Wafanyabiashara katika Soko la Machinga, lililopo kata ya Mlandege, mkoani Iringa, wanakabiliana na changamoto kubwa ya kukosa miundombinu ya vyoo. Hali hii inawalazimu kutumia eneo la nyuma ya soko, ambalo ni la makaburi, kama sehemu ya kujisaidia. Hii ni hali ya hatari kwa afya, kwani eneo...