KIFO CHA MKULIMA
1.
Hadithi nawaletea, sikiliza kwa makini,
Zamani kulitokea, porini kundi la nyani,
Mitini walirukia, mara juu mara chini,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.
2.
Waliposikia njaa, lienda huko shambani,
Mahindi wakachukua, kurudi nayo porini,
Wakanywa na maji pia, kwenye...