Katiba ni sheria au kanuni zinazoainisha jinsi ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shughuli zao.
Kwa upande wa nchi, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba za nchi pia huainisha haki za msingi za wananchi...