SURA YA 1
KWA mara nne mfululizo katika wiki ile, Luteni Maige alijiwa na ndoto ile ile usingizini. Aliamka kwa mshtuko, jasho likimtoka huku akihema kwa kasi.
Safari hii, hata alipofumbua macho, alikuwa na hakika kabisa kuwa risasi mbili alizofyatua zilimpata kiongozi wa nchi kichwani na...