kariakoo

Kariakoo is a ward in the Ilala District of Dar es Salaam, Tanzania. It has a population of 9,405 (2002). The name derives from a corruption of the British "Carrier Corps", that used to be based in this area. Today, Kariakoo is mainly known for its extensive market, that spans several city blocks.

View More On Wikipedia.org
  1. kavulata

    Wafanyabiashara Kariakoo ni wakwepa kodi, wasichekewe.

    Wengi wao hawataki katakata kutoa risiti halali kwa malipo halali. Unanunua bidhaa kwa bei kubwa wanakupa risiti yenye malipo pungufu. Ukikataa wanakwambia rudisha mali. Fukuza wote wenye tabia hii hata kama awe nani.
  2. GENTAMYCINE

    RC wa Dar Chalamila vitisho vyako vya Siku Mbili Tatu kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo vimesaidia nini kama bado Wanagoma na hakuna Suluhisho?

    Wafanyabiashara wa Kariakoo, Dar es Salaam waliogoma kufungua maduka tangu juzi, Juni 24,2024 wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutoka hadharani na kutoa tamko. Wametoa maombi hayo leo Jumatano Juni 26, 2024 baada ya kufanya kikao na mwenyekiti wao na kuonekana kutoridhishwa na tamko...
  3. BLACK MOVEMENT

    Kwanini wafanyabiashara wa Kariakoo wasipeleke maumivu kwa mtumiaji wa mwisho(mlaji)?

    Nipo napitia pitia vitabu vya biashara naona kama wafanya biashara wa Kariakoo wako against na sheria za Biashara hii ni maajabu kidogo. Kwa sababu kikawaida kama kodi iko juu anaye takiwa kulia ni mnunuaji wa mwisho yeye ndie anapaswa kulia na hata kuingia Barabarani. Sasa hii ya Kariakoo ni...
  4. toriyama

    Raia wa Kichina (mfanyabiashara ) achezea kichapo leo Kariakoo kutoka kwa kina mama wanyonge wenye hasira kali

    Raia wa kichina (mfanyabiashara ) achezea kichapo Leo KARIAKOO na kina mama wanyonge wenye Hasira kali https://x.com/OKisioki/status/1805534690570273276?t=yZtJYTPn70h-bZuPEx2PAQ&s=19 #mgomo KARIAKOO 24/6/2024 Kosa la mchina: Kafungua Duka wakati wenzake wamefunga
  5. hp4510

    Rais Samia achana na wafanyabiashara wa Kariakoo, wasikupe presha!

    Mheshimiwa Rais najua ww ni Member wa JF Me naona nimeseme neno moja tu Achana kabisa na wafanyabiashara wa kariakoo, waache wagomeeeee mpaka Yesu akirudi Serikali ishasema inashughulikia Jambo Lao na bado wamegoma kufungua maduka sasa unahangaika nao wa kazi gani? Kuwadekeza hawa kutaibua...
  6. L

    Serikali isiwabembeleze wafanyabiashara Kariakoo waacheni watafungua wenyewe

    Sawa nakubali Kariakoo ndio kitovu cha uchumi nchini, biashara zote nchini watu wanafungashia Kariakoo, mapato ya nchi kwa kiasi kikubwa yako kariakoo, nafahamu pia athari za kiuchumi endapo biashara zitafungwa pale kariakoo, lakini kwanini serikali iendelee kulea wapuuzi wanaokwepa kulipa kodi...
  7. M

    Mtaji nitafute mimi, biashara nianzishe mimi, wewe uamke uje kunitishia , eti ni serikali, dunia ni kubwa sio lazima kukaa kariakoo

    Maneno ya rafiki yangu mkinga . Kama mnavofahamu , mchakato wa kusimama kibiashara ni mgumu sana , serikali wao wanawaza kukusanya tu Kwa sera zao mbovu. Hakuna mfanyabiashara anaweza kukataa kulipa kodi hayupo , lakini kodi iwe stahimilivu inayoweza kulinda biashara yangu na sio tozo na kodi za...
  8. BLACK MOVEMENT

    Kariakoo haina umuhimu kwa uchumi wa nchi kama tunavyo aminishana Bongo lala

    Kariakoo haihamisishi ukuaji wa viwanda vya ndani, Kariakoo ni Dumping site ambako asilimia 100 ya products zinazo uzwa pale ni Made in nje. Ni wajinga pekee ndio wanaoweza kuamini kwamba soko lenye asilimia 100 ya bidhaa za nje ya nchi lina umuhimu sana kwa uchumi wa nchi kuliko, Kilimo...
  9. Roving Journalist

    Maduka mengi yaendelea kufungwa Kariakoo, Jumanne ya Juni 25, 2024

    Licha ya kuripotiwa kuwepo kwa suluhu kwenye baadhi ya madai ya Wafanyabiashara waliyowasilisha Serikalini na kufanyika kikao cha pamoja lakini mpaka kufikia Saa tatu Asubuhi hali ya mgomo inaonekana kuendelea maeneo ya Kariakoo ambapo maduka mengi yameendelea kufungwa. Itakumbukwa kwamba jana...
  10. L

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam umenikosha sana leo sakata la wafanyabiashara Kariakoo

    Umeongea kwa mamlaka dhidi ya wafanyabiashara, na umenikuna sana kiongozi. Umeonyesha ujasiri mkubwa kwa wananchi unaowaongoza Dar es Salaam. Umenigusa sana pale uliposema kama nchi inapeleka jeshi kupigana Congo, vipi ishindwe kulinda Kariakoo. Dawa yao hao wafanyabiashara wanaotumwa na...
  11. A

    Sensa (needs assessment) ya wafanyabiashara Kariakoo inahitajika

    Ili kuepusha migomo kujirudia inahitajika elimu kubwa hapo kariakoo, taarifa zifuatazo zitasaidia kutengeneza maudhui ya kozi husika, 1. Majina kamili (kama yanavyoonekana kwenye NIDA), 2.TIN (anwani ya biashara ilipo), 3. Kiwango cha juu kabisa cha elimu, cha wafanyabiashara. 4. Mahojiano...
  12. Jaji Mfawidhi

    Kariakoo Machinga vs Wenye Maduka! Kufa kufaana!

    Wafanyabishara wanauliza Mmachinga ni nani ? Je watu kama hawa mwenye vyombo vingi kiwango hiki ,wanapanga barabarani vyombo vyote hivi bado wanasifa za kuitwa Wamachinga. Mtu ambaye ana bidhaa ukizijaza kwenye duka moja havitoshei eti ni machinga lakini bidhaa hizo hizo nje ya kariakoo...
  13. JanguKamaJangu

    Chalamila: Kama Serikali inatuma vikosi kupigana Congo, inashindwa kuja kupigana Kariakoo?

    DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amesema ikihitajika kuweka Vyombo vya Dola maeneo ya Kariakoo kwaajili ya kulinda biashara wakati mazungumzo ya Wafanyabiashara na Serikali yakiendelea atafanya hivyo Amesema “Nataka niwaambie ukweli, Serikali haishindwi jambo, kama Serikali inatuma...
  14. Mturutumbi255

    Mgomo wa Kariakoo: Siri ya Maduka Kufungwa na Hali Halisi Inayowakabili Wafanyabishara

    Leo, wafanyabiashara wa Kariakoo wamesitisha shughuli zao kwa pamoja kwa kugomea kodi na ukaguzi mkali, hatua ambayo imesababisha maduka kufungwa na kuathiri biashara kwa kiasi kikubwa. Mgomo huu unakuja baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu ongezeko la kodi na...
  15. JanguKamaJangu

    Chalamila awasili Kariakoo awaambia Wafanyabiashara “Fungueni maduka, Biashara sio Siasa”

    Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefika soko la Kariakoo kutokana na Biashara kufungwa kuanzia leo Juni 24, 2024 na kuongea na wafanyabiashara. Chalamila amesema wafanyabiashara wako wa aina kadhaa ikiwemo walioshiba, kati na wachanga na iwapo wataigana kuna watakaojuta leo...
  16. D

    Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024

    Hadi Sasa ni saa 2:24 asubuhi maduka mengi hayajafunguliwa. Licha ya Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, kuwasisitiza Wafanyabiashara wa Kariakoo kuendelea na shughuli zao kama kawaida, hadi Saa 9 Asubuhi Wafanyabiashara wengi wamefunga Biashara zao katika Mitaa ya Kariakoo, leo Juni 24, 2024...
  17. The Assassin

    Mwenyekiti wa Wafanyabishara Kariakoo: Tunataka kugoma kwa Sababu ya TRA haitaki kutuelewa

    Mwenyekiti wa Wafanyabishara Kariakoo anasema chanzo cha mgomo wao ni TRA kurudisha enforcement. Malalamiko yao makubwa ni kwamba TRA inawaonea kwa sababu inawadai VAT na waziri mkuu aliagiza TRA iwasikilize. Nachokiona ni kwamba wafanyabishara hawataki kabisa kulipa kodi nchi hii. Hii nchi...
  18. Paul Alex

    Ni Nani anayumbisha Serikali, Nani alitoa go ya kumtukana mama, Nani anayetaka Bashe aanguke, Nani anataka biashara K koo isimame?Nani?

    Wakuu salaam! Naweza kupingana na mama sehemu nyingi ila kuna mambo ya kimaslahi kitaifa siwezi kupinga. Mama ana mapungufu yake ila??? Ila?? Nani anayetaka wafanyabiashara Kariakoo wagome na kwanini? Ni Nani huyo anayetaka kunyonga koo la uchumi wa nchi na kwanini? Wasukuma bwana! Hawajawahi...
  19. kimaus

    KERO Mamlaka haziioni barabara ya mtaa wa Lindi Kariakoo?

    Nimekuwa nikipita mara kwa mara mtaa wa Lindi kariakoo ili kuegesha gari kwenye eneo la maegesho gerezani. Ile barabara kuanzia makutano ya mtaa wa Lindi na Msimbazi mpaka makutano ya Lindi na Kawawa Road (Karume) ni mbaya mno. Eneo ambalo daladala za Tandika zinapaki lina mabwa makubwa ya...
  20. The Supreme Conqueror

    Kinachodaiwa kuwa mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo ni mazingaombwe yaliyotengenezwa kumngo'a mkuu wa TRA Kidata

    Jana zilisambaa taarifa kwamba wafanyabaishara wa soko la Kariakoo wataanza mgomo usio na kikomo kuanzia Jumatatu Juni 24. Kinachodaiwa kuwa mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo ni mazingaombwe yaliyotengenezwa pia Kuna Waziri Mwandamizi anahusishwa katika mgomo huo kutokana na kile...
Back
Top Bottom