uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. M

    Kama kuna hitilafu na wizi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, itakuwaje kwenye uchaguzi mkuu?

    Chama kama kinakubalika na wapiga kura Kuna haja Gani ya kutumia nguvu kubwa namna hii na wizi wa kura ata uchaguzi wa serikali za mitaa? Aya ni maajabu mengine nayashuhudia Tanzania Kwamba kura zishapigwa kitambo waliopiga awajulikani Daah hii kitu inaitwaje sijaelewa kabisa ni mambo ya aibu...
  2. Mtoa Taarifa

    LGE2024 Waziri Mchengerwa: Taarifa nilizonazo hadi sasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaendelea Vizuri na kwa Hali ya Amani nchi nzima

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewaelekeza wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi kuwasaidia wapiga kura kusoma orodha ya majina vizuri ili wote waliojiandikisha wapate fursa ya kupiga kura. Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya...
  3. Robert Heriel Mtibeli

    LGE2024 Kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea wa upinzani kumefanya zoezi la uchaguzi kukosa mvuto kwa wananchi.

    Habari za uchaguzi Wakuu! Nafikiri siku ya Leo imeenda kinyuma na lengo lilivyopangwa. Serikali iliiweka siku ya Leo kama siku ya mapumziko ili kutoa fursa kwa watu kupata muda wa kwenda kupiga Kura katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa. Lengo lilikuwa zuri lakini likapoteza maana baada ya...
  4. Mindyou

    LGE2024 Lindi: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa apiga kura kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa

    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Novemba 27, 2024 ameshiriki katika zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa, Lindi. Akizungumza baada ya kupiga kura ambapo aliongozana na Mkewe Marry Majaliwa...
  5. The Watchman

    LGE2024 Mchengerwa: Matokeo ya uchaguzi kutangazwa ndani ya saa 72

    Wakati upigaji kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ukiendelea maeneo mbalimbali nchini, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amesema matokeo yote yatakuwa yametoka ndani ya saa 72. Pia, Mchengerwa...
  6. Waufukweni

    LGE2024 Geita: Utata majina ya wapiga kura, mkurugenzi atoa ufafanuzi

    Mpiga kura Mtaa wa Mwatulole katika kituo cha kupigia kura Mwatulole Center ambaye awali alilalamika kutoona jina lake, hatimaye amekiri mbele ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Geita Mjini, Yefred Mnyenzi kuwa jina lake limeonekana na ametimiza haki yake.
  7. Waufukweni

    LGE2024 Kilimanjaro: Naibu Waziri Ummy Nderiananga apiga kura Kiriche katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga ameungana na wananchi wa Kitongoji cha Kiriche kupiga kura mapema leo Novemba 27, 2024 kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Makuyuni, Kitongoji cha Kiriche...
  8. Z

    LGE2024 Nimevunjika moyo na uchaguzi huu wa leo

    Leo majira ya saa 5 asubuhi nimeenda kupiga kura (uchaguzi wa wenyekiti) Mimi sio mwanasiasa na sijui hata majina ya wanao gombea, lakini nilijipanga kuenda kuwachagua wagombea wa upinzani pekee. Nilipofika nimekutana na mambo haya. Nilianza kwa kutafuta jina langu kwenye makaratasi yaliyo...
  9. The Watchman

    LGE2024 Chalamila: Kumbe Kuna uchawi kwenye uchaguzi, nimeshangaa kusikia huo muujiza wa watu kupiga kura kabla vituo havijafunguliwa

    “Kuna vyombo vya habari vimetangaza kuwa kuna mahali kura zimepigwa kabla ya vituo kufunguliwa nimeshangaa kumbe kuna Uchawi kwenye Uchaguzi maana nimeshangaa kusikia huo muujiza wa watu kupiga kura kabla vituo havijafunguliwa" Soma pia: Kituo cha Kupigia Kura cha Lugalo, Kawe chakutwa na...
  10. Mzee wa Code

    LGE2024 Dodoma: Baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi hawapo vituo vya kupigia kura. Mawakala wa vyama waingia mitini, askari wamekuwa wasimamizi wazuri

    Baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi hawapo katika Vituo vya Kupigia Kura Jijini Dodoma, Mfano ni Kituo cha kupigia Kura Ofisi ya kata ya Chamwino hakuna msimamizi wa uchaguzi na Askari wote kwa pamoja hawapo kwenye vituo vya kupigia kura, Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura Mtaa wa nduka chamwino...
  11. Waufukweni

    LGE2024 Dodoma: RC Senyamule apiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa

    Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepiga kura katika kituo cha shule ya msingi Dodoma Mlimani iliyopo Mtaa wa Salmini kata ya Tambukareli. Baada ya kupiga kura amezungumza na Waandishi wa habari ambapo amewahimiza wakazi wa Dodoma kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza...
  12. Mindyou

    LGE2024 Chamwino, Dodoma: Rais Samia apiga kura katika Kitongoji cha Sokoine. Asisitiza amani na majibu kutoka kwenye masanduku

    Wakuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye foleni tayari kwa kupiga Kura katika Uchaguzi wa Seikali za Mitaa katika kitongoji cha Sokoine Kijiji cha Chamwino Mkoani Dodoma, leo tarehe 27 Novemba, 2024. === Samia amepiga Kura katika Uchaguzi wa Seikali...
  13. T

    LGE2024 Lema: Hakuna mazingira huru kabisa ya uchaguzi, ila imenipasa kutimiza wajibu

  14. Akilindogosana

    LGE2024 Nape Nnauye apewe maua yake kwa kuongea ukweli kuhusu mbinu Haramu za kushinda uchaguzi

    Nape Nnauye apewe maua yake kwa kuongea ukweli, kuhusu mbinu Haramu za kushinda uchaguzi. Leo watanzania tunajionea Mbinu Haramu zinazotumika kushinda uchaguzi. Pamoja na ubaya wake na mapungufu yake. Ila apongezwe kwa kuongea UKWELI. Pia soma Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo...
  15. The Watchman

    LGE2024 Simiyu: Karatasi za kupigia Kura zakamatwa zikiwa zimewekewa tiki kwa wagombea wa CCM

    Anaandika mkurugenzi wa mawasiliano na mambo ya nje wa CHADEMA John Mrema kupitia mtandao wa X "Karatasi za Kupigia kura zikiwa tayari zimekwa tiki kwa wagombea wa CCM zimekamatwa Mkoa wa Simiyu Jimbo la Bariadi Mjini Mtaa wa Ngashanda kata ya Malambo" Soma pia: Mbinu za wizi wa kura...
  16. Papaa Mobimba

    LGE2024 Mikumi: Kata 8 hazijaanza kupiga kura, msimamizi adaiwa kutopokea simu

    Wakati zoezi la upigaji wa kura za kuchagua viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa likiwa limeanza tangu saa 02:00 asubuhi nchini, hali ni tofauti kwa jimbo la Mikumi, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro ambapo inadaiwa kuwa kata nane (8) kati ya 15 za jimbo hilo zoezi la upigaji wa kura...
  17. KiuyaJibu

    Teknolojia katika Uchaguzi

    Nilitegemea kujiandikisha 1. Online (kwa mtandao) na 2. Kwenda kwenye vituo vya kujiandikisha. Sasa hadi wakati huu wa kupiga kura bado mtu analazimika kwenda mahali alipojiandikisha?! Kutekelezwa kwa Na. 1, maana yake yote yangefanyika popote mtu alipo bila tatizo lolote; kwa hali ilivyo...
  18. Mindyou

    LGE2024 Mbeya: Mkurugenzi adaiwa kusitisha Uchaguzi eneo la Ubaruku bila taarifa yoyote

    Wakuu, Sarakasi za Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa zinaendelea huko Mbeya mambo yameanza kuchanganya! Zoezi la upigaji kura katika kata ya Ubaruku limesitishwa kwa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi. Hadi kufikia saa tatu asubuhi, hakuna taarifa rasmi au maelezo ya kina yaliyotolewa kuhusu sababu ya...
  19. Don Gorgon

    LGE2024 Sosopi: Tunaijua mipango miovu ya CCM kuzuia Uchaguzi

    Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA taifa Patrick Ole Sosopi Patrick ole Sosopi akielezea uovu waliokutana nao wakati wa kuapisha mawakala wa chama hicho wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kata ya Idodi ,Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
  20. M

    LGE2024 Zanzibar hakuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tupeane elimu kidogo kuhusu Chaguzi

    Hivi karibuni huko Tanzania Bara kumekuwa na mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo leo Novemba 27, 2024 Wananchi wanapiga kura. Mimi kama mdau wa siasa na mifumo ya Uchaguzi Zanzibar nimekuwa nikipokea maswali mengi kuhusu kwanini Zanzibar kumekuwa hamna shamrashamra za Uchaguzi kama...
Back
Top Bottom