Paka kiwepo pahala,panya hawana pirika,
Pale kakamata dola, panya wanadhoofika.
Mashimoni wanalala, kero tunapumzika.
Tangu paka kuondoka,panya nyumba watawala.
Paka walikuwa jela,kifungo walifungika,
Wakawa si wa kitala,midomo walifungika.
Kuondoka wa kuwala,jikoni ni patashika,
Tangu paka...