Ninaomba kujua ulipaji wa ushuru wa bandarini ukoje maana nahitaji kuagiza mashine toka China, mashine bei ni $ 2000 dimension zake urefu ni futi 8 upana fut 3 na kimo ni futi 4 lkn nashindwa kutokana na kutokujua gharama ya ushuru bandarini ukoje isije ikawa gharama kubwa zaidi ya mashine...
Siamini kabisa kwamba kuna wasomi walikaa sehemu wakajadili na kulipana posho za kikao kwamba:
Magari yanayodaiwa ushuru wa maegesho (parking) Yaanze kufungwa minyororo ili kushinikiza wamiliki kulipia tozo hizo.
Huu ni utaratibu wa hovyo sana
1. Huu utaratibu ni Hovyo kwasababu...
Naombeni msaada hivi ukiagiza bidhaa online mfano pieces 50,000 za urine container kutoka Alibaba zenye thamani mfano sh. 2500000 ushuru wake hapa bongo unaweza fika shilingi ngapi
Sisi Wafanyabiashara wa mbao tuliopo Mbalizi, Mbeya Vijijini tuna malalamika kuhusu Watoza Ushuru wanaosimama kwenye mageti.
Wanatengeneza mazingira ya rushwa kwa kutaka kutupiga faini na kututaka tukate ushuru wa TP (Transportation Permit) mara mbilimbili.
Utaratibu uliopo tunaopewa na Wakala...
Ndugu zangu habari za leo? Bila shaka nyote mko salama, wale walio na magonjwa au shida mbalibali mwenye enzi Mungu awafanyie wepesi.
Ndugu zangu ninaomba kufahamu kuhusu ushuru wa boat ya uvuvi ya ukubwa wa 15m kwa 3m pamoja na upatikanaji wa vibali vya uvuvi.
USHURU MAEGESHO + TRAFFIC PENALTY JIJINI DAR VIMEKUWA KERO KUBWA SANA
Tunaomba wizara husika ziangalie upya hizi taratibu
1. Gari moja inaweza kuta ina madeni ya miaka hadi 3.
2. Kiwango ni kukubwa mno, madeni yasiolipika.
3. Inaturudisha kwenye tatizo la zamani la Motor Vehicle...
Habari wakuu.
Kuna mtu wangu yupo nje ya nchi anataka kunitumia smartphones tano (5) brand new. Utaratibu wa ushuru ukoje pindi zikifika nchini? Nadhani kuna wakati serikali iliondoa import duty ila ikarudisha tena. Naomba kuwasilisha.
Wakuu habari.
Nimesikia vibaya au vipi kwamba kwenye bajeti iliyopitishwa bungeni hivi leo kwa kishindo Kila kilo ya sementi itatozwa ushuru shillingi mia mbili.
Sasa kilo hamsini itauzwa shilling ngapi kama ushuru tu itakuwa elfu kumi?
Duh kule bado mafuta Lita ushuru mia.
Tunatoboaje?
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaanza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia tano kwenye magari yenye uwezo wa injini (Engine Capacity) wa kati ya 1,000 CC hadi 2,000CC.
“Ushuru huo utatozwa ili kuwianisha na magari mengine yenye ukubwa unaofanana...
Ili kuiwezesha Nchi kuwa na Sera za Kodi zinazotabirika na kuweka mazingira bora ya uwekezaji, Serikali imependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru Kwa kuanzisha utaratibu wa kurekebisha viwango vya Ushuru wa Bidhaa kila baada ya miaka mitatu (3)
Kuanzia mwaka wa fedha 2023/24...
Huwa nasema mara nyingi sana kwamba Tanzania hii Serikali inadekeza sana Watu hasa wa Mijini..
Imagine mtu anakataa tozo ya mafuta Shilingi 100 ambayo inatakiwa Kujengea Barabara ila Barabara anazitaka.
Kama Mfanyakazi wa Umma anakatwa Asilimia 3% Kila Mwezi hiyo ni zaidi ya 10,000 Kila Mwezi...
WAZIRI ASHATU KIJAJI AAHIDI KUTATUA KERO YA UTOZAJI USHURU KWA WAFANYABIASHARA WADOGO MKOA WA MANYARA
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewaahidi wafanyabiashara wa soko la Mchele la Magugu mkoani Manyara kufanyia kazi kero ya utozaji wa ushuru wa Shilingi...
Ripoti ya robo mwaka unaoishia Machi 2023 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha gharama za ushuru wa bando la intaneti zimeongezeka ikiliganishwa na kipindi kama hiko Machi 2022.
Machi 2022 kwa kila MB moja ushuru uliokuwa unakatwa ni shilingi mbili ambayo imeongezeka hadi...
Wengi wao.....
1. Wana Hasira (Usununu)
2. Wakali
3. Wajeuri (Ngumi Mkononi)
4. Wana PhD"s za Matusi
5. Hawajui Kutabasamu
6. Wana Stress na Frustrations
7. Mabingwa wa Kugongea Misosi ya Watu na Kulazimisha kupewa Lifti nyakati za Jioni / Usiku
Kuna Mmoja nimekutana nae mahala nimemchanganyia...
Wadau anaejua taratibu za ushuru wa bidhaa pale bandarini kama umenunua vitu zanzibar inakiwaje anijuze. Kama wanachaji kwa asilimia za bei ya bidhaa au wanakuangalia unafananaje ndio wanakuchaji.
Nataka nikafanye shopping huko naona vitu bei imekaa poa.
Makusanyo ya maegesho ya magari jijini Dar es Salaam yanayokadiriwa kufikia Sh 25 milioni kwa siku huenda yakatoweka kutokana na mgomo wa wakusanya ushuru huo kutoka kampuni ya Excel Parking Service (EPS).
Wakusanya ushuru hao wamegoma wakidai kutolipwa mishahara yao miezi miwili.
Tofauti na...
Nimejaribu kuisoma kanuni iliyotolewa na TRA ya kukokotoa kodi inayolipiwa bidhaa zinaoingizwa toka nchi za nje nimepata maswali mengi sana.
Mojawapo ya maswali ni kwanini Ushuru wa Forodha unatozwa Ushuru wa Bidhaa pia unatozwa Ushuru wa Ongezeko la Thamani (VAT)?
Kwanini Ushuru wa Bidhaa...
sasa bandiko kama hili linajibu swali la bwana yule mliyemtoza mamlioni kwa pampas na viguo vya mtoto. Hamuwezi kutumia mifano rahisi kuwafanya wananchi waelewe?
Mfano shida ya watanzania wengi iko hapa;
Mtu kanunua gari kwa dola 1000 sawa na TZS 2,270,000 inakuwaje anaishia kulipa TZS...
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri,
Kwanza kabisa mimi na raia mwema na sina nia ya kukwepa ushuru wa tarura tena ukizangitia fees zao ni ndogo sana kwa sasa (reasonable).
Niendelee, leo nimeangalia ushuru wa maegesho kwenye website ya TARURA nakukuta nadaiwa nilipoangalia maelezo ya Tiketi...