maji

  1. BigTall

    KERO Wakazi wa Mtaa wa Mshikamano -Mbezi Louis (Dar) hatuna huduma ya maji na Mamlaka zipo kimya

    Huku Mbezi Louis maeneo ya Mtaa wa Mshikamano Jijini Dar es Salaam hakuna maji ni mwezi sasa (Hadi muda naandika andiko hili Februari 10, 2024). Mara chache yanayoka usiku mwingi, Watu wanasumbuka kuamka mida hiyo na kukuta maji yanayotoka ni machafu balaa. Imagine kukaa mwezi mzima maji...
  2. Stephano Mgendanyi

    Mbunge Condester na DG RUWASA, Kivegalo Wafika Chilulumo, Ivuna na Kamsamba Kutatua Changamoto ya Ukosefu wa Maji Vijijini Jimboni Momba

    MBUNGE CONDESTER NA DG RUWASA ENG. KIVEGALO WAFIKA CHILULUMO, IVUNA NA KAMSAMBA KUTATUA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MAJI VIJIJINI, JIMBONI MOMBA Mbunge wa Jimbo la Momba, Mhe. Condester Sichalwe leo tarehe 09 Disemba, 2024 ameendelea na ziara akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Clement...
  3. Erythrocyte

    Uchaguzi wa CHADEMA Mbeya Mjini ni moto, John Mwambigija Maji ya Shingo, akabiliwa na Ushindani mkali

    Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , leo 09/02/2024 kuna Uchaguzi wa Viongozi wa Chadema Mbeya Mjini . Habari zinadokeza kwamba Ni kama vile Mbeya Mjini leo ni siku ya Mapumziko , huku wafanyakazi wa Serikali na makampuni wakitoroka makazini mapema , kwa kisingizio cha ibada ya Ijumaa ...
  4. Stephano Mgendanyi

    Momba: DG RUWASA Afika Jimbo la Momba Kutatua Kero ya Ukosefu wa Maji Kata ya Ndalambo na Msangano

    MOMBA: DG RUWASA AFIKA JIMBO LA MOMBA KUTATUA KERO YA UKOSEFU WA MAJI Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Eng. Clement Kivegalo amesema Wastani wa upatikanaji wa maji safi na salama nchini ni asilimia 79.7 lakini kwa Jimbo la Momba Wastani wa upatikanaji wa maji safi na salama ni sawa na asilimia 51...
  5. Determinantor

    Ubungo, Mabibo, Mburahati, Manzese hakuna maji siku zaidi ya tano sasa

    Maeneo tajwa hayana maji kwa zaidi ya siku tano sasa, Wahusika wako kimyaaa, jana nimewaona Watendaji WA Dawasco wako kwenye Bajaj wanazunguka Tu. Hii Hali ni hatari, kipindupindu kiko nje nje, mahotel mengi Sana hapa Manzese hayana maji. Umeme NAO unakatwa kwa zaidi ya masaa SITA Hadi 12 kwa...
  6. Mjanja M1

    Upungufu wa Gesi na maji ndio chanzo mgao wa umeme

    Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, imeweka wazi kuwa sababu ya mgao wa umeme nchini umesababishwa na upungufu wa maji na gesi. “Sababu za uzalishaji wa umeme kuwa mdogo ni pamoja na upungufu wa maji kwenye mabwawa tegemezi yakiwemo Mtera, Kidatu na Kihansi; uchakavu wa mitambo ya kuzalishia...
  7. Wizara ya Afya Tanzania

    Upatikanaji wa umeme vijijini mwarobaini katika kuwezesha uwepo wa maji safi na salama ili kuzuia magonjwa ya mlipuko

    Na.Elimu ya Afya Kwa Umma. Imeelezwa kuwa upatikanaji miundombinu ya maji safi iliyounganishwa na miundombinu ya umeme katika vijiji vya Nyanguge na Bunamhala Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu imekuwa mwarobaini katika kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu. Hii ni baada ya...
  8. Stephano Mgendanyi

    Momba: Anayepinga Madai ya Shida ya Maji Momba Akapimwe Akili?

    MOMBA: "ANAYEPINGA MADAI YA SHIDA YA MAJI MOMBA AKAPIMWE AKILI"? BAANDA ya February 2. 2024 Mbunge wa Jimbo la Momba kwenda na ushahidi wa video ikionyesha Wananchi wa Kijiji cha Lwatwe kata ya Ivuna wakifukua Maji chini ya ardhi, baadhi ya watu wameandika mitandaoni kwa kichwa kinachosema "...
  9. Mto Songwe

    Kwetu sisi watanzania maji na umeme havina umuhimu wowote ule. Sisi wananchi tumesema

    Sisi wananchi Watanzania kwa kauli moja tunasema" Tunapenda tuendelee kuishi hivi hivi miaka yote" Maisha ya sasa tunayoishi bila umeme wa uhakika wala maji ndio maishi bora kwetu. Huo umeme, maji kwetu hauna umuhimu wowote kazi zetu wala hata hazihitaji kabisa matumizi ya umeme wala maji...
  10. BARD AI

    Hitilafu ya Umeme yawakosesha Maji wakazi wa Dar na Pwani

    Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani kuwa kumekuwa na ukosefu wa huduma kutokana na hitilafu katika mfumo wa umeme wa Gridi ya Taifa. Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi Februari 3,2024 na kitengo cha...
  11. JanguKamaJangu

    Mbunge wa Momba alia na Wizara ya Afya kuhusu Huduma mbovu ya maji jimboni kwake

    Mbunge wa Momba, Condester Michael Sichalwe amedai kuna changamoto ya maji safi katika Jimbo na kuwalaumu Wizara ya Afya Kwa kutoshughulikia Hali hiyo. Amedai maji wanayotumia Wanamomba hayastahili kutumiwa na Binadamu kutokana na kutokuwa masafi.
  12. Kaka yake shetani

    Mpaka leo sijaelewa ziwa victoria na msaada wake kwenye huduma za maji kanda ya ziwa

    katika vitu ambavyo vina nishangaza kanda ya ziwa yani unakosa maji huku ukiangalia ziwa likiwa lina maji ambayo siyo ya chunvi. kuna siku mvua ilinyesha ndio maji yaka toka yani mpaka mvua kweli.huduma za maji kanda ya ziwa ni za kusua sua tunaishi na ndoo na mapipa kwa mgao. tatizo ni nini kwa...
  13. Roving Journalist

    Katavi: Mkandarasi akwamisha mradi wa maji wa Miji 28

    Wakati Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maji hapa nchini ili wananchi waweze kusogezewa huduma ya maji hasa kwa kumtua mama ndoo kichwani, imeeleza kuwa bado baadhi ya wakandarasi wanashindwa kutekeleza miradi hiyi kwa wakati ambapo mradi wa maji unaotekelezwa katika bwawa la Milala...
  14. K

    KERO Dar: Maeneo ya Segerea hadi Kinyerezi hakuna Maji

    Mkuu Naomba nilete kwako kero hii ambayo kwa hapa Dar es Salaam imeelekea kukomaa sasa. Kuanzia tabata, segerea kinyerezi huduma ya maji haipatikani. Bila shaka kuna kutoa rushwa maji yafunguliwe upande wenu. Maeneo ya Kanga Kinyerezi maji hayatoki wiki ya 3. Mheshimiwa unahujumiwa tunaomba...
  15. S

    CPA Habibu Suluo LATRA Mkoa wa Arusha wako juu yako? Daladala za Kikatiti na King'ori zinageuzia Maji ya Chai

    Mkurugenzi mkuu wa LATRA unataka tutumie lugha ipi ili uelewe kuwa abiria tunaosafiri kutoka Arusha mjini kwenda Kikatiti ja King'ori tunashushwa Maji ya Chai wakati magari yana vibao vimeandikwa Kikatiti na mengine King'ori. Mnasubiri mpaka wananchi wajichukulie sheria mkononi? Tumechoka na huu...
  16. sanalii

    Fikiria umeme hamna na maji hamna!

    Kama ingekuwa sehemu za watu wawajibikaji kuna watu wangeondolewa kwenye nafasi walizonanzo maana hawatoshi. Kweli na mvua hizi lakini maji hayatoki? Nani yuko responsible?
  17. donlucchese

    Naomba msaada jinsi ya kusoma Mita ya maji (DUWASA)

    Salam wakuu, Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, naomba msaada jinsi ya kusoma hizi Mita maana muda mwingine nahisi wananibambika bili. Matumizi ya kawaida tu ya maji na hapo ni familia ya watu wanne tu lakini jana wamenitumia bili elfu thelathini. Ningesema pengine labda kwakuwa nilipanda...
  18. A

    DOKEZO Maringo, Kawe kuna wenzetu wanaziba mitaro ya barabarani kwa viroba ili wapate maji ya kumwagilia maua

    Eneo la Kawe katika Kituo cha Daladala cha Maringo kuna hali ambayo imekuwa ikinikera kwa muda mrefu, mitaro inayopotisha maji inazibwa kwa makusudu kwa kutumia viroba na vijana wanaofanya biashara ya kuuza maua ‘original’, yaani yale maua halisi, wanafanya hivyo ili wapate maji ya kumwagilia...
  19. Webabu

    Watu wa Gaza waanza kula majani na kunywa maji machafu

    Tangu vita kuanza vyakula vimekuwa vikiingia eneo hilo kwa shida sana na ni asilimia chini ya 10 ya mahitaji ya kawaida. Pamoja na hivyo ujasiri na uvumilivu wa wapalestina umewafanya waendelee kusihi kwa kidogo wanachopata mpaka pale Israel ilipotia fitna ya kutaka hata hicho kidogo...
  20. mwanamwana

    Hadhari: Baadhi ya Barabara Morogoro zimefurika maji

    Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimezidi kuleta athari kubwa kwa wananchi, uchumi na miundombinu. Mamlaka ya hali ya hewa imetangaza uwepo wa mvua mikoa ya Morogoro Iringa, Ruvuma, Songwe, Mbeya na Njombe nk, hivyo kama raia wema ni vyema kupeana taarifa barabara korofi ambazo zimekumbwa na...
Back
Top Bottom