zitto kabwe

Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe (Zitto Kabwe)
Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe, maarufu kama Zitto Kabwe, ni mwanasiasa kutoka Tanzania kutoka chama cha ACT-Wazalendo. Zitto aliwahi kuwa mwanachama wa Chama Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) toka mwaka 1992 mpaka 2015 alipoachana na chama hicho.

Zitto ameshika nafasi ya Kiongozi wa Chama ACT-Wazalendo kwa miaka 9, mpaka March 2024 ambapo nafasi hiyo imechukuliwa na Dorothy Semu. Amewahi kuwa Mbunge wa Tanzania kwa vipindi viwili kuanzia 2005 mpaka 2015 akiwakilisha Jimbo la Kigoma Kaskazini.
  1. Zitto

    Zitto Kabwe: Kwaheri John Magufuli, Buriani Tingatinga

    Kwa Heri John Magufuli, Buriani Tingatinga Zitto Kabwe Imenichukua karibu wiki nzima kuandika, japo kidogo, kukuaga Rais Magufuli. Unajua kwanini ninapata ugumu kuandika japo napenda sana kuandika tanzia kiasi huwa nawaza nani ataandika tanzia yangu na ataandika nini. Lakini pia imenichukua...
  2. ACT Wazalendo

    Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

    MAHINDI YA TANZANIA NI SALAMA. Tanzania na Kenya Zimalize Mzozo Kidiplomasia - Zitto Kabwe Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndg. Zitto Kabwe ameitaka Serikali ya Tanzania kukaa mezani na Serikali ya Kenya kumaliza mzozo wa Soko la Mahindi ya Tanzania nchini Kenya. Ndugu Zitto amesema...
  3. J

    Changamoto: Mazrui aapishwa kuwa Waziri wa afya Zanzibar; Je, Zitto Kabwe atamshawishi alete chanjo za Corona?

    Waswahili husema mchawi mpe mwanao amlee. Nassor Mazrui ameapishwa leo kuwa Waziri wa Afya wa SUK Zanzibar. Zitto Kabwe ambaye ni KC wa ACT Wazalendo siku zote amekuwa mstari wa mbele kuponda namna Serikali inavyoshughulikia suala la Corona na amekuwa akitumia zaidi mitandao ya kijamii hasa...
  4. J

    Zitto Kabwe: Jina la Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar tulilompelekea Rais Mwinyi limetokana na wosia wa Maalim Seif

    Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema jina walilompelekea Rais Hussein Mwinyi kwa ajili ya uteuzi wa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar limetokana na wosia aliouacha Maalim Seif mwenyewe. Zitto Kabwe amesema mtu huyo anaenda kumsaidia sana Rais Mwinyi na pia atawaunganisha wana...
  5. Idugunde

    Zitto Kabwe, Pemba sio Kigoma

    Jana tumeshuhudia maziko ya Mwanasiasa mkongwe yaliyofanyika huko Pemba Zanzibar kijijini Nyali Mtambwe na kuona jinsi wananchi wa huko walivyokuwa na simanzi nzito mithili ya kuwa wameondokewa na mfalme wao. Na wengi walionekana kama kuwa sasa ndio basi tena hakuna wa kuja kuwapigania. Maana...
  6. M

    Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

    Nimeshangazwa na majibu ya mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe aliyoyatoa kwenye mtandao wa twitter. Zitto alikuwa akimjibu mwananchi mmoja aliyekuwa akionyesha frustrations zake juu ya uamuzi wa chama cha ACT kujiunga na Serikali ya CCM huko Zanzibar katika kile kinachoitwa...
  7. M

    Kisiasa, Zitto Kabwe yupo wapi?

    Ni vigumu sana kuamini kwamba Zitto Kabwe ambaye wiki chache zilizopita alikuwa mshirika wa Chadema leo ni mshirika wa CCM. Nadhani maneno yangu hayatakuwa na nguvu kama hii picha. Najiuliza maswali mengi kama watanzania wengine, ila majibu sipati. Zitto atawaambia nini watanzania kuanzia sasa...
  8. S

    Zitto Kabwe, tunaomba status ya madeni yako na utueleze unataraji kuyalipa vipi nje ya ubunge

    Nakumbuka uliwahi kututangazia mali na madeni yako kulingana na katiba ya chama chenu cha ACT inavyowataka. Binafsi leo hii nakuomba utueleze hali ya madeni yako, na ikiwezekana utueleze unatarajia kuyalipa vipi nje ya ubunge in case bado unayo. Vile vile utueleze kama uliingia madeni mapya...
  9. Mzito Kabwela

    Zitto Kabwe mpishe Maalim Seif awe kiongozi wa chama

    Hii ni baada ya ACT Ku-Surrender kwa ma CCM. Maalim kwa sasa na kwa nafasi yake anatakiwa ndio awe KC na Zitto atafute nafasi nyingine. Sababu iliyo wazi kabisa ni kuwa Mara baada ya Zitto kukubali kuungana na Seif, ni wazi kabisa Zitto alikubali "kukiuza" chama kwa Seif na kundi lake. Sio...
  10. MsemajiUkweli

    Je, Zitto Kabwe alijisahau na kuanza kuung'ata mkono unaomlisha?

    Kwa mtu anayezijua vizuri siasa za nchi hii lazima atakuwa anajua kuwa bila ''mkono'' wa CCM, Zitto Kabwe asingekuwa hapa alipo kisiasa! Ukweli huu ndio ambao ulimfanya Zitto Kabwe kutoaminika ndani ya chama chake cha mwanzo (CHADEMA) mpaka chama kikaamua kumfukuza uanachama! Malezi yake ya...
  11. Roving Journalist

    Rais Dkt. Mwinyi amteua Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Maalim Seif Shariff Hamad, kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar kuanzia leo Disemba 06, 2020. ===== Taarifa kwa vyombo vya Habari Kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka...
  12. Mwl.RCT

    ACT-Wazalendo yaridhia kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Vyombo vya Uwakilishi

    ADO SHAIBU: Kamati kuu ilikutana jana jijini Dar es Saalam Tarehe 5 Disemba katika hoteli ya Onomo ambayo iko Posta kwa ajili ya kutafakari hali ya kisiasa inayoendelewa nchini kwetu. Tumetoka katika uchaguzi uliofanyika tarehe 28 ya mwezi Oktoba, uchaguzi ambao ulitawaliwa na uchafuzi mkubwa...
  13. mugah di matheo

    Zitto Kabwe: Kesho Mahakama inatoa amri ya kuachiwa Mazrui

    "Polisi wanajibu hoja, kesho tunatarajia mahakama itatoa Amri ya kuachiwa Nasoro Mazurui. Sisi viongozi wa ACT- Wazalendo hatutalala hadi tuhakikishe viongozi wote waliokamatwa kwa hila wameachiliwa" Zitto Kabwe Amenukuliwa Zitto kabwe kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo kupitia ukurasa rasmi wa...
  14. Q

    Zitto Kabwe: Hadi sasa wafuasi 13 wa ACT-Wazalendo wamepoteza maisha kwa vurugu za uchaguzi

    Kwa upande wetu @ACTwazalendo na kutokana na Taarifa tulizokusanya mpaka sasa: Wananchi 13 wameuawa kwa kupigwa risasi na mabomu katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, Watu 130 Wamejeruhiwa, Watu 120 Wamekamatwa na Polisi, mtu Mmoja Amebakwa na Watu 14 Wametekwa Akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chama...
  15. Cannabis

    Zitto Kabwe akamatwa na Polisi baada ya kwenda kuwaona viongozi wa vyama vya upinzani waliokamatwa na Polisi

    Kiongozi wa Chama, cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na kushikiliwa na Jeshi La Polisi baada ya kufika Kituo cha Polisi Oysterbay kuwaona Viongozi wa Vyama vya Upinzani waliokamatwa tangu Juzi kwa ajili ya kuandaa maandamano ya amani ya kudai Uchaguzi mpya na Tume Huru ya Uchaguzi...
  16. Q

    Polisi wavamia Ofisi za ACT-Wazalendo Vingunguti alizokuwepo Zitto Kabwe

    Jeshi la Polisi @tanpol wamevamia Ofisi ya ACT -Wazalendo Kata ya Vingunguti ili kumkamata Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe aliyekuwa Ofisini hapo kuratibu Maandamano kwa Njia ya Buguruni kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi ===
  17. IslamTZ

    Tumeumia, lakini chonde chonde tusiandamane...

    Hatimaye uchaguzi mkuu wa 2020 umekamilika na kutuletea matokeo ya kushangaza. Sio siri kuwa uchaguzi haukuwa huru, haukuwa wa haki wala haukuwa wa wazi. Ushahidi wa uhalifu uliofanywa dhidi ya Demokrasia ulikuwa mwingi na kila mahali. Hakika, watu wengi wameumizwa kwa yaliyofanyika. Baada ya...
  18. CHADEMA

    Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo Wapinga Matokeo, Wataka Uchaguzi Urudiwe, pia NEC na ZEC zivunjwe

    UPDATES: 05:55 Asubuhi: Viongozi wa vyama vya ACT na CHADEMA wakiongozwa na Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Zitto Kabwe wanaingia kwenye ukumbi ambapo watafanya mkutano na waandishi wa habari. MNYIKA: Viongozi wakuu wa vyama vyetu tumekuwa kwenye vikao vya mashauriano na vimeendelea leo asubuhi...
  19. Q

    Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe apoteza jimbo la Kigoma Mjini

    Mgombea wa CCM jimbo la Kigoma mjini, Kilumbe Ng'enda ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 27, 688 huku Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo akipata kura 20, 600. Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi, jimbo hilo Mwailwa Pangani amesema kura zilizopigwa ni 50268. Zitto: Licha ya kuingiza...
  20. mugah di matheo

    Zitto Kabwe: Wanashangilia Meli ya DRC, Kigoma hamna meli toka Uhuru

    Amesema meli iliyopokelewa leo kwa mbwembwe na wanaCCM si ya Tanzania bali ni mali ya DRC. Ameongeza kuwa ni aibu Tanzania kutokuwa na meli na kutegemea ya DRC Chanzo: Zitto kabwe on all social media
Back
Top Bottom