Mbona content ya alichoongea ni ya kawaida tu na ilieleweka vizuri tu. Ilikuwa ni ya kisiasa ya upinzani, aliitoa kwa kistaarabu na bila kuweka uwongo. Alikikosoa chama chake cha ccm na serikali yake kwa kuendesha baadhi ya mambo kihuni.
Kwa wenye akili hawakutakiwa kujadili hiyo content bali ktafakari dhamira ya hiyo content. Wenye akili waligundua kuwa dhamira yake ya kuacha kazi ya umma ghafla ni kwenda kusaka kazi ya ubunge kama wafanyavyo wakuu wa mikoa na watumishi wengine wa umma kipindi hiki. Wenye akili waligundua kwamba ombi lake la kuacha kazi kwenda kusaka ubunge kama ambavyo wakuu wa mikoa walivyokuwa wanafanya, lilikataliwa na mamlaka ya uteuzi. Hivyo akalazika kufanya alichokifanya akijua kuwa sasa hataweza kuusaka huo ubunge kupitia chama chake cha ccm. Hivyo kaanza siasa ya upinzani. Bila shaka atajiunga na moja wapo wa vyama hivyo vya upinzani kuusaka ubunge. Na bila shaka hivi karibuni ccm watamtimua kwenye chama chao.
Watanzania wanampenda na wanamkaribisha kuja kuwa mbunge wao. Hana haja ya kuogopa na kujificha huko Florida. Hajafanya kosa lo lote. Arudi aimarishe siasa za upinzani kwa faida ya taifa letu.