Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.
Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.
Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.
Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
MBUNGE GHATI CHOMETE: CCM IMEJIPANGA VIZURI, LAZIMA ITASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe. Ghati Zephania Chomete, tarehe 26 Novemba 2024 ahitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwaombea kura wagombea wa CCM Wilaya ya Musoma...
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Tundu Lissu, akielezea hali waliyokutana nayo wakati wa kuapisha mawakala wa chama hicho wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Tarafa ya Ikungi, wilayani Ikungi mkoa wa Singida, leo Novemba 26, 2024.
Nchi yetu ya ajabu sana, iliyojaliwa kuwa na viongozi wa ajabu pia, viongozi wanaobariki maovu alimradi maovu hayo yawe ni dhuluma ya kuwanufaisha CCM.
Fikiria, waziri Mchemgerwa ndiye mwenye jukumu la kutengeneza kanuni za uchaguzi, akatengeneza kanuni za hovyo kabisa, ikiwemo ile ya kifungo...
Tumeona ukiukwaji mkubwa katika kujiandikisha, kuenguliwa wapinzani, /kuteuliwa. kuwekewa mapingamizi ya uongo na kweli, kuapishwa wamekataliwa, sasa UPINZANI mnadhani kesho ndiyo CCM watatenda haki?
Kwa wale wote tutakao shiriki uchaguzi muhimu mno na wa maana sana wa serikali za mitaa,
Nawatakia nyote matumizi sahihi uhuru na haki ya kikatiba, kwa kuchagua viongozi makini na watakao saidia kuchochea mageuzi na maendeleo katika mtaa au kijiji unachoishi.
Hongera kwa uchaguzi wa...
Saa chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji kesho Jumatano tarehe 27 Novemba, 2024 Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe mapema leo Novemba 26, 2024 limefanya doria za magari na miguu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Songwe ikiwemo mji wa Tunduma wilaya ya...
Wananchi wa jimbo la Lupembe wameeleza utayari wao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika leo Novemba 27, 2024 Nchi nzima huku wakiweka wazi Matarajio yao kwa viongozi wapya watakaochaguliwa
Wananchi hao akiwemo Fikiria Vicent Kisogole, Salvina Barton Mpolo na Martina Isdol...
Wakuu.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu anazungumza muda huu huko mkoani Singida kuhitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,
Fuatilia uzi huu kujua nini kinaendelea
Tundu Lissu amesema kuwa mara ya mwisho Tanzania kufanya Uchaguzi ilikuwa nwaka 2014 kwani mwaka 2019...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Novemba 2024.
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na abiria...
Wakuu,
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya mwananchi yeyote atakayeonesha viashiria vya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika kesho Novemba 27, 2024 nchini.
"Siku ya kesho ya kupiga kura kila mtu atunze amani...
Msije baadaye mkasema mmedhulumiwa kura au kura zimeibwa.
Mnapoingia uwanjani ni kuwa mmekubaliana na sheria na taratibu za mchezo. Hakuna excuses za kipuuzi. Ni kupambana na kukubaliana na matokeo. Hakutakuwa na excuses ni mapambano. Mshindi apatikane.
Maana hamchelewi kusema mlinyanyaswa...
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amemuonya mtendaji wa Kijiji cha Angalia kutopendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) wajibu wake nikutumikia wananchi sio ubaguzi wa itikadi katika uchaguzi.
Kauli hiyo ameitoa baada ya mtendaji huyo kuzuia mikutano ya chama hicho kutumia maeneo ya Umma, Semu...
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Ndg.Shemsa Mohamed ameendelea na ziara yake yenye jina la Siku Saba za Moto ambapo tarehe 25 Novemba, 2024 aliweka kambi katika Jimbo la Kisesa akitembelea Kata ya Bomani ,Kata ya Isengwa na Mwasengela.
Ndg.Shemsa amekutana na kuzungumza na...
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kimesema kimejipanga kwa njia zote kuhakikisha kinalinda amani kabla ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi ikiwemo kuwadhibiti wale wote wenye nia mbaya (ovu) ya kutaka kuvuruga Uchaguzi kwa kuanzisha Vurugu.
"Asitokee mtu yeyote au kundi kupanga njama za kutaka...
Inajulikana wazi kuwa CCM hawawawezi CHADEMA katika sanduku la kura, hivyo imeweka nguvu kubwa kwenye figisu na dhulma.
CCM tayari wameonesha taa nyekundu ktk hatua za mwanzo kwa kuwaengua wagombea wa chadema 16,0000, na baada ya rufaa wagombea 5,000 tu ndiyo wamerejeshwa. Pia viongozi wa...
Ukiniuliza mimi ntasema mambo yangu matatu; siyo mageni sana lakini naamini yanaweza kuisadia CHADEMA kujiandaa na uchaguzi mkuu mwakani. Na wewe kama unayakwako yaweke labda katika wastani yatapatikana mambo matatu makubwa.
1. Itangaze mapema kama msimamo wa chama kuwa wagombea wote wa ubunge...
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza jijini Dar es salaam kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mnamo mwezi Novemba 27, 2024 amesema hali ya usalama mkoa wa Dar es salaam ipo vizuri na mtu yeyote atakayejaribu kuharibu amani iliyo siku ya uchaguzi hatoachwa salama na...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewahimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Dkt. Biteko ametoa rai hiyo leo Novemba 25,2024 akiwa mkoani Geita ambapo amesema uchaguzi huo ni muhimu hususan kwa ukuzaji wa demokrasia...
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo wa Jimbo la Tunduru Kaskazini mkoani Ruvuma, Yasin Mohamed Mawila, ametoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la udanganyifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Akizungumza Jumapili, Novemba 24, 2024, kwenye mkutano wa kampeni...
Mussa Azzan Zungu, ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, ameendelea na kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Upanga Magharibi, jijini Dar es Salaam. Amengia kuogea na wananchi mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba, Zungu amewanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.