uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. J

    CHADEMA wamtupa Wenje, sasa wanajadiliana ni nani Kati ya Mbowe na Lissu atafanya Kazi kiushirikiano zaidi na Heche

    Hizo ndio hesabu zinapigwa Chadema kwa sababu Nyota ya John Heche inang'aa Sana Hivyo anaangaliwa nani ni Pacha wa Heche Kati ya Mbowe au Lissu Wenje na Mahela yake Mfumo umemtupa nje bila kutarajiwa Ahsanteni Sana 😂
  2. Petro E. Mselewa

    Uchaguzi wa CHADEMA: Yakitokea haya itakuwaje? Mpasuko hauepukiki

    Si vibaya, mwanzo mwanzoni, kuweka wazi kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa ndani na nje ya Tanzania. Lakini, ni mfuatiliaji mkubwa wa siasa za dunia nzima, nikianza na za kwetu hapa Tanzania. Pia, ni mfuasi wa hoja na mkosoaji wa maigizo na vihoja vya kisiasa. Chama cha...
  3. MamaSamia2025

    Ninawapa alama 0/100 washiriki wote wa mdahalo StarTv kuhusu uchaguzi wa CHADEMA. Tazama video.

    Huyu mfuasi wa Lissu hajui kilichotokea kwenye uchaguzi wa 2020 au kaamua kujifanya mwendawazimu? Kwa huu mdahalo wa jana hakuna mwenye nafuu kwenye hawa washiriki wanne. Wote nawapa alama 0/100. Yericko anastahili na viboko kabisa. Ntobi aliyesema CHADEMA imeanzishwa 2019 anastahili kuwekewa...
  4. M

    UCHAGUZI CHADEMA: Hotuba ya leo, kisiasa Heche amemucha mbali sana Lissu

    Nimesikiliza Hotuba ya Heche leo akitangaza kugombea Umakamu Mwenyekiti CHADEMA, nimegundua kisiasa Heche ni Mkubwa sana kuliko Lissu ingawa kiharakati Lissu kamuacha mbali sana Heche. Heche katambua nguvu ya Mbowe ndani ya CHADEMA, hotuba yake imekwepa sana kumshambulia Mbowe Binafsi na...
  5. milele amina

    Madhara ya uchaguzi wa Chadema January 2025 na Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025.

    Katika hali ya kisiasa nchini Tanzania, chama cha Chadema kinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kosa la kiufundi lililofanywa na uongozi wake. Chama hiki kimeamua kuitisha uchaguzi wa ndani wa chama katika mwaka ambao kuna uchaguzi mkuu wa kitaifa, ambao unahusisha uchaguzi wa Rais...
  6. GANJIBHAAI

    Pre GE2025 Kwa Kuwa CHADEMA haioneshI dalili ya kushika dola leo wala kesho, nafasi ndani ya chama ndo zimekuwa dili

    Mimi niko pale na popcorn zangu kama kawaida yangu, jina la Series silijui ila niliposoma majina ya actor na actress, director na producer nika_press play, Episode ya pili sasa.
  7. gcmmedia

    Uchaguzi CHADEMA na kutawala siasa za Tanzania

    Bila kujali nani atashinda ama kushindwa na nini kitatokea baada ya uchaguzi, nimeona ukubwa wa CDM katika siasa za Tz. Uchaguzi wa Mwenyekiti CDM Taifa umetawala siasa za Tanzania kwa wiki kadhaa. Hakuna Chama tawala wala vyama vingine vya upinzani ambavyo vina-trend kwa sasa. Hili ni jambo...
  8. Suley2019

    Abasi Mayala: Uchaguzi wetu usitengeneze mpasuko ndani ya chama

    Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa chama cha Mkoa wa Mwanza, Abbas Mayala amewatahadharisha wanachama, wafuasi na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa juu katika chama hicho kuepuka kutafuta kura huku wakitumia lugha ya matusi, kejeli na fedhea wakati wa kampeni. Akizungumza na Jambotv_...
  9. Suley2019

    Pre GE2025 Mbowe: Uchaguzi kila baada ya miaka mitano ndiyo uomo wa madaraka

    Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho uchaguzi kila baada ya miaka mitano ndio ukomo wa madaraka. Mbowe aliyeiongoza Chadema kwa miaka 20 tangu 2004, ameyasema hayo jana Desemba 3, 2025 katika mahojiano na Crown Media jijini Dar es Salaam. “Katika...
  10. MamaSamia2025

    Njia pekee ya kuiokoa CHADEMA ni Lissu kumuunga mkono Mbowe baada ya uchaguzi wao

    Nimetafakari sana nimeona namna pekee ya kukinusuru chama rafiki CHADEMA ni Lissu kukubali matokeo na kumuunga mkono mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe mara baada ya uchaguzi wao. Kinyume na hapo CHADEMA haitasalimika. Itavunjika vipande baada ya muda mfupi. Lissu na genge lake...
  11. Tlaatlaah

    Kuleta maridhiano na amani CHADEMA, 4rs za Dr. Samia Suluhu Hassan zitumike kutuliza joto la siasa kuelekea uchaguzi wake wa ndani ngazi ya taifa

    Kwa ushahidi wa mahojiano ya viongozi waandamizi wa Chadema Taifa hususani Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Taifa, ni wazi hekima na busara inahitajika ili kuinusuru Chadema kwenye kupasuka na kwakweli kusambaratika kabisa kwasababu za ubinafsi uliokithiri baina ya viongozi hao, uchu na tamaa ya...
  12. 4

    Kama kuna mtu kachukua pesa za watu huko CHADEMA uchaguzi umeisha kwisha rudisha .

    Wakuu amani ya Bwana iwe juu yenu, kila mmoja kwa imani yake. Leo nimeona nitoe onyo , kama yupo ambae amekwapua mpunga toka upande ule, utazitapika, uchaguzi umeishaisha . Team Mbowe mnaenda kupigwa kama Ngoma. Mtajua hamjui.
  13. sonofobia

    Pre GE2025 Kama uchaguzi ni namba, mpaka sasa Lissu ana kura 14 kati ya 21 za Njombe

    Awa ni wajumbe wa Njombe 14 kati ya 21 waliojitokeza kumuunga mkono Lissu. Mpaka sasa Lissu ameshachukua uenyekiti Njombe bado kuapishwa tu.
  14. Crocodiletooth

    Endapo kama chadema haina fedha kwa sasa hakuna ubaya uchaguzi wao ukahairishwa mpaka mwakani!

    Hii ni kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa chadema, tulimsikia akidai chadema kwa sasa haina fedha, hata za uchaguzi. -Hekima ni uhairishwe ili pia bwana mbowe anusurike 😁😁😁 #savembowe #helpmbowe #rescuembowe
  15. Mganguzi

    Pre GE2025 Kabla ya Uchaguzi Mkuu, viongozi wafuatao hawatakiwi kuendelea na nyadhifa zao. Hawana sifa na wamepoteza mvuto kwa jamii

    ( 1) Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, anaonekana kama Wizara ya Fedha ni mali yake na ni kama aliyemteua kapigwa upofu huyu mtu ni hatari sana katika kusimamia mambo ya fedha za nchi na Kuna viashiria vingi vya ufisadi tunahisi huenda Kuna Siri kubwa kati yake na aliyemteua...
  16. kibori nangai

    Pre GE2025 Kwanini Lissu analalama kila mara, kwanini usisubiri uchaguzi ushinde au ushindwe?

    Ndugu wana Jamvi ! Mimi nimevuka salama kabisa Please wale wafuasi wa Lissu na kama Lisu upo himu mwenyewe Jibu hilo swalii. Kwanini kila siku umekuwa unalalama kuhusu uchaguzi unayogombea. Mboye nayeye anagombea kama wewe Na wanotoa ushind ni wajumbe Sasa kwanini unakuwa na wasiwasi kila...
  17. Nawashukuru Sana

    Akili za mtu mweusi zinashangaza , unanunua jengo la Billion 1.6 baada ya hapo unasema hauna hela ya uchaguzi!.

    Chama Chadema kuna watu waliokosa maono . Tundu lissu , yupo sahihi kutokubali kukichangia hiki chama I agree with him. Mimi nachojua life is about priority Maisha ni swala la vipaumbele zaidi . Kulikuwa kuna haja gani ya kununua jengo la billion 1.6 wakati tunashindwa kugharamikia uchaguzi...
  18. Mudawote

    Mbowe Amuita Tundu Lissu: Njama za Kisiasa Kabla ya Uchaguzi?

    Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya CHADEMA, Kamati Kuu ya Chama inatarajiwa kukutana tarehe 6 Januari 2025 kwa ajili ya kujadili masuala mawili makubwa: uvujishaji wa taarifa za ndani ya chama na tuhuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti Taifa, Tundu Lissu. Hii imeibua maswali mengi, hasa ikizingatiwa kuwa...
  19. Mkalukungone mwamba

    Pre GE2025 Miundombinu ya Barabara na Madaraja: Wanasiasa na Hila za Kukarabati Kipindi cha Uchaguzi

    Tunaelekea Mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani Kadri tunavyokaribia mwaka wa uchaguzi mkuu, tutashuhudia mengi kutoka kwa viongozi walioko madarakani na hata wale wanaotaka kuonyesha nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Kwa kawaida, kuna tabia za viongozi fulani —...
  20. T

    Wenje: Bajeti ya Uchaguzi mkuu wa CHADEMA ni zaidi ya milioni 700

    "Chama chetu kina ruzuku ya milioni 107, huwezi kukiendesha Chama kikubwa kama Chadema kwa kiasi hicho cha fedha. Tunaenda kwenye Uchaguzi Mkuu huu ambao yeye anagombea, bajeti yake ni zaidi ya milioni 700.
Back
Top Bottom