Analogia Malenga

    #COVID19 Wataalamu: Kirusi cha Omicron kitashusha ufanisi wa chanjo kwa 40%

    Katibu wa Nchi, Afya na Jamii wa Uingereza Sajid Javid amesema aina mpya ya kirusi cha #COVID19, Omicron ni kikali kuliko virusi vilivyotangulia Wataalamu wa Afya wamesema kirusi hicho kinaweza kupingana na chanjo zilizopo na kushusha ufanisi wa chanjo kwa 40% Nchi kadhaa zimechukua hatua...
  13. J

    #COVID19 Chanjo za COVID-19 zimepitia hatua muhimu za kiusalama

    Wataalamu wa Afya kutoka Chuo Kikuu cha John Hopkins wanasema utengenezwaji wa haraka wa chanjo za COVID-19 haumaanishi kuwa hatua za usalama zilirukwa Teknolojia zinazotumiwa kutengeneza chanjo hizo zimekuwa zikitengenezwa kwa miaka mingi ili kujiandaa na milipuko ya virusi vya kuambukiza...
  14. M

    #COVID19 Kirusi cha corona kimejibu mapigo dhidi ys chanjo: Kimejibadilisha na kutokea Super Corona Variant Nu!!

    Wakati mataifa ya ulaya yakitangaza kuwa chanjo mbili za corona hazitoshi na inabidi kuchanja booster kila baada ya miezi 6, kirusi cha corona kimekuja kivingine kikitokea Afrika ya kusini na kimeshasambaa mataifa kadhaa yakiwemo ya ulaya!! Mataifa mengi ya ulaya yameshapiga marufuku wasafiri...
  15. Stephano Mgendanyi

    #COVID19 Semina na wanahabari na watu mashuhuri katika mitandao kuhusu afua za kinga ya UVIKO-19 pamoja na chanjo

    SEMINA NA WANAHABARI NA WATU MASHUHURI KATIKA MITANDAO KUHUSU AFUA ZA KINGA YA UVIKO-19 PAMOJA NA CHANJO Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Amref Health Africa kupitia Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma inawakaribisha wote KESHO JUMAMOSI...
  16. Sema Kimeumana

    #COVID19 Chanjo ya UVIKO-19: Wasiotaka kuchanjwa wafunguliwe kesi ya kutaka kujiua

    Wadau, Dunia sasa linaingia katika wimbi la nne (fourth wave) ya maambukizi ya korona, kama tunavyosikia na kuona kupitia vyombo vya habari vya kimataifa, Ujerumani maambukizi yamefikia takriban 52,000+ ndani ya masaa 24 ambacho ni kiwango kikubwa ukilinganisha na waves zilizopita huko nyuma...
  17. J

    #COVID19 Chanjo ya COVID-19 ni salama kwa wagonjwa wa Saratani

    Je, hupaswi kupata chanjo ya COVID-19 ikiwa kwa sasa unapokea matibabu ya saratani? Jibu: Baada ya kukagua kwa uangalifu chanjo hizi, wataalam wa matibabu wa MD Anderson katika Chuo Kikuu cha Texas wameamua kuwa chanjo za COVID-19 ni salama na zinapendekezwa kwa wagonjwa wa saratani. Wataalam...
  18. J

    #COVID19 Prof. Makubi: Wanasayansi Wazalendo wanakaribia kutengeneza Chanjo ya Corona ya Kitanzania

    Katibu mkuu wa wizara ya afya Prof. Makubi amesema kama taifa tunakaribia kupata chanjo yetu ya Corona. Prof Makubi amesema wanasayansi wazalendo hawajalala katika utafiti na wako mbioni kutupatia chanjo ya Corona ambayo itakuwa ni ya kwetu wenyewe. Source: ITV habari ============= Katibu...
  19. J

    #COVID19 Chanjo ya COVID-19 haiathiri nguvu za kiume

    Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa nadharia zote zinazozihusisha Chanjo za #Coronavirus na kupunguza nguvu za kiume na mfumo wa uzazi kwa mwanaume sio za kweli. Aidha kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa juu ya suala hili Wataalamu wanabainisha kuwa Chanjo za corona zimetengenezwa ili...
  20. J

    #COVID19 Mchakato wa kupata Chanjo ya COVID-19 hauchukui muda mrefu

    Watu wengi wanauliza shughuli nyingi sana kupata chanjo; je, ni lazima mchakato kuchukua muda mrefu? Wataalamu wa Afya kutoka Chuo Kikuu cha Augusta huko Georgia Nchini Marekani wanasema ingawa chanjo za Pfizer-BioNTech na Moderna huchomwa kwa awamu mbili, mchakato huwa ni wa haraka na...
Back
Top Bottom