uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Mhafidhina07

    Pre GE2025 Matokeo ya uchaguzi yanatoa taswira gani katika uchaguzi wa 2025?

    Hakuna ubishi kuwa trending ya matokeo ya hivi karibuni inaonesha CCM inashinda kwa kishindo kikubwa,kwa mwenendo huu inawezekana kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani hali ikaendelea hivi hivi lakini kuna athari kubwa ya matokeo yanayotengenezwa. Hata kama upinzani umeanguka sio kwa kasi...
  2. Waufukweni

    LGE2024 Amos Makalla: Tunakemea na kulaani matukio ya mauaji yaliyotokea kwa vyama vyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Leo Novemba 29, 2024 kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, Amos Makalla amesema: Tunakemea na kulaani matukio ya mauaji yaliyotokea kwa vyama vyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Na mimi niungane na viongozi wa dini kukemea matukio haya...
  3. D

    Alichofanyiwa huyu askari wakati wa uchaguzi jana kitampunguzia ari ya kipolisi maisha yake yote

    Ni katika kituo cha kupigia kura Mivumoni madale Majira ya asubuhi vituo vinafunguliwa! Polisi wanawathili kwa ajili kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao (kura zao) Masanduku ya kura yakaandaliwa na kupangwa kwa ajili ya upigaji kura! Wasimamizi wa uchaguzi (walimu ) wakiwa...
  4. GenuineMan

    LGE2024 Haya Matokeo ya Uchaguzi Mnayaelewa?

    Habari wakuu. Katika kupitapita mtandaoni nikakutana na haya matokeo ya uchaguzi kwenye moja ya mitaa l, Wilaya ya Ubungo. Nimeangalia naona kama namba sizielewi. Labda nyie mnisaidie Hiyo
  5. Genius Man

    LGE2024 Rais na Viongozi wengine wa Serikali ndani ya nchi kuto kulaani mauaji yaliyofanyika kwenye Uchaguzi sio sawa

    Kuna mauwaji ya kigaidi yaliofanyika kwenye uchaguzi huku wengi wameuliwa kwa kupigwa risasi, lakini cha kushangaza hatuwaoni viongozi wetu wakikemea vitendo hivyo kama vile ni vizuri hii sio sawa walio kufa ni ndugu zetu sio mifugo. Tuliona katika lile tukio la Zuchu kupigwa mawe na wananchi...
  6. B

    LGE2024 Kijana mzalendo aivaa CCM na serikali juu ya uchaguzi " wameshindwa leadership wanaogopa nini "

    ACHAMBUA MATUKIO YA UCHAFUZI WA UCHAGUZI WA TAMISEMI 2024 https://m.youtube.com/watch?v=gRp4sZuVa-A Kada wa CCM akihoji chama dola kongwe na serikali yake kwa kuteka na kuvuruga mchakato mzima wa uchaguzi wa serikali za mitaa TAMISEMI 2024, na kusema huku ni kushindwa kwa chama kongwe dola...
  7. Waufukweni

    LGE2024 Wenyeviti na Wajumbe 1,953 wa Manispaa wala kiapo cha Uadilifu baada ya kushinda Uchaguzi

    Jumla ya wenyeviti na wajumbe 1953 leo Novemba 28.2024 wameongozwa kula kiapo cha uaminifu na uadilifu na Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Illuminata Lutakana mara baada ya viongozi hao kushinda uchaguzi uliofanyika Novemva 27 mwaka huu. Akizungumza baada ya zoezi la hilo liliofanyika katika...
  8. S

    Pre GE2025 Roho, damu na manung'uniko ya watu, vitajibiwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025

    Watanzania hawaandamani lakini wanamlilia mwenye mamlaka mbinguni na duniani awaadhibu wale wote wanaogiza, kubariki na kutekeleza mauji ya watu wasio na hatia pamoja na ukatili mwingine wowote unaomwaga damu za watu. Binafsi, naamini kwakuwa wanayafanya haya hasa wakilenga uchaguzi mkuu wa...
  9. Inside10

    LGE2024 Dar: BAKWATA yahimiza ushirikiano baada ya uchaguzi

    Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka Watanzania wote kuungana na kushirikiana mara baada ya uchaguzi wa serikali kufanyika kwa amani. Akizungumza kwa niaba ya Baraza hilo, Katibu Mkuu wa BAKWATA, Alhaji Nuhu Mruma, aliwasihi wananchi kuwapa ushirikiano viongozi waliochaguliwa...
  10. S

    LGE2024 Matokeo ya uchaguzi - Wapinzani wameshinda wapi?

    Naona kimya kingi. Sijaona hata sehemu moja wapinzani wameshinda. Naomba mwenye matokeo please... Hapo ulipo wewe chama gani kimeshinda?
  11. S

    Hesabu ndogo sana; Kwanini Serikali iliwaamuru Polisi wasimtaje mmiliki wa jengo lililoporomoka Kariakoo hadi uchaguzi wa serikali za mitaa uishe

    Ndivyo watawala wa chama tawala wanavyoendesha nchi hii. Makosa yanayofanywa na watu wao huwa kila jitihada itafanywa kuyafunika. Na hawaoni aibu juu ya hili, huwa wanasema waziwazi ukiwa mtu wao watakulinda. Kwa maneno mengine kuwa mtu wao kunakufanya uwe juu ya sheria. Na kibaya zaidi, Polisi...
  12. Z

    LGE2024 Mbowe ajiuzulu kwa kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

    Namshauri Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ajiuzulu kwa kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. Mwenyekiti asitafute kisingizio kingine, anachotakiwa ni kujiuzulu kwa maslahi ya Chama.
  13. R

    LGE2024 Anaandika Lyenda kutoka X: SHIDA ZA UCHAGUZI 2024

    LYENDA (iamLyenda) posted at 5:57 PM on Wed, Nov 27, 2024: Tunachukua fomu kwa SHIDA. Tunarejesha fomu kwa SHIDA. Tunateuliwa kwa SHIDA. Tunafanya kampeni kwa SHIDA. Tunapiga kura kwa SHIDA. Mawakala wanasimamia kura kwa SHIDA. Tunahesabu kura kwa SHIDA. Tunatangazwa kwa SHIDA. Yaani...
  14. Waufukweni

    LGE2024 Njombe: Mwenyekiti wa CHADEMA, Rose Mayemba alivyoliamsha baada ya kubaini madudu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Njombe Rose Mayemba amedai kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana, Novemba 27.2024 nchini kote haukuwa uchaguzi kama ilivyodhaniwa badala yake ilikuwa ni oparesheni kuwashughulikia wapinzani nchini Rose ameeleza hayo...
  15. mwanamwana

    LGE2024 Kagera: Wananchi waipa CCM Katerero 100% uchaguzi Serikali za Mitaa

  16. Mindyou

    LGE2024 Arusha: Mgombea wa CUF ashinda Uchaguzi Kijenge Kusini, alalamikia kuzuiwa kwa mawakala wa chama chao

    Wakuu, Katika kipindi hiki ambacho matokeo yanaendelea kutangazwa, mengine mapya yanaibuka. Aliyekuwa mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) mshindi wa Uchaguzi katika mtaa wa Kijenge Kusini, kata ya Kimandolu, jijini Arusha, Shaaban Suleiman Mzava, ameeleza malalamiko yake juu ya mawakala wa...
  17. Mindyou

    LGE2024 Mwanza: Mawakala wa Uchaguzi wapongeza zoezi la kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Wakuu, Huko Misungwi mkoani Mwanza Mawakala wa Uchaguzi wapongeza zoezi la kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Soma pia: Matokeo ya Uchaguzi Mwanza yaanza kutangazwa, CCM yaongoza maeneo mengi ikifuatiwa na CHADEMA Ina maana kuwa hawa mawakala hawakuona changamoto zilizojitokea...
  18. Roving Journalist

    LGE2024 Matokeo ya Uchaguzi Mwanza yaanza kutangazwa, CCM yaongoza maeneo mengi ikifuatiwa na CHADEMA

    Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya mitaa Jijini Mwanza yameanza kutangazwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionesha kuongoza kwenye vituo vingi Wilayani Nyamagana. Aidha, licha ya baadhi ya Mitaa Wilayani Nyamagana na kushuhudiwa Wagombea wa CCM wakitangazwa kuongozwa Kwa...
  19. Burure

    LGE2024 Madudu kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2024

    Jana tumepata wasaa wa kushuhudia Uchaguzi wa Serikali za mitaa tuliosubiria kwa muda mrefu. Licha ya kuwa umefikia idadi ya chaguzi Tisa (9) Toka uanze kufanyika hapa nchini lakini bado kuna Mapungufu makubwa. Mosi ni msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni TAMISEMI ambaye na yeye anahusika kwenye...
Back
Top Bottom