11 wafariki dunia, 44 wajeruhiwa kwa ajali ya basi Mbeya

11 wafariki dunia, 44 wajeruhiwa kwa ajali ya basi Mbeya

Watu 14 wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa baada ya basi la abiria la kampuni ya AN Coach kupata ajali leo Septemba 6, 2024 wilayani Chunya, mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi katika Kijiji Cha Lwanjiro, wakati basi hilo lilipokuwa safarini likitokea Mbeya kuelekea Tabora.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Chunya, John Gungumka amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kuongeza kuwa majeruhi sita kati ya 29 wako katika hali mbaya.

✍ Kakuru Msimu

#AzamTVUpdates
 
Duh aisee na huko kenya wanafunzi 14..siku ya leo ni mbaya sana pole kwa wafiwa wote ..tuendelee kufuatilia kwa makini huenda na wewe au mimi nikawa nimefiwa na mtu wa karibu kwenye ajali hio
 
Mungu azilaze roho za marehem mahali pema
FB_IMG_1725628824114.jpg
 
Sijui kwa nini hio kanda ina wingi wa ajali kiasi hicho!
Pole nyingi kwa walio athirika, taarifa hizi zinakuwa ni nyepesi kwa wengine ila wanahusika ni nzito mno.
Ni miuondo mbinu mibovu sana, ndugu yangu hata hivyo ni Mungu tu anasaidia kwa hizi route za Mbeya-Tabora
 
Wapumzike kwa amani waliotangulia, pole sana kwa familia zao.....

Majeruhi wapone haraka
 
Tumuombe mchina bus za nchi hii aweke speed mwisho 80 baasi
 
Miundo mbinu finyu
Tutalaumiana lakini mzizi wa tatizo ni miundombinu mibovu, barabara zina ramani ya mkoloni enzi magari machache, leo hii watu wengi, vyombo vingi barabara zinatakiwa kua na upana wa kueleweka sio kupishana Kwa kuchunguliana,
 
Kuna wale jamaa zetu hawakawii kutuambia kuongezeka kwa ajali ni viashiria vya Taifa kuendelea, hawako serious maana waliweza hata kusema yule jamaa eti alienda polini kujisaidia huku kukiwa na tuhuma nzito zilizohitaji maelezo yaliyoshiba.

Wapumzike kwa amani Marehemu wote na majeruhi wapone kwa haraka, amen.
 
Ujinga wetu kama kawaida unazidi kuchukua mamilioni ya watu na wala hatujaali kama sisi tuwajinga na tunapaswa kuupiga vita ujinga.
 
Back
Top Bottom