11 wafariki dunia, 44 wajeruhiwa kwa ajali ya basi Mbeya

11 wafariki dunia, 44 wajeruhiwa kwa ajali ya basi Mbeya

Mwenye takwimu za idadi ya ajali before na after initiative za usalama barabarani zilioanzishwa na polisi na serikali kwa ujumla atupie humu
 

Watu 11 wamepoteza maisha na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya A-N Coach kupata ajali katika eneo la Luanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini.​
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Ijumaa, Septemba 6, 2024 baada ya basi hilo lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora kupinduka wakati likilikwepa lori, kisha kutumbukia mtaroni.

Mganga wa Mkuu wa Hosptali ya Wilaya ya Chunya, Dk Darson Andrew amethibitisha kupokea idadi ya hiyo na vifo huku akieleza kati ya majeruhi 44 wanne wana hali mbaya na watapewa rufaa kupelekwa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.


Pia soma Mbeya: Basi la Kampuni ya Shari lapata ajali Mbarali, Watu 9 wapoteza maisha, Polisi wamshikilia Dereva
Napendekeza madereva wa magari ya abiria wawe na elimu angalau ya kidato cha nne na ufaulu mzuri
 
Napendekeza madereva wa magari ya abiria wawe na elimu angalau ya kidato cha nne na ufaulu mzuri
Ni ajali tu na mda wao ulikuwa umefika lakini kama ni elimu dereva aliefariki anaelimu za zaid, kama ntakuwa sijasajau alisomea Malaysia na alikuwa mbobevu katika ufundi pia na uendeshaji
 
Back
Top Bottom