Kwa jicho la karibu hauwezi kuiona faida, lkn kwa wenye jicho la mbali tunaona kabisa jamaa anapata faida lukuki kupitia thread zake.
Iko hivi, hapa JF kuna wasomaji mbali mbali wa kimya kimya wanaotumia ID fake kwa sababu za kiusalama, heshima zao kisiasa, kijamii nk. Kuna wanasiasa wa vyama vyote, kuna viongozi wa serikali nk. Sasa kuna mtu amefanikiwa kuwakamata baadhi ya wanasiasa au viongozi wa serikali kupitia thread zake.
Mfano kuna mtu anaweza kuwa analipwa na Mbowe kimya kimya kupitia inbox yake ili awe tu anamuandika yeye (Mbowe) na chama chake vizuri kwa lengo la kukikuza na kukitangaza chama hapa JF. Pia mfano kuna mtu anaweza kuwa analipwa kimya kimya kupitia inbox yake na Kinana ili awe anaandika thread za kumsifu sifu (Kinana) na chama chake kwa lengo la kukitangaza chama hicho. Mtu wa aina hii anaweza kuwa na ID mbili hadi 10 akijua kwamba katika hizo ID 10 au 5 kuna ID 2 au 3 zinazompa ugali kupitia watu fulan hapa JF. Hii haujalishi anaemsifu ni chama gani, ilimradi mkono uende kinywani.
Ni sawa sawa na mcheza mpira yeye anaweza kuwa mpenzi wa Yanga damu lkn akasajiliwa na kuichezea Simba tena akafunga Yanga magoli vilevile, maana atachoangalia yeye ni pesa kutoka kwa waliomsajili na sio swala la timu anayoipenda.
Narudia tena hizo ID mbili ukizifutilia kwa makini utaona moja inatumika kuimsafisha Mbowe, Sugu na chama chao, na nyingine inatumika kumsafisha raisi Samia, Dr Tulia na serikali na chama chao kwa ujumla. Kikubwa ujue kucheza na timing tu.