Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) is a public university in Dar es Salaam, Tanzania. It is accredited by the Tanzania Commission for Universities (TCU).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo Septemba 12, 2024 amezindua kituo cha upandikizaji mimba (IVF) cha Dkt. Samia Suluhu Hassan kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar Es Salaam.
Sambamba na hili , Dkt. Philip Isdor Mpango leo...
Jana siku ya jumatatu 26.08.2024 nilimsindikiza mgonjwa Muhimbili akaandikiwa kipimo cha Ultrasound tulivyoenda kulipia tumekuta bei imepanda zamani ilikuwa Tsh 25,500 lakini jana tumelipishwa 35,500,je ina maana na vipimo vingine navyo vimepanda bei au imekaaje hii.
Je hali ikiwa hivi sisi...
Magwiji wa tiba radiolojia duniani ambao hutumia vifaa kama vile CT-Scan, MRI, Xray, Angiography system, Utrasound n.k kufanya uchunguzi na kutibu magonjwa mbalimbali kupitia matundu madogo, mapema wiki hii wamekutana Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutathmini hali ya utoaji huduma hiyo...
Mwalimu na Ustaadh Mkuu Dr Musa amedakwa akitapeli wagonjwa Muhimbili. Tukimbilie wapi?.Hawa ndo wanafundisha watoto Madrasa, kweli Kwa design hii watoto wapo salama?
Prof Janabi dhibiti Hawa kama uhusiki
Nilikuwa na mgonjwa wangu ambaye alikuwa anasumbuliwa na Saratarani, alikuwa anapatiwa huduma Ocean Road, tukiwa hapo tukapata referral ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga), Dar es Salaam.
Wakati tunaelekea Muhimbili tukapita Hindu Mandal kwa kuwa kuna Daktari ambaye pia...
Siku kadhaa zilizopita tutakumbuka hapa jukwaani lililetwa dokezo na mdau kuhusiana na hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufunga CCTV-camera kwenye vyoo kiume, suala ambalo pia lilichapishwa hadi kwenye kurasa rasmi za #Jamiiforums ikiwemo Facebook, Instagram na X.
Kati ya hoja zilizobainishwa...
Habari wana JF,
Husika na kichwa hapo juu. Naomba kufahamishwa ada ya diploma ya nursing kwa mwaka ni shilingi ngapi?
Pia, gharama za hostel zao ni shilingi ngapi kwa mwaka na je, mwanafunzi anaweza pata hostel kwa miaka yote mitatu?
Naomba kwasilisha, mnaojua mnisaidie!
Hii hospitali kama serikali na uongozi hautachukua hatua za haraka watanzania wengi wataendelea kufa kwa uzembe wa madaktari wanafunzi ambao hawasimamiwi ipasavyo na wakuu wao kazi.
Nimeshuhudia mgonjwa wangu akiambiwa hana tatizo lolote la nyonga baada ya kumpeleka akiwa amepata ajali na...
1. Majuzi nilipata msiba wa Kaka yangu hapo Muhimbili basi akapelekwa Mochwari.
2. Siku ya kutoa maiti kwa ajili ya ibada na Maziko (mhudumu anataka TSH 200,000) mbali na zile gharama ambazo tulililipia na kupewa risiti halali.
3. Wale wahudumu kama hujatoa pesa ya chai utashinda kutwa nzima...
Ndugu wajumbe,ubora wa Vyuo Vikuu hupimwa Kwa Wingi wa tafiti na machapisho ya kitaalmu.
Kwa mujibu wa taarifa ya jarida la masuala ya Elimu ya Juu,Limetaha Vyuo 10 Bora Barani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ambapo Chuo Kikuu Muhimbili kimeshika nafasi ya 3 na Chuo Kikuu Ardhi kimeshika...
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Prof. Mohamed Janabi amesema kila siku takriban Wagonjwa 150 wa Figo wanasafishwa Damu hospitalini hapo na 90% wamegundulika kuwa na Kisukari na Shinikizo la Damu
Amesema kama watu wasipochukua hatua za...
Hivi haiwezekani kutafuta maeneo mapya na ikajengwa Hospitali Mpya kuliko kukarabati Hospitali moja kila baada ya muda mfupi?
Au mimi kuna kitu sielewi?
Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Aprili 9, 2024 imesema kutokana na maboresho yaliyofanyika na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili upande wa Kliniki za VIP Jengo la wagonjwa wa nje inayoitwa 'NOPD VIP', bei ya kumwona Daktari kwa Kliniki kwa sasa ni Shilingi 100,000/=...
Kutokana na baadhi ya hospitali binafsi kusitisha huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia leo Machi mosi, 2024, uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umekuja na mpango wa dharura wa kuwahudumia.
Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wawe na mwendelezo wa huduma...
Kufuatia baadhi ya Hospitali kusitisha huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia Machi 1, 2024, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umekuja na mpango wa dharura wa kutoa huduma kwa wanachama hao ili waweze kuwa na mwendelezo wa huduma hizo.
Mkurugenzi...
Hospitali ya Taifa Muhimbili, leo kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji wa kutoa mfupa kwenye ubavu na kutengeneza kiungio (joint) cha taya la chini na fuvu ili kumtengenezea mgonjwa taya jipya la kulia lililoathiriwa na uvimbe.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Uso na Taya Dkt Arnold Augustino...
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi amewapokea madaktari bingwa wabobezi wa upasuaji wa nyonga Watatu kutoka nchi ya Pakistan watakaoendesha kambi ya siku tano ya upasuaji wa nyonga kwa wagonjwa 40 kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa...
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uwekezaji uliofanyika hospitalini hapa ambao umewezesha huduma mbalimbali za kibingwa na ubingwa bobezi kufanyika ikiwemo upasuaji mkubwa wa kutenganisha...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.