Dar es Salaam, 01 Januari, 2025:
Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inautaarifu umma kuwa, katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/25 (Oktoba – Desemba 2024) imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 8.741, sawa na ufanisi...