Kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007(PCCB Act, 2007); Rushwa ya ngono ni pale ambapo mtu aliye katika mamlaka na katika kutekeleza mamlaka yake akitaka au akiweka upendeleo wa ngono kama kigezo cha kutoa ajira, cheo, haki, au huduma ya upendeleo...