Desturi ya kuoana kwao.
Wazaramu wakitaka mke, kwanza huenda kwa mjomba wa yule mwanamke, akampa khabari—ya kama: "Mimi namtaka mpwa wako kumwoa." Na yule mjomba humjibu: "Vema, lakini nataka mkalio wangu wa maneno, ndipo nikujue kama wewe mkwe wangu." Basi yule mume hutoa reale moja au mbili...