Yesu alikuja kabla ya Mtume Muhammad(rehma na amani zimfikie). Kwa hiyo Injili haiwezi ikazungumzia maisha ya Muhammed(rehma na amani zimfikie) kwani alikuwa bado hajaletwa duniani. Isipokuwa Yesu alisema kuwa Mtume Muhammad(rehma na amani zimfikie) atakuja badala ya yeye kuondoka. Soma John 16:7
"Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu."
Huyo Msaidizi ni Muhammed(rehmana amami zimfikie). Katika Bible ya Hebrew wanemtaja kwa jina lake kabisa. Lakini katika hii tafsiri ya kiswahili wameandika Msaidizi. Fuatilia.
Sababu ya Quran kumzungumzia Yesu kwa wingi ni kwa Sababu ni mtume wetu aliyepita kama walivyo zungumziwa mitume yote iliyopita, Moses, Abraham,Adam,Noah na wengine wengi. Sababu ingine kuwa Yesu anazungumziwa kwa Quran ni kwamba Yesu mwenyewe alisema kwenye Biblia kuwa huyo Msaidizi atamzungumzia. Soma John 16:26
"Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia".
Kwa hiyo yathibitisha kuwa Quran ni kitabu cha kweli na Mtume Muhammad(rehma na amani zimfikie) ni mtume wa kweli hata Yesu alimbashiria ujaji wake. Kama Quran ni kitabu cha Uongo kwanini Mtume Muhammad(rehma na amani zimfikie) asijizungumzie yeye mwenyewe tu?? Tafakari. Haya ni maneno ya Mungu na Mungu anawapenda watumwa wake.