uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. The Watchman

    LGE2024 Askofu Tanga: Siku kabla ya kupiga kura msisahau kuombea Uchaguzi wa mwaka huu kwani ni maandalizi ya uchaguzi wa mwakani

    Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika novemba 27 mwaka huu, Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Dayosisi ya Tanga Maimbo Mndolwa ametoa wito kwa watanzania kuchagua viongozi wakufaa bila kujali itikadi za vyama vya siasa. Askofu Mkuu Maimbo...
  2. Stephano Mgendanyi

    LGE2024 Tamko la CCM kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

    TAMKO LA CCM KWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandaa tamko maalum kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024. Uchaguzi huu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, kwani utahusisha kuchagua wenyeviti wa mitaa, vijiji, vitongoji, wajumbe wa kamati za...
  3. Stephano Mgendanyi

    Samia Kagera CUP Yahitimishwa kwa Kuwahamasisha Vijana Kushiriki Uchaguzi Serikali za Mitaa

    Mashindano ya Samia Kagera Cup 2024 yaliyowakutanisha vijana na wananchi wa Mkoa Kagera kwa kuwahamasisha kushiriki kikamilifu na kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024, kushiriki shughuli za maendeleo, kuonyesha vipaji pamoja na kuongeza ushiriki...
  4. Nehemia Kilave

    LGE2024 Tamko la kutangaza siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa siku ya mapumziko la mwaka 2024

    TAMKO LA KUTANGAZA SIKU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA SIKU YA MAPUMZIKO LA MWAKA 2024 KWA KUWA kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35, kinampa Rais mamlaka ya kutangaza siku yoyote kuwa siku ya mapumziko kama nyongeza ya siku zilizoainishwa kwenye Jedwali la Sheria...
  5. Waufukweni

    LGE2024 Wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi 1,213 wapewa mafunzo na kula kiapo

    Kuelekea siku ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa, wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi 1,213 wamepewa mafunzo na kuapishwa kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo utakaofanyika siku ya Jumatano ya Novemba 27, 2024. Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa amewasihi...
  6. Waufukweni

    LGE2024 DC Malinyi, Waryuba awahakikishia wananchi Usalama na Amani kipindi cha Uchaguzi

    Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba ameyasema hayo wakati aliposhiriki uchaguzi marathoni Wilayani Malinyi kwa lengo la kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura Novemba 27, 2024. DC Waryuba amesema kuwa huu ni wakati sahihi kwa wananchi kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba...
  7. Waufukweni

    LGE2024 Kayandabila: Uchaguzi hauna uzoefu, fuateni mafunzo ya Uchaguzi wa mwaka huu

    Wasimamizi wasaidizi zaidi ya 600 wa vituo vya kupiga kura uchaguzi Serikali za Mitaa wa jimbo la Tabora wametakiwa kutokutanguliza uzoefu wa usimamizi wa chaguzi zilizopita katika uchaguzi wa mwaka huu badala yake wafuate mafunzo na mwongozo wa usimamizi wanaopewa ili kuweza kufanikisha zoezi...
  8. Waufukweni

    LGE2024 Uchaguzi Manispaa ya Songea: Vituo 210, Wagombea 987 tayari kwa kinyang’anyiro

    Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Songea, Wakili Bashir Mhoja, ametoa taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi ulio karibu kufanyika. Akizungumza na waandishi wa habari, Mhoja amesema kuwa hali ya utulivu inaendelea kutawala katika mji huo na kwamba kampeni za uchaguzi zinaendelea kama...
  9. lugoda12

    LGE2024 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa: Kura yako ni muhimu, usiache kupiga kura

    Kura yako ni muhimu, jitokeze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27.11.2024, vituo vitafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi jioni.
  10. Bams

    Uchaguzi Serikali za Mitaa, Tunawapongeze Viongozi wa Dini Wanaokemea Udhalimu.

    Toka mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulipoanza, tumeshuhudia mambo mengi ya hovyo yakifanywa na TAMISEMI, chini ya Waziri Mchengerwa, kuanzia kutunga kanuni mbaya za kusimamia uchaguzi, kama ile ya kuwalinda wasimamizi wa uchaguzi wasishtakiwe wanapofanya makosa hata ya kijinai wakati...
  11. Bams

    LGE2024 Uchaguzi Serikali za Mitaa, hongereni viongozi wa Dini kwa kusimama katika Imani

    Toka mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulipoanza, tumeshuhudia mambo mengi ya hovyo yakifanywa na TAMISEMI, chini ya Waziri Mchengerwa, kuanzia kutunga kanuni mbaya za kusimamia uchaguzi, kama ile ya kuwalinda wasimamizi wa uchaguzi wasishtakiwe wanapofanya makosa hata ya kijinai wakati...
  12. J

    LGE2024 Wajibu wa Wadau wa Uchaguzi wakati wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    1. Jeshi la Polisi 2. Vyama vya Siasa - 3. Wananchi - 4. Msimamizi wa Uchaguzi Chanzo: TAMISEMI 2024
  13. Mindyou

    LGE2024 Geita: Maneno haya ya Dotto Biteko kwenye Uchaguzi si mageni jijini. Labda kwa mgeni jijini. Kwa wenyeji tushayazoea

    Wakuu, Nimekutana na clip hii ya Dotto Biteko akizungumzia malengo ya CCM kwenye Uchaguzi huu. Tunajua nini wataenda kufanya. Ni kama marudio ya 2019. Ushindi wa asilimia 99.99
  14. Mhaya

    Pre GE2025 Vitu vya kuzingatia na vya kutokufanya kwa Jeshi la Polisi wakati wa uchaguzi au kipindi cha Siasa

    Habari za siku mbili tatu wakuu na wananzengo hapa jukwaani? Hi video ni ile ya uchaguzi Mkuu 2020 nimeitumia hapa kutaka kusema kitu kuhusu hizi chaguzi Unajua kwa kawaida kabisa ni wazi Majeshi yetu hayatakiwi kuchagua upande, majeshi yetu hayatakiwi kuonesha hisia zao wazi kisiasa...
  15. mwanamwana

    LGE2024 Abdul Nondo: Chini ya ACT Wazalendo hakuna raia atachukuliwa na Uhamiaji bila mwenyekiti kupata taarifa, akumbushia kutekwa kwake

    "Tunajua mna tatizo kubwa la uhamiaji. Hata mimi walishawahi kunisumbua, wakaniambia mimi si raia wa nchi hii na kunitaka nipeleke vyeti vya babu yangu aliyemzaa babu yangu. Lengo lao lilikuwa kunisumbua tu, lakini chama changu cha ACT kilisimama nami mpaka mwisho. Hivyo kupitia ACT, hakuna raia...
  16. L

    LGE2024 Mbowe na wenzake wamekiuka Kanuni ya 49 (k) ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, adhabu yake ni faini au jela mwaka au vyote viwili

    Nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni, miongozo nk, vyama vya siasa vilitakiwa kuwasilisha ratiba zao za kampeni na kule Songwe alikokamatwa Mbowe na genge ratiba ilikuwa inaonyesha kuwa ACT wangefanya mkutano, Mbowe kwenda kufanya mkutano kwenye ratiba ya ACT ilikuwa ni...
  17. Jaji Mfawidhi

    Haiwezekani kubaki mwaminifu kwenye Mapenzi!

    Siku zote utakutana na wanawake wenye mvuto kuliko mwanamke wako, utakutana na wanawake wenye vibes zaidi, utakutana na wanawake ambao wana habari zaidi, utakutana na wanawake wanaofanya kana kwamba wanamjali kuliko mwanamke wako. Pia ukiwa mwanamke utakutana na wanaume ambao ni matajiri sana...
  18. Mindyou

    LGE2024 Msimamizi Wa Uchaguzi Dodoma: Maandalizi ya Uchaguzi yamekamilika na wagombea 326 kutoka vyama 14 vitashiriki!

    Wanabodi, Kuna hii taarifa kwamba kuna vyama takriban 14 ambavyo vimejitokeza kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa huko mkoani Dodoma. Hivi ukitoa CCM, CHADEMA na ACT hivyo vyama vingine ni vipi? Au ndo matawi ya CCM? ==========================================================...
  19. Mindyou

    LGE2024 Msimamizi Wa Uchaguzi Katavi: Msifungue vituo kabla ya saa mbili, saa kumi askari atasimama nyuma ya mtu wa mwisho.

    Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya vituo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia muda wa kufungua na kufunga vituo vya kupigia kura ili kuepusha vurugu zinazoweza kutokea katika vituo hivyo. Akizungumza mara baada ya kufanga mafunzo hayo Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya...
  20. Jamaa Fulani Mjuaji

    Kero kuhusu ajira za muda kwa watumishi wa umma, hususan walimu

    Katika hali ya sasa ambapo ukosefu wa ajira kwa vijana nchini Tanzania unazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka, inasikitisha kuona kwamba serikali bado inaajiri watumishi wa umma, hususan walimu, kushiriki kwenye ajira za muda kama vile kusimamia uchaguzi, sensa, au kuandikisha majengo. Hii imekuwa...
Back
Top Bottom