Septemba 22, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, aliongoza kikao muhimu na wamiliki wa hoteli mkoani Ruvuma. Kikao hiki kilifanyika kama sehemu ya maandalizi ya kuimarisha sekta ya utalii, hasa wakati huu ambapo mkoa unasherehekea Tamasha la Tatu la Kimataifa la Utamaduni...