uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. T

    Utabiri kuelekea uchaguzi Ukimya wa Mungu haumanishi mmekubalika jambo kubwa litatokea

    Mungu huweka serikali na viongozi kwa wakati na muda anautaka yeye. Warumi 13. Najuwa kuna watu hamuwezi kupenda ila leo natamani mjiulize ktk serikali ya hayati Magufuli idadi ya viongozi ndani ya serikali yake walitutoka wakati tukiwa tunategemea uwepo wao. Nani angeamini tungempoteza Magufuli...
  2. M

    Pre GE2025 UCHAGUZI CHADEMA: BAVICHA waelewe bila Maridhiano hata huo Uchaguzi labda usingefanyika, punguzeni Dharau kwa Mbowe

    Nimekwazika sana baada ya kufuatilia Mdahalo wa Wagombea wa BAVICHA kuona wanashambulia Maridhiano kwamba hawakubaliani nayo na mambo mengine ya kijinga waliyoongea kuonyesha upeo mdogo sana wa kuona mambo kwa upana. Kwa wanaoelewa hali ya kisiasa ilipofikia hata Vikao vya ndani vya Chama...
  3. Erythrocyte

    Pre GE2025 Wadau washangazwa na Kitendo cha Mkutano Mkuu wa CCM kupuuzwa, huku wa Chadema ukiwa Gumzo

    Wengine wanasema kwamba tangu wazaliwe hawajawahi kuona hamasa kubwa ya Chama cha Upinzani kwa kiwango cha kufunika ccm kwa kiwango hiki Taarifa zingine zinadokeza kwamba hata hili la Mrithi wa Kinana limechomekwa tu ghafla ili kujaribu kutafuta Kiki na labda kufifisha uchaguzi wa Chadema...
  4. GENTAMYCINE

    Kwanini Watu wa 'Msaada Kontena Oysterbay' wanautolea macho mno huu Uchaguzi wa CHADEMA?

    au Uchaguzi huu wa CHADEMA ni sehemu ya Utendaji wao (kwa Kipaumbele) na kwamba yale mengineyo ya Kimsingi kwa sasa si Kipaumbele chao?
  5. M

    UCHAGUZI CHADEMA: Mahojiano ya Mbowe leo Clouds yamesitisha moja kwa moja Mdahalo wa Lissu na Mbowe

    Mbowe leo kadhihirisha ni Mwanasiasa Genius,smart,broad,wise,mtulivu na Mvumilivu sana.Nimeangalia Interview nzima ni as if alikuwa anaprove ni kwa kiasi Gani Level yake ya kisiasa ni ya juu sana kucompare na Lissu. Utumiaji wa Vifungu vya Katiba katika Uongeaji wake ni kama alikuwa anaonyesha...
  6. milele amina

    Pre GE2025 Athari za TAL kwa siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

    Lissu akimaliza mchakato wa uchaguzi wa ndani wa Chadema, kuna uwezekano mkubwa kwamba atahamishia mapambano yake kwenye serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Hii ni kutokana na historia yake ya kisiasa na mbinu zake za kukabiliana na changamoto zinazohusiana na utawala. Hivyo, ni muhimu kwa...
  7. Tlaatlaah

    Unadhani ni kwanini uchaguzi wa chadema wa mwaka huu ni baina ya wanaokusudia kuibomoa chadema dhidi ya wanaokusudia kuijenga na kuimarisha chadema?

    Ni wazi kuelekea uchaguzi wa chadema ngazi ya Taifa, kuna wagombea wasio wazalendo, makuwadi wa mabenyenye ya magharibi, wanaokusudia kuigawanya, kuisabaratisha na kuipoteza kabisa chadema kwenye medani ya siasa kwa makusudi, kwasababu za tamaa zao, ubinafsi, uchu wa madaraka na vyeo, unafiki na...
  8. kavulata

    Uchaguzi CHADEMA ni sawa na kuchagua kati ya heri na shari

    Wagombea uwenyekiti CHADEMA Wana sofa na tabia tofauti kiasi cha kuwafanya wanachama kuamua kuchagua kati ya heri na shari.
  9. M

    Uchaguzi CHADEMA kizazi cha Gz kushuhudia mabadiliko makubwa

    Wakuu ,kwa wale vijana wetu ambao hawakuwahi kusikia sauti tofauti ya Mwenyekiti wa chama cha Chadema, mwezi huu Mungu atatenda, ukumbuke ya kwamba hawa vijana wakati wa uhai wa maisha hawakuwahi kushuhudia Mwenyekiti tofauti na Mzee Mbowe. Kwa jinsi hali ilivyo ni dhahiri ya kuwa Mzee Mbowe...
  10. M

    Uchaguzi wa Gari zuri

    Habari za leo wanajamvi Naombeni ushauri wenu juu ya uchaguzi wa gari. Ushauri uangalie vitu kama 1. Unywaji wa mafuta ( naendesha km 5o kwa siku) 2. Upatikanaji wa vifaa 3. Ubora na kudumu kwa gari kwa kuzingatia mazingira ya barabara zetu Ni lipi gari zuri kati ya hizi 1. Subaru XT 2. Suzuki...
  11. Z

    Lissu ana nia njema, lakini hatoboi uchaguzi m/kiti CHADEMA

    Lissu hawezi kamwe kushinda uchaguzi Mwenye kiti CHADEMA hapo januari 2025, licha ya uchaguzi kuwa wa wazi. Sababu ni zifuatazo: 1) Sasa hivi, hii imekuwa ni vita kati ya CHADEMA kanda moja tu (asilia- Mbowe) na CHADEMA Tanzania iliyobaki (Lissu). Haitatokea kwa mazingira Lissu...
  12. kavulata

    Uchaguzi CHADEMA ni litote lizame, liwalo na liwe.

    Kwavyovyote vile chadema kuna upande hauna nia njema na chama. Wana uhakika kwa asilimia 100 kuwa chadema itapungua nguvu kuelekea October 2025 wakati wa uchaguzi mkuu. Pamoja na kulijua hilo bado kuna mtu anasema liwalo na liwe nitagombea. Ili kuepusha mpasuko Chadema inahitaji hekima na...
  13. Ngongo

    Uchaguzi Mkuu wa Mwenyekiti Taifa na wagombea wengine mpaka muda huu Mbowe anaongoza kwa 81.5%

    Heshima sana wanajamvi. Baada ya tathimini ya hali ya juu kutoka kanda 8 Mhemiwa Mbowe anaongoza 81.5% huku mshindani wake mkuu Mheshimiwa Lissu akiambulia 17.3% Wajumbe wengi wameonyesha msimamo wa kumuunga Mwenyekiti mkono kwa wivu mkubwa. Ngongo kwasasa Mikocheni.
  14. Tlaatlaah

    Kuna mgombea uongozi wa CHADEMA ngazi ya Taifa anaweza kuenguliwa kabla ya Uchaguzi asipojirekebisha

    Kwakua tayari inasemekana amejiandaa kwa hali hiyo endapo hilo litatokea, na kwamba anayo destination mpya ya uhakika ya kufanikisha malengo yake. Kwa makusudi, mgombea huyo anasema na kutenda kinyume na katiba ya chadema ili tu achukuliwe hatua, halafu kisha afanye mass defections aloipanga na...
  15. H

    SI KWELI Mnyika: Nawaonya team Lissu kuacha mpango wa kutaka kufanya fujo siku ya uchaguzi

    Watakaoanzisha fujo uchaguzi wa chadema watashughulikiwa - Mnyika
  16. K

    Pre GE2025 Uchaguzi Chadema: Mbowe anasema wapigaji kura watahojiwa mmoja baada ya Mwingine

    Akihojiwa na Kikeke nimemsikia Mbowe akisisitiza kwamba wapiga kura wataitwa mmoja mmoja na kuhojiwa hadharani (live) katika Kumchagua Mwenyekiti Mpya. Binafsi nadhan hiyo sio sawa, wangepiga kura za Siri na baada ya hapo ndio kura zihesabiwe live, hili kuepuka intimidation kwa wapiga kura...
  17. milele amina

    Kalenda za uchaguzi wa ndani wa Chadema ni hatari. CHADEMA itaendelea kutokufanikiwa na haitashika dola milele!

    Chadema ilitakiwa kufanya uchaguzi wa chama mwaka 2022 kama sehemu ya mkakati wa kujiandaa kwa chaguzi muhimu zinazokuja. Uchaguzi huu ungekuwa na umuhimu mkubwa kwa sababu ungewapa nafasi wanachama wa chama kuweka msingi imara kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024, ambao ni...
  18. Tabutupu

    Pre GE2025 Mipango ya Team Mbowe (FAM) kushinda uchaguzi, Kujitangaza ni 100%

    1. Kuna idadi ya makatibu wengi sana wanabadirishwa kipindi hiki. Makatibu ni waajiriwa ukigoma huna kazi. 2. Makatibu wa ngazi za chini kupeleka majina yenye makosa mikoani ili washi dwe kujisajili. 3. Support ya sirikali, kama ilivyo tokea kwa mbatia nccr mageuzi. 4. Vitisho vinaendelea...
  19. M

    Pre GE2025 UCHAGUZI CHADEMA: WanaCHADEMA unganeni kumtetea Mwenyekiti wenu Mbowe asidhalilishwe, Lissu anavuka Mipaka

    Liwalo na liwe this is too Much!Nikiri mimi ni Shabiki wa Lissu lakini anapoelekea hapana,kama anahama CHADEMA ahame tu namtakia Safari njema asituharibie Taasisi,sisi tutabaki Mashabiki wa CHADEMA hadi mwisho. Hakuna asiyefahamu Mchango wa Mbowe kwenye Siasa za Upinzani Tanzania kama yupo...
  20. Petro E. Mselewa

    Uchaguzi wa CHADEMA Taifa: Hawa hapa wapiga kura na wamaliza utata siku ya uchaguzi

    Ijulikane mwanzoni kabisa kuwa Mkutano Mkuu wa CHADEMA ndiyo, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, chombo mahsusi cha kumchagua Mwenyekiti na Makamu wake wawili-wa Tanzania Bara na yule wa Zanzibar. Mkutano huu mkuu wa CHADEMA hufanyika mara moja katika miaka mitano. Lakini, mikutano mikuu ya...
Back
Top Bottom