KATIKA kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka, idadi ya abiria katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam, imepungua tofauti na miaka mingine inavyokuwa. Kipindi cha Pasaka katika miaka mingine kuanzia Alhamisi Kuu na kuendelea kunakuwepo na abiria wengi wanaokwenda mikoani...