Inasikitisha kwasasa kigamboni kuguka ni kadi tu uwe mtoto uwe mkubwa ni Tsh 200 tu kwa wote sasa hakuna tena ile mtoto tsh 100 kweli hii vita Ukraine inatonyoosha kila idara aisee ila hongera kwa temesa kwa kutuminya wanakigamboni big up kwa uongozi temesa kazi iendelee
Nauli za bajaj tayari zimepanda kutoka 500 mpaka 1,000/=
Na hakuna ufafanuzi wowote.
Jana natoka zangu mishe naambiwa nauli 1000 badala ya 500.
Hii siyo haki.
Watu kadhaaa wanahofiwa kufariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakiwa kwenye shughuli za machimbo ya mawe katika eneo la machimbo ya Kikikaka, Mji Mwema Kigamboni, Dar es salaam. Kwa mujibu wa taarifa za awali shughuli za uokoaji zinaendelea.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo eneo la...
Wakuu hi tozo ikiondolewa wakazi wa Kigamboni itawapunguzia Sana Ukali wa Maisha.
Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) ameitaka Serikali kuondoa tozo za Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni na badala yake Serikali ibebe mzigo wa deni la mkopo wa NSSF.
Ndugulile ameyasema haya leo...
Mama Samia tunaomba Huruma yako Kigamboni:
Kwanza naanza kukusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano WA Tanzania..., Natumai umeitikia "Kazi iendelee.."
Pili nakupa pole kwa kazi ngumu ya kuongoza Tanzania, nchi yenye Mazonge ya kila rangi kila uchao,
Na Tatu nakupa pongezi kwa siku hii ya...
Wadau nina jambo hapa tuweke siasa kando tujadili maendeleo
Baada ya huu uzi hapa chini kutolewa
Rais Samia wasaidie wananchi hawa wa Kigamboni kuna wakubwa ‘wanawapiga’ katika ardhi yao
Inaelezwa kuwa kuna kigogo mmoja pande za kule kwenye kuvuka maji kule, Kigamboni anahaha kupiga simu...
Inadaiwa kuwa huu mchongo unawahusisha vigogo wa kwenye mamlaka za juu na ndiyo maana kuna danadana zinaendelea.
Taarifa za uhakika kutoka wa watu ambao wamekuwa sehemu ya waathirika wa mradi huo kwa ardhi yao kutaka kuuzwa kwa bei ya chini amedai kuwa wameshafanya vikao vingi lakini hakuna...
Wakuu, jana na leo! Nimeshuhudia kitu kisicho cha kawaida wakati navuka kati ya Feri na Kigamboni.
Sijui kivuko ni kibovu ama vipi.
Tumepanda kikagoma kabisa kwenda, nafikiri tulikuwa wengi kupita kiasi.
Tukapunguzwa at least kikatembea kwa shida.
Yaani kwa sasa Feri ni shida kweli kweli...
Ni matumaini yangu Makubwa kuwa hizo Helicopter huwa zinakuwa Salama na zinafanyiwa Matengenezo makubwa kwani kwa mwaka huu Watanzania hatuhitaji Kuomboleza tena.
Halafu wala msihangaike kwenda huko Avic Town Kigamboni ilipo Yanga SC Kisirisiri kwani wengine tunawajua hata mlivyokuwa Uongozini...
Kipindi nakua mji ulikuwa mwisho ubungo, pale lilipo jengo la Tanesco ndio ulikuwa mzani wa kupima malori ambao sasa uko mkoa wa Pwani, Dar inakuwa kuelekea kaskazini,npaka wa Dar na kibaha unafutika, mpaka wa Dar, Bagamoyo unafutika kwa kasi sababu ya ujenzi unaokuwa kwa kasi ya ajabu...
Habari ya asbuhi wakuu. Ninahitaji nyumba ya kupanga maeneo ya Kigamboni kuanzia Mji mwema kuja uelekeo wa Maweni, hadi kwa Mwingira.
Ninahitaji iwe na vigezo vifuatavyo:
1. Vyumba viwili vya kulala ambapo kimoja kati ya hivyo kiwe self contained.
2. Kuwe na sebule
3. Public toilet ndani
4...
Nilikuwa Dege Kigamboni siku ya leo. Nimeshangaa sana baada ya kuona majumba makubwa sana ya ghorofa, majumba kama utitiri.
Baada ya kuuliza nikaambiwa ni mradi unaitwa Dege Eco Village. Kwa haraka haraka tunaweza kusema ni kama Kariakoo au hata zaidi.
Nakosa hata ya kuandika maana bado...
Yaliyomshinda Mbunge wangu Kigamboni:
Sina pa kusemea, ukurasa wangu hapa facebook ndio kipaza Sauti changu.
Anyways, Sikuwa na matarajio mkubwa kwake kwa kuwa Sina Imani na kikundi cha watu(chama) kilichomweka kwenye nafasi hiyo, kwa mantiki hiyo pia Sishangazwi na jinsi anavyotupuuza wana...
Salaam Wakuu,
Abiria wanaotumia kivuko cha Magogoni Kigamboni mnakumbushwa kwamba mwisho wa matumizi ya tiketi za karatasi kwenye kivuko hicho ni Tarehe 28 Februari 2022 hivyo abiria wote mnaombwa kununua kadi za N-CARD. Kadi hizo zinapatikana Kivukoni pande Zote mbili.
Wakala wa Ufundi na...
Habari wana JF,
Nina kiwanja changu nakiuza 4mil kipo Kigamboni kimbiji golani eneo la kidagaa kina hati toka ardhi 600sq ni km 35 kutoka Kigamboni Ferry ..
Kwa mawasiliano zaidi piga 0657940974
Wana JF,
Kuna article mtandaoni inasema Egypt inajenga sehemu itakayoitwa "Egyptian Industrial City in Kigamboni" nchini Tanzania. Sijaelewa vizuri maana yake. Tumewauzia sehemu ya nchi au tulikuwa wavivu wa kukubaliana jina la hiyo Industrial City? Hebu tusaidiane kutafakari hayo maandishi...
Katika tambia yangu mkoa dsm kigambo nahisi ni mahali ambapo panaongoza kwa askari barabarani.yaani sijui kwanini maana mikoani tunahitaji pia maana mimi nipo musoma sijawahi kuona trafiki labda kuwe na jambo kigamboni nimekutana na camera 3 na sehemu zaidi ya 5 tumesikamishwa ebu mje mkoani pia...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.